Friday, December 21, 2012

BPL: KURINDIMA WIKIENDI, ARSENAL KUANZISHA DW STADIUM!

TIMU ZASAKA USHINDI KABLA MECHI MFULULIZO X-MASI, MWAKA MPYA!
+++++++++++++++++++++++++++
RATIBA:
Jumamosi 22 Desemba 2012
[SAA 9 Dak 45 Mchana]
Wigan v Arsenal
[SAA 12 Jioni]
Man City v Reading
Newcastle v QPR
Southampton v Sunderland
Tottenham v Stoke
West Brom v Norwich
West Ham v Everton
[SAA 2 na Nusu Usiku]
Liverpool v Fulham
Jumapili 23 Desemba 2012
[SAA 10 na Nusu Jioni]
Swansea v Man United
[SAA 1 Usiku]
Chelsea v Aston Villa
+++++++++++++++++++++++
AMESHATAMKA kuwa zawadi yake bora kwa Krismasi ni kubakia Pointi 6 mbele kileleni mwa Ligi Kuu England wakielekea kwenye Mechi mfululizo za wakati wa Krismasi na Mwaka mpya na Sir Alex Ferguson ataisafirisha Timu yake Manchester United kwenda huko Wales kucheza na Swansea City hapo Jumapili kulinda pengo hilo.
Lakini Ratiba ya Mechi za Ligi itaanza Jumamosi kwa Arsenal kucheza ugenini DW Stadium na Wigan na baadae Siku hiyo zitafuata Mechi 7 ikiwemo ya Mabingwa watetezi Man City kucheza kwao Etihad na Timu ya mkiani Readimg
+++++++++++++++++++++++++++
MSIMAMO:
=Tofauti ya Magoli inatajwa kwa Timu zilizofungana Pointi
1 Man United Mechi 17 Pointi 42
2 Man City Mechi 17 Pointi 36
3 Chelsea 29 [Tofauti ya Magoli 11]
4 Tottenham Mechi 17 Pointi 29 [Tofauti ya Magoli 5]
===============
5 Arsenal Mechi 17 Pointi 27 [Tofauti ya Magoli 13]
6 Everton Mechi 17 Pointi 27 [Tofauti ya Magoli 7]
7 WBA Mechi 17 Pointi 27 [Tofauti ya Magoli 3]
8 Norwich Mechi 17 Pointi 25
9 Stoke Mechi 17 Pointi 24 [Tofauti ya Magoli 2]
10 Swansea Mechi 17 Pointi 23 [Tofauti ya Magoli 4]
11 West Ham Mechi 17 Pointi 23 [Tofauti ya Magoli 1]
12 Liverpool Mechi 17 Pointi 22
13 Fulham Mechi 17 Pointi 20
14 Aston Villa Mechi 17 Pointi 18
15 Newcastle Mechi 17 Pointi 17
16 Sunderland Mechi 17 Pointi 16
17 Southampton 15 [Tofauti ya Magoli -10]
===============
18 Wigan Mechi 17 Pointi 15 [Tofauti ya Magoli -14]
19 QPR Mechi 17 Pointi 10
20 Reading Mechi 17 Pointi 9
+++++++++++++++++++++++
BPL_LOGOMechi ya mwisho Jumamosi ni ile ya Anfield kati ya Liverpool na Fulham.
Jumapili zipo Mechi mbili kati ya Swansea na Man United na Chelsea v Aston Villa.
Vinara Man United wapo kileleni Pointi 6 mbele baada ya kushinda Mechi zao 10 kati ya 11 walizocheza mwisho lakini Man City, kwa vile wanacheza Jumamosi Uwanjani kwao Etihad kabla ya Man United wanaocheza Jumapili, wakishinda wanaweza kukata pengo hilo na kuwa Pointi 3.
Man City watakuwa nyumbani kwao kwa mara ya kwanza tangu wafungwe hapo na Man United Desemba 9 Bao 3-2 na kupoteza Rekodi yao ya kutofungwa nyumbani kwa Miaka miwili na pia kutofungwa kwenye Ligi Msimu huu lakini huenda safari hii wakapata ubwete maana Reading wako mkiani na wamefungwa Mechi 6 mfululizo.
Arsenal, baada ya kuishindilia Reading, wamepaa na kukamata nafasi ya 5 na wako ugenini kucheza na Wigan ambayo imevutwa chini na kuwa moja ya Timu 3 za mkiani baada ya kufungwa Mechi 3 na sare moja katika Mechi zao 4 za mwisho.
Baada ya kuchapwa kwao Anfield na Aston Villa katika Mechi yao ya mwisho, bila shaka Meneja wa Liverpool, Brendan Rodgers, atawashikia bakora Wachezaji wake wasifungwe na Fulham, ambao hata hivyo, hawana rekodi nzuri Uwanjani Anfield, na wameshinda Mechi moja tu kati ya 9 walizocheza mwisho.
Newcastle wapo nyumbani St James Park lakini, baada ya kuanza vyema, wameporomoka hadi nafasi ya 15 wakiwa na Pointi 17 kwa Mechi 17 na wanacheza na QPR ambayo juzi ndio iliambua ushindi wao wa kwanza Msimu huu chini ya Meneja wao mpya Harry Redknapp ambae itakuwa Mechi yake ya 5 baada ya kwenda sare 3 na kushinda hiyo moja majuzi walipoifunga Fulham 2-1.
Tottenham wapo nafasi ya 4 baada ya kushinda Mechi zao 4 kati ya 5 walizocheza mwisho na safari hii wapo nyumbani White Hart Lane kucheza na Stoke City ambao hawajafungwa kati Mechi zao 7 za mwisho.
Sare 8 kati ya Mechi 11 zimewafanya Everton waporomoke toka nusu ya juu ya Msimamo wa Ligi lakini, hata hivyo, wapo Pointi mbili tu nyuma ya Tottenham ambao wamekamata nafasi ya 4 lakini watakuwa Upton Park kucheza na West Ham ambayo haina masihara wakiwa Uwanjani kwao.
WBA wanacheza na Norwich na Timu zote hizi zimeonyesha Soka safi sana.
Mechi nyingine ya msisimko ni ile kati ya Timu zinazosuasua Southampton na Sunderland na ushindi ni muhimu kwa kila Timu.
+++++++++++++++++++++++++++
RATIBA MECHI ZIJAZO:
Jumatano 26 Desemba 2012
[SAA 12 Jioni]
Arsenal v West Ham
Everton v Wigan
Fulham v Southampton
Man United v Newcastle
Norwich v Chelsea
QPR v West Brom
Reading v Swansea
Sunderland v Man City
[SAA 2 na Nusu Usiku]
Aston Villa v Tottenham
[SAA 4 Dak 45 Usiku]
Stoke v Liverpool

No comments:

Post a Comment