Saturday, September 1, 2012

Huu Ndio baadhi ya usajili wa dakika za mwisho.

 Edinson Cavan amesaini mkataba mpya wa kuendelea kuichezea Napoli na kuzima uvumi wa kutaka kujiunga na Chelsea.

 Nigel De Jong ameondoka rasmi Manchester City na kujiunga na AC Milan kwa ada ya uhamisho ya £3.4million


 Gael Kakuta ameenda kwa mkopo Vitesse Arnhem kutokea Chelsea

 Yossi Benayoun amekamilisha uhamisho wa kujiunga na West Ham kwa mkopo wa mwaka mmoja.

 Liverpool wamepigwa bao na Tottenham baada ya Clint Dempsey kujiunga na Spurs dakika za mwisho kutoka Fulham kwa ada ya uhamisho wa £6million.

 Stephen Mbia yupo Loftus Road akikamilisha vipimo vya afya kwa ajili ya kujiunga na QPR.



 Matija Nastasic amekamilisha uhamisho wake kutoka Fiorentina na kujiunga na Mannchester City, na anakuwa mchezaji wa 3 kujiunga na mabingwa hao wa England kwenye siku ya mwisho ya usajili. Wakati huo huo Javi Garcia anafanya vipimo vya afya kwa ajili ya kukamilisha uhamsiho wake kutoka Benfica kwenda City.




Nicklas Bendtner amehama Arsenal na kwenda kujiunga na Juventus ya Italia


Scott Sinclair amekamilisha uhamisho wake kutoka Swansea na kuhamia kwa mabingwa wa England Man City

 Andy Carroll amejiunga na West Ham kwa mkopo wa mwaka mzima



 Rafael Van Der Vaart amejiunga na Schalke akitokea Tottenham Hotspur

 Mchezaji wa kimataifa wa Brazil Douglas Maicon amesajiliwa kutoka Inter Milan kwenda Manchester City

 Pablo Hernandez amejiunga na Swansea City akitokea Valencia ya Spain







 Javi Garcia akiingia kwenye hosptali ya Bridge water kwa ajili ya kufanya vipimo vya afya baada ya klaby yake ya Benfica kukubaliana ada ya uhamisho na City - £16MILLION


 Charlie Adam amejiunga na Stoke City City akitokea Liverpool kwa ada ya £4MILLION

 Hatimaye Dimitar Berbatov amehamia rasmi Fulham kutoka Manchester United kwa ada ya £5million
 Ryan Babel mchezaji wa zamani wa Liverpool, amerudi timu yake ya utotoni Ajax akitokea Hoffenheim

 Golikipa Hugo Lloris wa Lyon amekamilisha vipimo vya afya na Tottenham na muda mchache na amesaini mkataba wa miaka minne kujiunga klabu hiyo kwa ada ya uhamisho wa £13million.

 Micheal Essien amethibitishwa kuwa ataungana tena na kocha Jose Mourinho, baada ya Chelsea kuthibitisha kwamba atajiunga na Real Madrid kwa mkopo wa mwaka mmoja.


Lassana Diara, mchezaji wa zamani wa Chelsea, Arsenal na Portsmouth, amejiunga na Anzhi Makhachkhala kutoka Real Madrid

No comments:

Post a Comment