Monday, December 31, 2012

UHAMISHO: CHELSEA KUNASA KADHAA LAKINI BA…??

>>STURRIDGE KUTUA LIVERPOOL??
>>NEWCASTLE YAMPATA BEKI WA KIMATAIFA WA FRANCE!!

BENITEZ-CHELSEAULE mpango wa Demba Ba kuhamia Chelsea unaelekea umekwama baada ya kuibuka tetesi kuwa Wawakilishi wa Mchezaji huyo wa Newcastle hawakufikia makubaliano na Chelsea lakini zipo ripoti nyingine kuwa Chelsea wako mbioni kuwanasa Kiungo wa Metalist Kharkiv, Taison, na Mchezaji wa Corinthians Paulinho.

DEMBA_BA
Chelsea walikuwa na nia ya kumnunua Demba Ba ili awe anatoa sapoti kwa Straika wao Fernando Torres baada ya kukosa kumchukua Radamel Falcao wa Atletico Madrid katika Dirisha la Uhamisho la Januari baada ya Klabu hiyo ya Spain kung’ang’ania kuwa hawezi kuhama sasa labda mwishoni mwa Msimu.

Kuhusu Demba Ba, kikwazo kikubwa ni kuwa Meneja wa Newcastle, Alan Pardew, hapendezewi kumuuza Straika ambae amefunga Bao 13 kwenye Ligi na pia Mkataba wa Mchezaji huyo una kipengele kuwa Uhamisho wowote ule lazima uambatane na Malipo ya Pauni Milioni 7.5.

Na habari toka ndani ya Klabu ya Chelsea zimedokeza kuwa Liverpool watailipa Chelsea Pauni Milioni 12 ili kumnunua Daniel Sturridge ambae imeripotiwa alishapimwa afya yake huko Liverpool na Uhamisho rasmi unasubiri Januari 1 wakati Dirisha la Uhamisho litakapofunguliwa.

Nae Meneja wa muda wa Chelsea Rafa Benitez amekataa kuzungumza lolote kuhusu Ba pale aliposema: “Hatuzungumzii shughuli zetu hadharani. Yeye ni Mchezaji wa Klabu nyingine na huwa siongelei Wachezaji wengine!”

NEWCASTLE KUMSAINI MATHIEU DEBUCHY TOKA LILLE

Newcastle imefikia makubaliano kumsaini Beki wa Kimataifa wa France, Mathieu Debuchy, kutoka Klabu ya Ufaransa, Lille.

Beki huyo wa kulia mwenye Miaka 27 alichezea Mechi zote 4 za France kwenye EURO 2012 na inasadikiwa Ada yake ya Uhamisho ni Pauni Milioni 5.

Debuchy anakuwa Mchezaji wa pili kusainiwa na Newcastle kutoka Lille hivi karibuni baada ya Klabu hiyo pia kumchukua Kiungo Yohan Cabaye Juni 2011.

No comments:

Post a Comment