Mara ya mwisho Timu hizi kukutana
ilikuwa ni Mwaka 2010 kwenye Mechi ya ufunguzi ya Chalenji Cup na
Chipolopolo kushinda Bao 1-0.
Leo, Chipolopolo, wataongozwa na Nahodha
wao Christopher Katongo, ambae juzi alitunukiwa Tuzo ya Mchezaji Bora
wa Afrika na BBC, Shirika la Utangazaji la Uingereza.
Stars, ambao wako chini ya Kocha toka
Denmark, Kim Poulsen, wataingia kwenye Mechi hii bila ya Wachezaji wao
wawili wanaocheza huko TP Mazembe, Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu
ambao wameripotiwa kuwepo Dar es Salaam lakini ni majeruhi.
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
AFCON 2013
MAKUNDI:
KUNDI A: South Africa, Cape Verde, Morocco, Angola
KUNDI B: Ghana, DR Congo, Niger, Mali
KUNDI C: Zambia, Ethiopia, Nigeria, Burkina Faso
KUNDI D: Ivory Coast, Togo, Tunisia, Algeria
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
Chipolopolo leo wataongezewa nguvu baada ya kuwasili kwa Kocha wao Mkuu Herve Renard ambae alikuwa Accra, Ghana akipokea Tuzo toka
CAF ya kuwa Kocha Bora wa Afrika ambako pia Zambia ilitajwa kuwa ndio
Timu Bora Afrika kwa 2012 baada ya kutwaa Ubingwa wa Afrka, AFCON 2012,
huko Gabon Mwezi Februari Mwaka huu.
Mwezi Januari, Chipolopolo watakuwa huko
Afrika Kusini kuanza utetezi wa Ubingwa wao wa Afrika kwenye michuano
ya Kombe la Mataifa Afrika, AFCON 2013, itakayochezwa kuanzia Januari 19
HADI Februari 10.
Taifa Stars wao wapo kwenye
vinyang’anyiro vya Mechi za Mchujo za CHAN, Kombe la Mataifa ya Afrika
kwa Wachezaji wa ndani wa Afrika, na Kombe la Dunia la 2014, na Mechi
hizo watazicheza Mwakani.
Viingilio katika mechi hiyo vitakuwa Sh.
5,000 kwa viti vya rangi ya bluu na kijani, Sh. 7,000 kwa viti vya
rangi ya chungwa, Sh. 10,000 kwa VIP C, Sh. 20,000 kwa VIP B wakati VIP A
itakuwa Sh. 30,000.
Tiketi zilianza kuuzwa tangu jana kwenye
vituo vya Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Uwanja wa Uhuru, Mgahawa
wa Steers ulioko Mtaa wa Ohio na Samora, Sokoni Kariakoo, kituo cha
mafuta cha Ubungo OilCom na Dar Live Mbagala.
No comments:
Post a Comment