Tuesday, January 1, 2013

MWAKA MPYA, VINARA MAN UNITED WAANZA KWA USHINDI 4-0 UGENINI!

BPL_LOGO
RATIBA/MATOKEO:  

Jumanne 1 Januari 2013
West Brom 1 Fulham 2
Man City 3 Stoke 0
Swansea 2 Aston Villa 2
Tottenham 3 Reading 1
West Ham 2 Norwich 1
Wigan 0 Man United 4



[SAA 2 na Nusu Usiku] 
Southampton v Arsenal
+++++++++++++++++++++++

WIGAN 0 MAN UNITED 4
Javier Hernandez ‘Chicharito’ na Robin van Persie leo wamepiga Bao 2 kila mmoja na kuwapa Vinara wa Ligi Manchester United ushindi wa Bao 4-0 walipocheza ugenini na Wigan na kuwabakiza kkileleni wakiwa Pointi 7 mbele ya Man City.
+++++++++++++++

MAGOLI:

Man United 4
-Hernandez Dakika ya 35 & 63
-Van Persie 43 & 88
+++++++++++++++

Hadi mapumziko Man United walikuwa mbele kwa Bao 2-0 kwa Bao la kwanza la Chicharito baada ya shuti la Patrice Evra kutemwa na Kipa wa Ali Al Habsi na kutua kwa Chicharito aliemalizia vizuri.

Robin van Persie alifunga Bao la pili tamu sana baada ya kumgeuza nje ndani Beki wa wa Wigan Ivan Ramis na kupinda shuti lake lililomshinda Kipa.

Kipindi cha Pili Chicharito alifunga Bao la 3 kufuatia frikiki ya Van Persie kuwababatiza Mabeki wa Wigan na Bao la 4 kufungwa na Van Persie alipopokea krosi safi ya Danny Welbeck.

VIKOSI:
Wigan: Al Habsi, Ramis, Caldwell, Figueroa, Boyce, McCarthy, McArthur, Beausejour, Di Santo, Maloney, Kone

Akiba: Pollitt, Jones, Gomez, McManaman, Boselli, Stam, Golobart.

Man Utd: De Gea, Da Silva, Ferdinand, Evans, Evra, Young, Carrick, Cleverley, Giggs, van Persie, Hernandez

Akiba: Lindegaard, Valencia, Smalling, Vidic, Welbeck, Scholes, Kagawa.

Refa: Andre Marriner

MAN CITY 3 STOKE 0
Manchester City wamebakia nafasi ya pili Pointi 7 nyuma ya Manchester United baada ya kuwafunga Stoke City Bao 3-0 Uwanjani Etihad.
+++++++++++++++

MAGOLI:

Man City 3
-Zabaleta Dakika ya 43
-Dzeko 56
-Aguero 74 (Penati)
+++++++++++++++

VIKOSI:
Man City: Hart, Zabaleta, Kompany, Lescott, Clichy, Milner, Toure, Barry, Silva, Dzeko, Aguero

Akiba: Pantilimon, Sinclair, Javi Garcia, Toure, Tevez, Nastasic, Razak.

Stoke: Begovic, Cameron, Huth, Shawcross, Wilkinson, Walters, Adam, Nzonzi, Whelan, Jerome, Jones

Akiba: Sorensen, Wilson, Whitehead, Upson, Kightly, Crouch, Etherington.

Refa: Michael Oliver

TOTTENHAM 3 READING 1
LEO wakiwa kwao Uwanja wa White Hart Lane, Tottenham walitoka nyuma kwa Bao 1-0 na kuichapa Reading Bao 3-1.
+++++++++++++++

MAGOLI:

Tottenham 3
Dawson Dakika ya 9
Adebayor 51′
Dempsey 79′

Reading 1
Pogrebnyak Dakika ya 4
+++++++++++++++

VIKOSI:
Tottenham: Lloris, Walker, Dawson, Vertonghen, Naughton, Lennon, Sandro, Dembele, Sigurdsson, Adebayor, Defoe

Akiba: Friedel, Dempsey, Huddlestone, Parker, Falque, Livermore, Caulker.

Reading: Federici, Gunter, Pearce, Mariappa, Harte, Kebe, Karacan, Leigertwood, Guthrie, McAnuff, Pogrebnyak

Akiba: Taylor, Le Fondre, Hunt, Morrison, Tabb, Robson-Kanu, Cummings.

Refa: Howard Webb

WEST HAM 2 NORWICH 1
+++++++++++++++

West Ham 2
Noble Dakika ya 3 (Penati)
O'Brien 26′

Norwich 1
R Martin Dakika ya 90
+++++++++++++++

VIKOSI:

West Ham: Jaaskelainen, Demel, Reid, Tomkins, O'Brien, Noble, Collison, Taylor, Jarvis, Vaz Te, Cole
Akiba: Spiegel, Maiga, Diarra, Spence, O'Neil, Lletget, Lee.

Norwich: Bunn, Martin, Bassong, Turner, Ryan Bennett, Snodgrass, Howson, Tettey, Pilkington, Hoolahan, Kane

Akiba: Rudd, Jackson, Fox, Elliott Bennett, Barnett, Tierney, Smith.

Refa: Mark Clattenburg

SWANSEA 2 ASTON VILLA 2
+++++++++++++++

MAGOLI:

Swansea 2
-Routledge Dakika ya 9
-Graham 90

Aston Villa 2
-Weimann Dakika ya 44
-Benteke 84 (Penati)
+++++++++++++++

VIKOSI:
Swansea: Vorm, Rangel, Chico, Williams, Davies, Britton, de Guzman, Routledge, Hernandez, Michu, Graham

Akiba: Tremmel, Tiendalli, Monk, Agustien, Ki, Dyer, Shechter.

Aston Villa: Guzan, Lowton, Clark, Bennett, Herd, Weimann, Delph, Stevens, Westwood, Benteke, Albrighton

Akiba: Given, Ireland, Holman, Bowery, Bannan, Lichaj, Carruthers.

Refa: Mark Halsey.

WEST BROM 1 FULHAM 2

Dimitar Berbatov na Alex Kacaniklic wameifungia Fulham Bao mbili na kuipa ushindi wao wa pili wa ugenini Msimu huu walipoitwanga WBA Bao 2-1.
+++++++++++++++
MAGOLI:

West Brom 1
-Lukaku Dakika ya 49

Fulham 2
-Berbatov Dakika ya 39
-Kacaniklic 58′
+++++++++++++++

Romelu Lukaku, Mchezaji ambae yuko kwa Mkopo kutoka Chelsea, aliisawazishia WBA baada ya Berbatov kufunga Bao la kuongoza lakini walishindwa kufunga Bao nyingine baada ya Lukaku na Zoltan Gera kupiga posti.

