Tuesday, December 25, 2012

UEFA CHAMPIONZ LIGI: BINGWA ni BAYERN au DORTMUND!!

KOCHA HITZFELD ATABIRI KLABU ZA GERMANY KUTAMBA!!
 
UEFA_CHAMPIONZ_LIGI_LOGO-BOMBAZKOCHA aliewahi kutwaa Ubingwa wa Ulaya akiwa na Bayern Munich, Ottmar Hitzfeld, ana imani kuwa Msimu huu Klabu za Germany Bayern Munich na Borussia Dortmund zinaweza kutwaa UEFA CHAMPIONZ LIGI.

Mabingwa wa Germany, Borussia Dortmund, vinara wa Bundesliga, Bayern Munich na Schalke, ndizo Klabu za Germany ambazo zipo kwenye Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA CHAMPIONZ LIGI ambayo Mechi zake zitaanza kuchezwa Februari 12 Mwakani.

Hitzfeld, Mwenye Miaka 63 na ambae sasa ni Kocha wa Timu ya Taifa ya Uswisi, amesema: “Schalke hawana mtiriko mzuri wa ushindi lakini naamini Bayern na Dortmund wanaweza kutwaa Ubingwa. Ligi ya Ujerumani ni imara.”

Kocha huyo mkongwe aliwahi kuzifundisha Borussia Dortmund Mwaka 1997 na Bayern Munich Mwaka 2001 ilipotwaa Ubingwa wa Ulaya.

Hitzeld pia amesema kazi yake kubwa kwa sasa ni kuifikisha Uswisi kwenye Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2014 huko Brazil.
+++++++++++++++++++
RATIBA:

[Mechi zote kuanza Saa 4 Dak 45 Usiku]

Jumanne 12  Februari 2013
Celtic v Juventus
Valencia v Paris St Germain

Jumatano 13  Februari 2013
Real Madrid v Manchester United
Shakhtar Donetsk v Borussia Dortmund

Jumanne 19  Februari 2013
Arsenal v Bayern Munich
FC Porto v Malaga

Jumatano 20  Februari 2013
Galatasaray v FC Schalke
AC Milan v Barcelona

Jumanne 5 Machi 2013
Borussia Dortmund v Shakhtar Donetsk
Man United v Real Madrid

Jumatano 6 Machi 2013
Juventus v Celtic
Paris St George v Valencia

Jumanne 12 Machi 2013
Barcelona v AC Milan
Schalke v Galatasaray

Jumatano 13 Machi 2013
Bayern Munich v Arsenal
Malaga v FC Porto
+++++++++++++++++++

No comments:

Post a Comment