Sunday, December 30, 2012

WALCOTT KUBAKI ARSENAL, NANI HAENDI KOKOTE, REFA MATATANI…!!

WENGER_MASHAKANIWALCOTT KUBAKI ARSENAL? NANI HAENDI KOKOTE! REFA MATATANI…!!
 
HUKU kukiwa na hatari ya kumpoteza Winga wao Theo Walcott bila kupata Senti hata moja ifikapo mwishoni mwa Msimu, Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, amesema bado wanamatumaini Mchezaji huyo atakubali kusaini Mkataba mpya na huko Old Trafford, Sir Alex Ferguson, ametamka Nani hauzwi Mwezi Januari na wakati huo huo, Refa alieboronga atachunguzwa na FA.


THEO WALCOTT: ARSENAL na ARSENE WENGER WANA MATUMAINI!

Arsene Wenger amesema Hetitriki ya Theo Walcott aliyopiga jana Arsenal ilipoitwanga Newcastle 7-3 haina uzito wowote kwenye mustabali wake Klabuni hapo ambapo kuna mvutano huku Mchezaji huyo akigoma kukubali Mkataba mpya wakati Mkataba wake wa sasa unamalizika mwishoni mwa Msimu na kuanzia Januari Mosi yuko huru kuongea na Klabu nyingine zinazomtaka.

Wenger ametamka: “Nia yangu ni asaini Mkataba mpya. Yeye ni Mchezaji wa hapa na hata kama angecheza vibaya na Newcastle bado sisi tunataka aongeza Mkataba!”

Walcott, Miaka 23, amefunga Bao 14 Msimu huu na 4 ni katika Mechi 3 ambazo amechezeshwa kama Straika wa Kati.

Arsenal ilimsaini Walcott akiwa na Miaka 16 kutoka Southampton Mwaka 2006 kwa Dau la Pauni Milioni 5 ambalo lilipanda hadi Pauni Milioni 12.5.

Akiongea mara baada ya Mechi na Newcastle, Walcott alisema: “Mazungumzo na Arsenal yanaeendelea na nina hakika mambo yatakamilika hivi karibuni.”

NANI HAUZWI!

Bosi wa Manchester United Sir Alex Ferguson amesisitiza Nani hatauzwa Dirisha la Uhamisho likifunguliwa Mwezi Januari.

Tangu awe hana namba ya kudumu Msimu huu, kulizuka uvumi kuwa Mchezaji huyo kutoka Ureno yuko mbioni kuuzwa lakini Ferguson amepuuzia hayo na kusema: “Hatutamwachia aondoke. Tunamhitaji Nani. Kwanini tumuachie aondoke??”

Aliongeza: “Bado Mkataba wake una Mwaka mmoja na nusu. Yeye anatupa kitu tofauti na Wachezaji wengine hapa. Ana kipaji kikubwa. Bahati mbaya ameumia na tumempeleka Dubai kupumzika na apone. Tunatarajia atarudi Uwanjani katikati ya Januari.”

REFA MATATANI!!

REFA Mick Russell yupo mashakani na FA, Chama cha Soka England, baada ya kutomtoa nje Staa wa Sheffield Wednesday Jeremy Helan licha ya kumpa Kadi za Njano mbili kwenye Mechi waliyotoka sare 0-0 na Huddersfield.

+++++++++++++++++++++++

MAKOSA ya MAREFA WENGINE:

STUART ATTWELL: Mwaka 2008, aliwapa Reading Goli dhidi ya Watford badala ya Kona na akaondolewa kwenye Listi ya Marefa wa Mechi kubwa.

GRAHAM POLL: Alimpa Mchezaji wa Croatia Josip Simunic Kadi za Njano 3 katika Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2006 kabla kumtoa nje kwa Kadi Nyekundu katika Mechi na Australia.

+++++++++++++++++++++++
Tukio hilo liliwapandisha hasira Huddersfield waliotaka Refa huyo apewe adhabu kali.

Helan, ambae yuko kwa mkopo Sheffield Wednesday akitokea Manchester City, alipewa Kadi ya Njano ya kwanza katika Dakika ya 9 kwa kujiangusha kwa makusudi na ya pili katika Dakika ya 26 kwa kucheza Faulo.

Licha ya Wachezaji wa Huddersfield kulalamika kwa Refa Mick Russell wakitaka Helan atolewe, Refa huyo alianzisha tena mpira bila kumtoa ikimaanisha Helan asingeweza kutolewa tena.

Mwenyewe Helan amesema: “Ilishangaza! Lakini mie sio Refa, nilicheza Dakika 90 na nafurahia kwa hilo!”
Baadae Refa Russell alikiri kosa lake na kudai alikosea kuandika Namba wakati akitoa Kadi za Njano.

Chama cha Marefa, PGMO [Professional Game Match Officials Limited] na FA zimesema uchunguzi kuhusu uchezeshaji wa Refa Russell.

No comments:

Post a Comment