Lakini Kacaniklic alifunga Bao la ushindi baada ya kupokea pasi murua kutoka kwa Bryan Ruiz.

VIKOSI:

West Brom: Foster, Jones, Tamas, McAuley, Ridgewell, Brunt, Mulumbu, Gera, Morrison, Fortune, Lukaku

Akiba: Myhill, Rosenberg, Long, Thorne, Jara Reyes, Odemwingie, Dawson.

Fulham: Stockdale, Riether, Hughes, Hangeland, Briggs, Dejagah, Sidwell, Karagounis, Kacaniklic, Ruiz, Berbatov

Akiba: Etheridge, Senderos, Baird, Kasami, Richardson, Rodallega, Frei.

Refa: Mike Dean
+++++++++++++++++++++++

RATIBA:
 
Jumatano 2 Januari 2013 

[SAA 4 Dak 45 Usiku]
Chelsea v QPR
Liverpool v Sunderland

[SAA 5 Usiku]
Newcastle v Everton

**WIKIENDI YA JANUARI 5 MECHI ZA RAUNDI YA 3 FA CUP

Jumamosi 12 Januari 2013

[SAA 12 Jioni]
Aston Villa V Southampton
Everton V Swansea
Fulham V Wigan
Norwich V Newcastle
Reading V West Brom
Stoke V Chelsea
Sunderland V West Ham

Jumapili 13 Januari 2013

[SAA 10 na Nusu Jioni]
Man United V Liverpool

[SAA 1 Usiku]
Arsenal V Man City

Jumatatu 14 Januari 2013

[SAA 5 Usiku]
QPR V Tottenham

Jumamosi 19 Januari 2013

[SAA 12 Jioni]
Liverpool V Norwich
Man City V Fulham
Newcastle V Reading
Swansea V Stoke
West Ham V QPR
Wigan V Sunderland

[SAA 2 na Nusu Usiku]
West Brom V Aston Villa

Jumapili 20 Januari 2013

[SAA 10 na Nusu Jioni]
Chelsea V Arsenal

[SAA 1 Usiku]
Tottenham V Man Utd

Jumatatu 21 Januari 2013

[SAA 5 Usiku]
Southampton V Everton

Jumatano 23 Januari 2013

[SAA 4 Dak 45 Usiku]
Arsenal V West Ham

**WIKIENDI YA JANUARI 26 MECHI ZA RAUNDI YA 4 FA CUP

Jumanne 29 Januari 2013

[SAA 4 Dak 45 Usiku]
Aston Villa V Newcastle
Norwich V Tottenham
QPR V Man City
Stoke V Wigan
Sunderland V Swansea

[SAA 5 Usiku]
Reading V Chelsea

Jumatano 30 Januari 2013

[SAA 4 Dak 45 Usiku]
Arsenal V Liverpool
Everton V West Brom
Fulham V West Ham

[SAA 5 Usiku]
Man United V Southampton

MANCINI: “RVP ndie anafanya Man United iwe tofauti na City!”

RVP_in_RED2Bosi wa Manchester City Roberto Mancini anaamini Straika wa Manchester United Robin van Persie ndie anaeleta tofauti kati ya Timu hizo mbili ambazo zinafukuzana kwenye Ligi Kuu England huku Man United wakiwa kileleni Pointi 7 mbele ya Man City ambao ni Mabingwa watetezi.

Mancini amesema: "Tulimtaka Van Persie kwa sababu tulijua ni Mchezaji muhimu! Yuko tofauti kabisa na Mastraika wengine! Van Persie ni muhimu kwa United na huyu ndie alieleta tofauti kati ya United na sisi hivi sasa!”

Mancini alibainisha kuwa walikuwa karibu kidogo kumsaini Robin van Persie lakini hilo halikutokea.

Hivi karibuni Mancini amekuwa akilia na Mastraika wake Sergio Aguero, Carlos Tevez, Edin Dzeko na Mario Balotelli kwa ubutu wa kufunga.

Amesema: “Msimu uliopita tulifunga Bao nyingi kupita Timu nyingine kwenye Ligi na tungempata Van Persie tungecheza Mfumo wa kutumia Mastraika watatu.”

Kwa sasa, Robin van Persie ndie anaongoza kwa ufungaji Bao nyingi kwenye Ligi Kuu England.

YANGA YAANZA MAZOEZI NCHINI UTURUKI!!

Source http://www.youngafricans.co.tz/

 

Africans Sports Club imeanza mazoezi leo asubuhi katika viwanja vya Fame Footballl vilivyopo pemebni kidogo mwa hoteli ya Fame Residence Lara & Spa iliyopo kusini mwa mji wa Antalya ambapo imeweka kambi ya mafunzo ya wiki mbili.

Kocha Brandts akisaidiwa na kocha msaidizi Fred Felix Minziro na kocha wa makipa Razaki Siwa waliongoza mazoezi hayo yaliyoanza majira ya saa 4 kamili asubuhi kwa saa za Afrika Mashariki na awamu ya pili ilianza majira ya saa 10 kamili jioni kwa saa za Afrika Mashariki.

Ratiba ya mazoezi ni mara mbili kwa siku asubuhi na jioni, ambapo timu inapata huduma zote za kambi katika Hoteli ya Fame Residence Lara & Spa kuanzia chakula, malazi, mazoezi ya viungo (Gym) ufukwe kwa ajili ya mazoezi ya stamina na kujenga mwili.
 

Mji wa Antalya ni maarufu katika medani ya soka kwani kwa ripoti tuliyopewa timu zaidi ya 200 zimeshafika katika mji huu kipindi cha majira ya baridi kuja kuweka kambi zikitokea katika nchi tofauti duniani.

Wenyeji wa Young Africans Team Travel wameandaa sherehe ya kuukaribisha mwaka mpya ambapo wachezaji na viongozi pamoja wenyeji wa mji huu watasherehekea pamoja.

22 WAITWA TAIFA STARS & HATIMAE KOCHA MPYA SIMBA ATUA!!

>>KOCHA SIMBA: KUSAINI MKATABA WA MIEZI 18
>>TAIFA STARS: SAMATTA & ULIMWENGU NDANI!!

TFF_LOGO12BAADA ya danadana ya Siku kadhaa, Kocha mpya wa Simba kutoka Ufaransa, Patrick Leiwig, hatimae alitua Jijini Dar es Salaam jana na kupokewa na Katibu Mkuu, Evodius Mtawala, pamoja na Mamia ya Washabiki wa Klabu hiyo.

Leiwig, ambae aliwahi kuifundisha Asec Mimosa ya Ivory Coast na pia Timu za Vijana za PSG ya Ufaransa, alisema anafahamu mambo mengi ya Simba na amejitayarisha vyema kuisaidia Timu hiyo katika Mashindano ya ndani na nje ya Tanzania.

Kocha huyo pia alisema amepewa Taarifa na Uongozi wa Klabu kuhusu safari yao ya kwenda Nchini Oman kujitayarisha na Raundi ya Pili ya Ligi Kuu Vodacom inayoanza Januari 26 pamoja na Mashindano ya CAF.
Akiongelea kuhusu Kocha huyo, Katibu Mkuu Mtawala amesema Kocha huyo atasaini Mkataba wa Miezi 18 na leo anatarajiwa kusafiri na Kikosi cha Simba kwenda Zanzibar kwa ajili ya Michuano ya Mapinduzi Cup inayoanza Januari 2.
+++++++++++++

MAPINDUZI CUP:

MAKUNDI:

KUNDI A:
Simba (Dar-es-Salaam),
Tusker (Kenya)
Bandari (Unguja)
Jamhuri (Pemba).

KUNDI B:
Azam FC (Dar-es-Salaam)
Mtibwa Sugar (Morogoro)
Coastal Union (Tanga)
Miembeni (Unguja).
+++++++++++++
 
Akiwa Simba, Kocha Leiwig atasaidiwa na Moses Basena kama Mkurugenzi wa Ufundi na Jamhuri Kiwele ‘Julio’ ambae ni Meneja wa Timu.

TAARIFA TOKA TFF:

Release No. 01
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Januari 1, 2013

WACHEZAJI 22 STARS WAITWA KAMBINI TAIFA STARS!!

Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen ametaja wachezaji 22 watakaoingia kambini Januari 6 mwaka huu jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mechi za kirafiki ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mechi ya mashindano dhidi ya Morocco itakayochezwa Machi mwaka huu.

Kwa mujibu wa Kocha Kim, wachezaji hao wanatakiwa kuripoti kambini katika hoteli ya Tansoma saa 11.30 jioni tayari kwa mazoezi yatakayoanza Januari 7 mwaka huu.

Wachezaji walioitwa ni makipa Juma Kaseja kutoka Simba ambaye pia ndiye nahodha wa Stars, Aishi Manula na Mwadini Ally wote kutoka Azam. Mabeki ni Aggrey Morris (Azam), Amir Maftah (Simba), Erasto Nyoni (Azam), Issa Rashid (Mtibwa Sugar), Kelvin Yondani (Yanga), Nadir Haroub (Yanga) na Shomari Kapombe (Simba).

Viungo ni Salum Abubakar (Azam), Athuman Idd (Yanga), Amri Kiemba (Simba), Khamis Mcha (Azam), Frank Domayo (Yanga), Mwinyi Kazimoto (Simba) na Shabani Nditi (Mtibwa Sugar).

Washambuliaji ni John Bocco (Azam), Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), Mrisho Ngasa (Simba), Simon Msuva (Yanga), na Thomas Ulimwengu wa TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).

Mbali ya Kim, benchi la ufundi la Taifa Stars linaundwa na Sylvester Marsh (Kocha Msaidizi), Juma Pondamali (Kocha wa makipa), Leopold Tasso (Meneja), Dk. Mwanandi Mwankemwa (Daktari wa timu), Frank Mhonda (Mtaalamu wa tibamaungo) na Alfred Chimela (Mtunza vifaa).

CAF YAMTUMA LIUNDA KUKAGUA VIWANJA ETHIOPIA

Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limemteua ofisa wake Leslie Liunda wa Tanzania kwenda Ethiopia kukagua viwanja na hoteli ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa utaratibu wa utoaji leseni kwa klabu zitakazoziwezesha kushiriki michuano inayoandaliwa na Shirikisho hilo.

Ofisa huyo atawasili nchini Ethiopia kesho (Januari 2 mwaka huu) ambapo anatarajiwa kukamilisha kazi hiyo Januari 6 mwakani na baadaye kupeleka ripoti yake CAF.

Utekelezaji wa kazi yake hiyo nchini Ethiopia utahusisha wadau mbalimbali ikiwemo Shirikisho la Mpira wa Miguu la Ethiopia (EFF), Wizara ya Michezo ya nchi hiyo, viongozi wa klabu na mameneja wa viwanja husika.

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Monday, December 31, 2012

MABINGWA MAN CITY WAHAHA KUSAINI WAPYA JANUARI, BA ALETA BALAA!!

>>CITY WAIKUBALI NYEKUNDU YA NASRI, KUIKOSA ARSENAL!
>>PARDEW ALIA NA WASHIRIKA WA DEMBA BA!!

MANCINI_n_MICAHMABINGWA wa England, Manchester City, wamedokeza kuwa upo uwezekano wa kusaini Wachezaji wapya Mwezi Januari na pia wamethibitisha kutokata Rufaa kuipinga Kadi Nyekundu ya Mchezaji wao Samir Nasri aliyopewa Juzi na huko Klabuni Newcastle, Meneja Alan Pardew, amelalamika kuhusu Washirika wa Straika wake Demba Ba ambae imetobolewa anasaka Klabu mpya Mwezi Januari.

MAN CITY
Meneja wa Manchester City Roberto Mancini amedokeza kuwa athari za kuwakosa Wachezaji wao, watakaokwenda kucheza AFCON 2013 na pia kuwa majeruhi, itawalazimisha kuingia Sokoni Mwezi Januari Dirisha la Uhamisho litakapofunguliwa ili kuimarisha Kikosi chao.

Mancini amethibitisha Mwezi Januari watawakosa Wachezaji watatu walioitwa kuichezea Ivory Coast kwenye AFCON 2013 ambao ni Yaya Toure, Kolo Toure na Abdul Razak, na pia inao majeruhi Micah Richards, JackRodwell, Aleksandar Kolarov na Maicon.

WAKATI HUO HUO, Man City imethibitisha haitakata Rufaa kupinga Kadi Nyekundu ya Mchezaji wao Samir Nasri aliyopewa Jumamosi huko Carrow Road wakati City ilipoifunga Norwich 4-3 kwa kumpiga kichwa Sebastien Bassong.

Mara baada ya uamuzi wa Man City, FA imetangaza kuwa Nasri atazikosa Mechi 3 ambazo ni za Ligi dhidi ya Stoke City Januari 1, FA CUP na Watford Januari 5 na ile ya Ligi ugenini na Arsenal hapo Januari 13.

PARDEW na BA
BOSI wa Newcastle Alan Pardew amewashambulia Washirika wa Demba Ba kwa kumshauri vibaya Straika huyo kutoka Senegal ambae juzi waliripotiwa kufanya mazungumzo na Chelsea kuhusu kuhama kwake lakini makubaliano hayakufikiwa.

Pardew amesema : “Kwa namna fulani, namsikitikia Demba kwani nadhani amezungukwa na Watu ambao si Wakilishi wake na wamekua wakisema hili na lile!”

Kwa Miezi kadhaa sasa, Newcastle imekuwa ikijitahidi kumpa Mkataba mpya Demba Ba ambao pia utaondoa Kipengele cha sasa kuwa anaweza kuuzwa wakati wowote ikiwa Malipo ya Pauni Milioni 7.5 yatatolewa.

2012: SPAIN YATAWALA KWA MATAJI!


 
CHELSEA_ULAYA_2012AUEFA leo, wakiaga 2012 na kuikaribisha 2013, wametoa pongezi kwa Spain,SPAIN_V_FRANCE Chelsea na Atletico Madrid kwa kutwaa Mataji katika Mwaka 2012 ambapo Spain ilitwaa Mataji 6 kati ya 11 katika Mashindano ya UEFA kwa Mwaka 2012 yakiwemo yale ya EURO 2012 kwa Timu ya Taifa ya Spain na Mataji ya EUROPA LIGI na UEFA SUPER CUP ambayo yote yalichukuliwa na Atletico Madrid.

Ingawa imeshindwa kutetea Taji lake na kuwa Bingwa wa kwanza wa Ulaya kutolewa hatua ya Makundi ya UEFA CHAMPIONZ LIGI, Chelsea imetajwa kuwa imefuata nyayo za Borussia Dortmund kutwaa Taji hilo kwa mara ya kwanza tangu Dortmund walipofanya hivyo Msimu wa 1996/7.

UEFA=WASHINDI MWAKA 2012

MASHINDANO
MSHINDI
MSHINDI WA PILI
UEFA EURO 2012
Spain
Italy
UEFA Champions League
Chelsea FC (ENG)
FC Bayern München (GER)
UEFA Europa League
Club Atlético de Madrid (ESP)
Athletic Club (ESP)
UEFA Super Cup
Club Atlético de Madrid (ESP)
Chelsea FC (ENG)
FIFA Club World Cup
SC Corinthians Paulista (BRA)
Chelsea FC (ENG)
UEFA European U-19
Spain
Greece
UEFA European U-17
Netherlands
Germany
FIFA U-20 -WANAWAKE KOMBE la DUNIA
United States
Germany
UEFA U-19 WANAWAKE
Sweden
Spain
FIFA U-17 -WANAWAKE KOMBE la DUNIA
France
North Korea
UEFA U-17 WANAWAKE
Germany
France
FIFA Futsal World Cup
Brazil
Spain
UEFA Futsal EURO 2012
Spain
Russia
UEFA Futsal Cup
FC Barcelona (ESP)
MFK Dinamo (RUS)
UEFA WANAWAKE CHAMPIONZ LIGI
Olympique Lyonnais (FRA)
1. FFC Frankfurt (GER)

ROBIN VAN PERSIE AMALIZA MWAKA AKIWA KILELENI KWA UFUNGAJI - UNITED WAKIIFUNGA 2-0 WEST BROM!!

ARSENAL BALAA, WALCOT AONYESHA THAMANI YAKE KWA HAT TRICK - NEWCASTLE WAKILA 7 - 3

YANGA YAWASILI SALAMA NCHINI UTURUKI!!



Kikosi cha mabingwa wa kombe la Kagame mara mbili mfululizo timu ya Young Africans imewasili salama katika mji wa Antalya kusini mwa nchi ya Uturuki majira ya saaa 10:30 jioni   kwa saa za afrika mashariki na kati na moja kwa moja kupolekewa na wenyeji wake kampuni ya Team Travel.

Young Africans imefikia katika hoteli ya Fame Residence Lara & Spa kilomita chahce kutoka katika uwanja wa ndege wa antalya, ambapo hoteli ya Fame Residence ipo mwambaoni mwa bahari ya mediteranian.

Mwanzoni Yanga ilikuwa ifikie katika hotel ya Sueno Beach Hotel iliyopo kilometa 70 kutoka uwanja wa ndege lakini jana siku moja kabla ya safari ilifanya mabadiliko na kuamua kuhamia katika hotel ya Fame Residence.

Wachezaji wamefurahi mandhari ya hotel kwani ni miongoni mwa hotel za nyota tano katika mjii huu wa Antalya hivyo wamefariijika na kuupa hongera uongozi kwa hatua waliyofikia ya kukubaliana na mwalimu kuweka kambi ya mafunzo  nchini Uturuki.
Timu itaanza mazoezi kesho asubuhi katika viwanja vilivyopo katika eneo la hotel ya fame, ambapo kwa siku timu itakua inafanya mazoezi mara mbili kwa siku asubuhi na jioni.

Kuhusu hali ya hewa ni baridi kiasi na sio baridi kali kama ilivyokuwa inatangazwa na vyombo vya habari hapo awali.

Mtandao wa huu utaendelea kwa hisani ya mtandao wa rasmi wa Yanga (www.youngafricans.co.tz) utaendelea kuwajuza juu ya kila kitu kinachojiri nchini Uturuki.

UHAMISHO: CHELSEA KUNASA KADHAA LAKINI BA…??

>>STURRIDGE KUTUA LIVERPOOL??
>>NEWCASTLE YAMPATA BEKI WA KIMATAIFA WA FRANCE!!

BENITEZ-CHELSEAULE mpango wa Demba Ba kuhamia Chelsea unaelekea umekwama baada ya kuibuka tetesi kuwa Wawakilishi wa Mchezaji huyo wa Newcastle hawakufikia makubaliano na Chelsea lakini zipo ripoti nyingine kuwa Chelsea wako mbioni kuwanasa Kiungo wa Metalist Kharkiv, Taison, na Mchezaji wa Corinthians Paulinho.

DEMBA_BA
Chelsea walikuwa na nia ya kumnunua Demba Ba ili awe anatoa sapoti kwa Straika wao Fernando Torres baada ya kukosa kumchukua Radamel Falcao wa Atletico Madrid katika Dirisha la Uhamisho la Januari baada ya Klabu hiyo ya Spain kung’ang’ania kuwa hawezi kuhama sasa labda mwishoni mwa Msimu.

Kuhusu Demba Ba, kikwazo kikubwa ni kuwa Meneja wa Newcastle, Alan Pardew, hapendezewi kumuuza Straika ambae amefunga Bao 13 kwenye Ligi na pia Mkataba wa Mchezaji huyo una kipengele kuwa Uhamisho wowote ule lazima uambatane na Malipo ya Pauni Milioni 7.5.

Na habari toka ndani ya Klabu ya Chelsea zimedokeza kuwa Liverpool watailipa Chelsea Pauni Milioni 12 ili kumnunua Daniel Sturridge ambae imeripotiwa alishapimwa afya yake huko Liverpool na Uhamisho rasmi unasubiri Januari 1 wakati Dirisha la Uhamisho litakapofunguliwa.

Nae Meneja wa muda wa Chelsea Rafa Benitez amekataa kuzungumza lolote kuhusu Ba pale aliposema: “Hatuzungumzii shughuli zetu hadharani. Yeye ni Mchezaji wa Klabu nyingine na huwa siongelei Wachezaji wengine!”

NEWCASTLE KUMSAINI MATHIEU DEBUCHY TOKA LILLE

Newcastle imefikia makubaliano kumsaini Beki wa Kimataifa wa France, Mathieu Debuchy, kutoka Klabu ya Ufaransa, Lille.

Beki huyo wa kulia mwenye Miaka 27 alichezea Mechi zote 4 za France kwenye EURO 2012 na inasadikiwa Ada yake ya Uhamisho ni Pauni Milioni 5.

Debuchy anakuwa Mchezaji wa pili kusainiwa na Newcastle kutoka Lille hivi karibuni baada ya Klabu hiyo pia kumchukua Kiungo Yohan Cabaye Juni 2011.

AFCON 2013: IVORY COAST YATAJA 23, DROGBA, YAYA, GERVINHO NDANI!

AFCON_2013_LOGOKOCHA wa Ivory Coast, Sabri Lamouchi, ametangaza Kikosi chake cha Wachezaji 23 kwa ajili ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2013 yatakayochezwa Nchini Afrika Kusini kuanzia Januari 19 hadi Februari 10 na Kikosi hicho kimesheheni Majina makubwa katika Soka wakiwemo Yaya Toure, Mchezaji Bora Afrika, na Straika hatari Didier Drogba.

 

+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

AFCON 2013

MAKUNDI:

KUNDI A: South Africa, Cape Verde, Morocco, Angola
KUNDI B: Ghana, DR Congo, Niger, Mali
KUNDI C: Zambia, Ethiopia, Nigeria, Burkina Faso
KUNDI D: Ivory Coast, Togo, Tunisia, Algeria
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

KIKOSI KAMILI:

MAKIPA: Copa Barry (Lokeren/Belgium), Daniel Yeboah (Hana Klabu), Badara Sangaré (Sewe San Pedro)

MABEKI: Abib Kolo Touré (Manchester City/England), Souleyman Bamba (Trabzonspor/Turkey), Emmanuel Eboué (Galatasaray/Turkey), Siaka Tiéné (PSG/France), Arthur Boka (Stuttgart/Germany), Ismaël Traoré (Brest/France), Igor Lolo (FC Kuban/Russia)

VIUNGO: Didier Zokora (Trabzonspor/Turkey), Cheik Tioté (Newcastle/England), Yaya Gnégnéri Touré (Manchester City/England), Max Gradel (Saint-Etienne/France), Romaric N'Dri (Saragosse/Spain), Abdul Razak (Manchester City/England), Didier Ya Konan (Hanovre/Germany)

WASHAMBULIAJI: Salomon Kalou (Lille/France), Gervinho (Arsenal/England), Didier Drogba (Shanghaï Shenhua/China), Wilfried Bony (Vitesse Arnhem/Netherlands), Lacina Traoré (Anzhi Makhachkala/Russia), Arouna Koné (Wigan/England)

BPL: MECHI ZA KUANZA 2013 ni JUMANNE JANUARI 1!!

BPL_LOGO>>ARSENAL KUCHEZA KIPORO NA WEST HAM JANUARI 23!!
 
BPL, Barclays Premier League, itafungua Mwaka mpya 2013 kwa Mechi 7 Jumanne Januari Mosi na Mechi 3 Jumatano Januari 2 huku Mabingwa watetezi Manchester City, ambao wako nafasi ya pili, kucheza nyumbani na Stoke City na Vinara wa Ligi, Manchester United, kuwa ugenini kuivaa Wigan.

Mechi za Ligi Kuu England kwa Mwezi Januari zitakuwa zikipisha Mechi za FA CUP kwa Wikiendi ya kuanzia Januari 5 ambapo Raundi ya 3 ya FA CUP itachezwa, Raundi ambayo Timu za Ligi Kuu England ndipo zinaanza Mashindano hayo na pia Wikiendi ya Januari 26 ambapo Raundi ya 4 ya FA CUP itachezwa.
+++++++++++++++++++++++

RATIBA:
 
Jumanne 1 Januari 2013 

SAA 9 Dak 45 Mchana]
West Brom v Fulham

[SAA 12 Jioni]
Man City v Stoke City
Swansea v Aston Villa
Tottenham v Reading
West Ham v Norwich
Wigan v Man United

[SAA 2 na Nusu Usiku]
Southampton v Arsenal

Jumatano 2 Januari 2013

[SAA 4 Dak 45 Usiku]
 Chelsea v QPR
Liverpool v Sunderland

[SAA 5 Usiku]
Newcastle v Everton
+++++++++++++++++++++++

Kimsimamo, Manchester United wako mbele kileleni kwa Pointi 7 wakifuatiwa na Man City na Timu ya 3 ni Chelsea, wenye Mechi moja mkononi, wakiwa Pointi 4 nyuma ya Man City.

Nafasi ya 4 inakamatwa na Tottenham lakini Arsenal wana nafasi ya kuikamata nafasi hiyo kwa vile wana Mechi moja mkononi baada ya Mechi yao na West Ham iliyokuwa ichezwe Desemba 26 kuahirishwa na sasa itachezwa Januari 23.
+++++++++++++++++++++++

MSIMAMO:

=Tofauti ya Magoli inatajwa kwa Timu zilizofungana Pointi

1 Man United Mechi 20 Pointi 49
2 Man City Mechi 20 Pointi 42
3 Chelsea Mechi 19 Pointi 38
4 Tottenham Mechi 20 Pointi 36
5 Arsenal Mechi 19 Pointi 33 [Tofauti ya Magoli 18]
6 Everton Mechi 20 Pointi 33 [Tofauti ya Magoli 8]
7 WBA Mechi 20 Pointi 33 [Tofauti ya Magoli 3]
8 Stoke Mechi 20 Pointi 29
9 Liverpool Mechi 20 Pointi 28 [Tofauti ya Magoli 5]
10 Swansea Mechi 20 Pointi 28 [Tofauti ya Magoli 5]
11 Norwich Mechi 20 Pointi 25 [Tofauti ya Magoli -9]
12 West Ham Mechi 19 Pointi 23
13 Sunderland Mechi 20 Pointi 22
14 Fulham Mechi 20 Pointi 21
15 Newcastle Mechi 20 Pointi 20
16 Wigan Mechi 20 Pointi 18 [Tofauti ya Magoli -13]
17 Aston Villa Mechi 20 Pointi 18 [Tofauti ya Magoli -24]
18 Southampton Mechi 19 Pointi 17
19 Reading Mechi 20 Pointi 13
20 QPR Mechi 20 Pointi 10
+++++++++++++++++++++++

WAFUNGAJI BORA:

Robin van Persie MAGOLI 14
Demba Ba 13
Miguel Michu 13
Luis Suarez 13
Jermain Defoe 10
Gareth Bale 9
Edin Dzeko 8
Marouane Fellaini 8
Steven Fletcher 8
Rickie Lambert 8
Theo Walcott  8
Sergio Aguero 7
Santi Cazorla 7
Juan Mata 7
Wayne Rooney 7
Carlos Tevez 7
Fernando Torres  7
+++++++++++++++++++++++

RATIBA MECHI ZIJAZO-LIGI KUU ENGLAND:

**WIKIENDI YA JANUARI 5 MECHI ZA RAUNDI YA 3 FA CUP

Jumamosi 12 Januari 2013

[SAA 12 Jioni]
Aston Villa V Southampton
Everton V Swansea
Fulham V Wigan
Norwich V Newcastle
Reading V West Brom
Stoke V Chelsea
Sunderland V West Ham

Jumapili 13 Januari 2013

[SAA 10 na Nusu Jioni]
Man United V Liverpool

[SAA 1 Usiku]
Arsenal V Man City

Jumatatu 14 Januari 2013

[SAA 5 Usiku]
QPR V Tottenham

Jumamosi 19 Januari 2013

[SAA 12 Jioni]
Liverpool V Norwich
Man City V Fulham
Newcastle V Reading
Swansea V Stoke
West Ham V QPR
Wigan V Sunderland

[SAA 2 na Nusu Usiku]
West Brom V Aston Villa

Jumapili 20 Januari 2013

[SAA 10 na Nusu Jioni]
Chelsea V Arsenal

[SAA 1 Usiku]
Tottenham V Man Utd

Jumatatu 21 Januari 2013

[SAA 5 Usiku]
Southampton V Everton

Jumatano 23 Januari 2013

[SAA 4 Dak 45 Usiku]
Arsenal V West Ham

**WIKIENDI YA JANUARI 26 MECHI ZA RAUNDI YA 4 FA CUP

Jumanne 29 Januari 2013

[SAA 4 Dak 45 Usiku]
Aston Villa V Newcastle
Norwich V Tottenham
QPR V Man City
Stoke V Wigan
Sunderland V Swansea

[SAA 5 Usiku]
Reading V Chelsea

Jumatano 30 Januari 2013

[SAA 4 Dak 45 Usiku]
Arsenal V Liverpool
Everton V West Brom
Fulham V West Ham

[SAA 5 Usiku]
Man United V Southampton

Sunday, December 30, 2012

QPR 0 LIVERPOOL 3!!

BPL_LOGOBao 3 ndani ya Dakika 28 za kwanza leo zimewapa Liverpool, waliocheza bila Meneja wao Brendan Rodgers ambae ni mgonjwa, ushindi wa 3-0 na kuzidi kuwadidimiza mkiani mwa Ligi Kuu England QPR huku Liverpool wakipanda nafasi moja na kumaliza Mwaka 2012 wakiwa nafasi ya 9.

Ushindi wa Liverpool ulipatikana kwa Bao za Luis Suarez, Bao 2, na Daniel Agger.


VIKOSI:
QPR: Julio Cesar, Onuoha, Nelsen, Hill, Traore, Mackie, Diakite, Mbia, Wright-Phillips, Taarabt, Cisse

Akiba: Green, Derry, Ferdinand, Granero, Da Silva, Hoilett, Faurlin.

Liverpool: Reina, Johnson, Skrtel, Agger, Jose Enrique, Allen, Henderson, Downing, Gerrard, Sterling, Suarez

Akiba: Gulacsi, Assaidi, Coates, Lucas, Carragher, Fernandez Saez, Shelvey.

Refa: Anthony Taylor
+++++++++++++++++++++++

RATIBA MECHI ZIJAZO:
 
Jumanne 1 Januari 2013
SAA 9 Dak 45 Mchana]
West Brom v Fulham
[SAA 12 Jioni]
Man City v Stoke
Swansea v Aston Villa
Tottenham v Reading
West Ham v Norwich
Wigan v Man United

[SAA 2 na Nusu Usiku]
Southampton v Arsenal

Jumatano 2 Januari 2013
[SAA 4 Dak 45 Usiku]
Chelsea v QPR
Liverpool v Sunderland

[SAA 5 Usiku]
Newcastle v Everton
+++++++++++++++++++++++

MSIMAMO:

=Tofauti ya Magoli inatajwa kwa Timu zilizofungana Pointi

1 Man United Mechi 20 Pointi 49

2 Man City Mechi 20 Pointi 42

3 Chelsea Mechi 19 Pointi 38

4 Tottenham Mechi 20 Pointi 36

5 Arsenal Mechi 19 Pointi 33 [Tofauti ya Magoli 18]

6 Everton Mechi 20 Pointi 33 [Tofauti ya Magoli 8]

7 WBA Mechi 20 Pointi 33 [Tofauti ya Magoli 3]

8 Stoke Mechi 20 Pointi 29

9 Liverpool Mechi 20 Pointi 28 [Tofauti ya Magoli 5]

10 Swansea Mechi 20 Pointi 28 [Tofauti ya Magoli 5]

11 Norwich Mechi 20 Pointi 25 [Tofauti ya Magoli -9]

12 West Ham Mechi 19 Pointi 23

13 Sunderland Mechi 20 Pointi 22

14 Fulham Mechi 20 Pointi 21

15 Newcastle Mechi 20 Pointi 20

16 Wigan Mechi 20 Pointi 18 [Tofauti ya Magoli -13]

17 Aston Villa Mechi 20 Pointi 18 [Tofauti ya Magoli -24]

18 Southampton Mechi 19 Pointi 17

19 Reading Mechi 20 Pointi 13

20 QPR Mechi 20 Pointi 10
+++++++++++++++++++++++

MKONGWE LAMPARD AIPAISHA CHELSEA NAFASI YA 3!!

BPL_LOGOFrank Lampard, Miaka 34, ambae mwishoni mwa Msimu Mkataba wake unamalizika na inadaiwa tayari hana nafasi Klabu hapo, leo alivaa utepe wa Nahodha na kuibeba Chelsea toka Goli 1 nyuma Uwanjani Goodison Park na yeye mwenyewe kupiga Bao mbili na kuwapa ushindi wa Bao 2-1, ukiwa ni ushindi wao wa kwanza kwa Miaka minne Uwanjani hapo.

Hi ilikuwa ni Mechi ya mwisho ya Ligi Kuu England kwa Mwaka 2012 kwa Klabu zote mbili ambazo zitacheza Mechi zao za Ligi zinazofuata hapo Januari 2, Mwaka 2013 kwa Chelsea kuikaribisha QPR Uwanjani Stamford Bridge na Everton kuwa ugenini huko St James Park kuivaa Newcastle.
++++++++++++

MAGOLI:

Everton 1
-Pienaar Dakika ya 2.

Chelsea 2
-Lampard Dakika ya 42 & 72
++++++++++++

Ushindi huu wa leo umeipaisha Chelsea kukamata nafasi ya 3 wakiwa Pointi 4 nyuma ya Timu ya Pili Manchester City huku wao wakiwa na Mechi moja mkononi.
+++++++++++++++++++++++

MSIMAMO-Timu za Juu:

=Tofauti ya Magoli inatajwa kwa Timu zilizofungana Pointi
1 Man United Mechi 20 Pointi 49
2 Man City Mechi 20 Pointi 42
3 Chelsea Mechi 19 Pointi 38
4 Tottenham Mechi 20 Pointi 36
5 Arsenal Mechi 19 Pointi 33 [Tofauti ya Magoli 18]
6 Everton Mechi 20 Pointi 33 [Tofauti ya Magoli 8]
7 WBA Mechi 20 Pointi 33 [Tofauti ya Magoli 3]
8 Stoke Mechi 20 Pointi 29
9 Swansea Mechi 20 Pointi 28
10 Liverpool Mechi 19 Pointi 25 [Tofauti ya Magoli 2]
+++++++++++++++++++++++

Ingawa Everton wamefungwa Mechi hii lakini walitoa upinzani mkubwa na wangeweza hata kushinda kwani Straika wao Nikica Jelavic alipiga posti na kukosa nafasi ya wazi mwishoni.

VIKOSI:

Everton: Howard, Jagielka, Heitinga, Distin, Baines, Naismith, Osman, Hitzlsperger, Pienaar, Anichebe, Jelavic.

Akiba: Mucha, Oviedo, Gueye, Barkley, Vellios, Duffy, Browning.
 
Chelsea: Cech, Azpilicueta, Ivanovic, Cahill, Cole, Ramires, Luiz, Lampard, Mata, Torres, Hazard.

Akiba: Turnbull, Oscar, Moses, Ferreira, Marin, Piazon, Ake.
 
Refa: Howard Webb
+++++++++++++++++++++++

RATIBA MECHI ZIJAZO:  

Jumapili 30 Desemba 2012
[SAA 1 Usiku]
QPR v Liverpool

Jumanne 1 Januari 2013
SAA 9 Dak 45 Mchana]
West Brom v Fulham

[SAA 12 Jioni]
Man City v Stoke
Swansea v Aston Villa
Tottenham v Reading
West Ham v Norwich
Wigan v Man United

[SAA 2 na Nusu Usiku] 
Southampton v Arsenal

Jumatano 2 Januari 2013 

[SAA 4 Dak 45 Usiku]
Chelsea v QPR
Liverpool v Sunderland

[SAA 5 Usiku]
Newcastle v Everton

AFCON 2013: WENYEJI BAFANA BAFANA WATANGAZA KIKOSI!

AFCON_2013_LOGOWENYEJI wa Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2013, Afrika Kusini wametangaza Kikosi chao cha Wachezaji 23 kwa ajili ya Mashindano hayo yatakayochezwa Nchini kwao kuanzia Januari 19 hadi Februari 10.

Akitangaza Kikosi hicho, Kocha Mkuu wa Bafana Bafana Gordon Igesund, amesema ni bahati mbaya hawezi kuchukua zaidi ya Wachezaji 23 lakini anaamini wale walioteuliwa wataiwakilisha vyema Afrika Kusini.
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

AFCON 2013
MAKUNDI:

KUNDI A: South Africa, Cape Verde, Morocco, Angola
KUNDI B: Ghana, DR Congo, Niger, Mali
KUNDI C: Zambia, Ethiopia, Nigeria, Burkina Faso
KUNDI D: Ivory Coast, Togo, Tunisia, Algeria
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

Nahodha wa Kikosi hicho ni Bongani Khumalo.

Kabla ya kuanza rasmi AFCON 2013, Bafana Bafana watacheza Mechi mbili za Kirafiki dhidi ya Norway Mjini Cape Town, Afrka Kusini hapo Januari 8 na Januari 12 kucheza na Algeria huko Soweto, Johannesburg.

Afika Kusini watacheza Mechi ya ufunguzi ya AFCON 2013 dhidi ya Cape Verde Januari 19 Uwanjani Soccer City Mjini Johannesburg.

KIKOSI KAMILI:

MAKIPA: Itemeleng Khune, Wayne Sandilands, Senzo Meyiwa

MABEKI: Bongani Khumalo, Siboniso Gaxa, Siyabonga Sangweni, Anele Ngcongca, Tsepo Masilela, Thabo Nthethe, Thabo Matlaba

VIUNGO: Lerato Chabangu, Thulani Serero, Kagisho Dikgacoi, Dean Furman, Reneilwe Letsholonyane, Siphiwe Tshabalala, May Mahlangu, Thuso Phala, Oupa Manyisa

MASTRAIKA: Bernard Parker, Tokelo Rantie, Lehlohonolo Majoro, Katlego Mphela.

WALCOTT KUBAKI ARSENAL, NANI HAENDI KOKOTE, REFA MATATANI…!!

WENGER_MASHAKANIWALCOTT KUBAKI ARSENAL? NANI HAENDI KOKOTE! REFA MATATANI…!!
 
HUKU kukiwa na hatari ya kumpoteza Winga wao Theo Walcott bila kupata Senti hata moja ifikapo mwishoni mwa Msimu, Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, amesema bado wanamatumaini Mchezaji huyo atakubali kusaini Mkataba mpya na huko Old Trafford, Sir Alex Ferguson, ametamka Nani hauzwi Mwezi Januari na wakati huo huo, Refa alieboronga atachunguzwa na FA.


THEO WALCOTT: ARSENAL na ARSENE WENGER WANA MATUMAINI!

Arsene Wenger amesema Hetitriki ya Theo Walcott aliyopiga jana Arsenal ilipoitwanga Newcastle 7-3 haina uzito wowote kwenye mustabali wake Klabuni hapo ambapo kuna mvutano huku Mchezaji huyo akigoma kukubali Mkataba mpya wakati Mkataba wake wa sasa unamalizika mwishoni mwa Msimu na kuanzia Januari Mosi yuko huru kuongea na Klabu nyingine zinazomtaka.

Wenger ametamka: “Nia yangu ni asaini Mkataba mpya. Yeye ni Mchezaji wa hapa na hata kama angecheza vibaya na Newcastle bado sisi tunataka aongeza Mkataba!”

Walcott, Miaka 23, amefunga Bao 14 Msimu huu na 4 ni katika Mechi 3 ambazo amechezeshwa kama Straika wa Kati.

Arsenal ilimsaini Walcott akiwa na Miaka 16 kutoka Southampton Mwaka 2006 kwa Dau la Pauni Milioni 5 ambalo lilipanda hadi Pauni Milioni 12.5.

Akiongea mara baada ya Mechi na Newcastle, Walcott alisema: “Mazungumzo na Arsenal yanaeendelea na nina hakika mambo yatakamilika hivi karibuni.”

NANI HAUZWI!

Bosi wa Manchester United Sir Alex Ferguson amesisitiza Nani hatauzwa Dirisha la Uhamisho likifunguliwa Mwezi Januari.

Tangu awe hana namba ya kudumu Msimu huu, kulizuka uvumi kuwa Mchezaji huyo kutoka Ureno yuko mbioni kuuzwa lakini Ferguson amepuuzia hayo na kusema: “Hatutamwachia aondoke. Tunamhitaji Nani. Kwanini tumuachie aondoke??”

Aliongeza: “Bado Mkataba wake una Mwaka mmoja na nusu. Yeye anatupa kitu tofauti na Wachezaji wengine hapa. Ana kipaji kikubwa. Bahati mbaya ameumia na tumempeleka Dubai kupumzika na apone. Tunatarajia atarudi Uwanjani katikati ya Januari.”

REFA MATATANI!!

REFA Mick Russell yupo mashakani na FA, Chama cha Soka England, baada ya kutomtoa nje Staa wa Sheffield Wednesday Jeremy Helan licha ya kumpa Kadi za Njano mbili kwenye Mechi waliyotoka sare 0-0 na Huddersfield.

+++++++++++++++++++++++

MAKOSA ya MAREFA WENGINE:

STUART ATTWELL: Mwaka 2008, aliwapa Reading Goli dhidi ya Watford badala ya Kona na akaondolewa kwenye Listi ya Marefa wa Mechi kubwa.

GRAHAM POLL: Alimpa Mchezaji wa Croatia Josip Simunic Kadi za Njano 3 katika Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2006 kabla kumtoa nje kwa Kadi Nyekundu katika Mechi na Australia.

+++++++++++++++++++++++
Tukio hilo liliwapandisha hasira Huddersfield waliotaka Refa huyo apewe adhabu kali.

Helan, ambae yuko kwa mkopo Sheffield Wednesday akitokea Manchester City, alipewa Kadi ya Njano ya kwanza katika Dakika ya 9 kwa kujiangusha kwa makusudi na ya pili katika Dakika ya 26 kwa kucheza Faulo.

Licha ya Wachezaji wa Huddersfield kulalamika kwa Refa Mick Russell wakitaka Helan atolewe, Refa huyo alianzisha tena mpira bila kumtoa ikimaanisha Helan asingeweza kutolewa tena.

Mwenyewe Helan amesema: “Ilishangaza! Lakini mie sio Refa, nilicheza Dakika 90 na nafurahia kwa hilo!”
Baadae Refa Russell alikiri kosa lake na kudai alikosea kuandika Namba wakati akitoa Kadi za Njano.

Chama cha Marefa, PGMO [Professional Game Match Officials Limited] na FA zimesema uchunguzi kuhusu uchezeshaji wa Refa Russell.

SIMBA YATANDIKWA 3-0 NA TUSKER - KOCHA MZUNGU BADO KITENDAWILI!!


Kiungo wa Simba, Mussa Mudde, akijaribu kupiga shuti mbele ya mchezaji wa Tusker ya Kenya, katika mchezo wao wa kimataifa wa kirafiki uliopiga leo katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo, Simba walipigwa bao 3-0.
 

KOCHA Mpya wa Simba, Mfaransa Patrick Liewig, aliyetarajiwa kuwapo uwanjani wakati kikosi hicho kilipomenyana na Tusker FC katika mchezo wa kirafiki kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ameshindwa kutokea uwanjani hapo na kuwaacha midomo wazi mashabiki wa timu hiyo.
Awali katika taarifa yake, Simba ilidai kwamba Liewig angetambulishwa rasmi kuinoa timu hiyo wakati wa mchezo huo, lakini kukosekana kwake ni jambo lililowaacha njia panda mashabiki wa timu hiyo waliofurika kwenye kumshuhudia kocha wao mpya.
 
Mechi hiyo ambayo ilitarajiwa na mashabiki wa timu hiyo kwamba watashuhudia kikosi kamili kikishuka dimbani ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya duru la pili la Ligi Kuu Tanzania Bara itakayoanza mwezi ujao, badala yake ni kikosi B cha timu hiyo ndicho kilichoanzishwa.
Tusker FC ambao siku kadha zilizopita waliinyuka Yanga bao 1-0, waliendeleza makali yao na kuzichapa timu za hapa nchini baada ya kuinyuka Simba mabao 3-0 katika  mchezo wa kirafiki uliofanyika kwenye dimba la Taifa, Dar es Salaam jana.
 
Mabao mawili ya Jesse Were na moja la Fredrick Onyango yalitosha kuitoa kimasomaso Tusker katika mchezo ambao mashabiki wa Simba walishindwa kupata burudani kutoka kwa nyota wao wa kimataifa kutokana na kutokuwapo katika mchezo huo.
 
Katika mchezo huo, Simba ilianza kumtumia tena kiungo wake mshambuliaji, Haruna Moshi 'Boban', aliyeingia kipindi cha pili kujaribu kuweka mambo sawa, lakini mambo yaliendelea kuwa magumu kwa kikosi hicho cha Wekundu wa Msimbazi.
 
Boban alicheza mechi hiyo akitokea kwenye adhabu ya kufungiwa mechi kadha za duru la kwanza la Ligi Kuu Bara kwa madai ya kwamba ni utovu wa nidhamu.
 
Kama timu tumeona hilo sio tatizo na kwamba kocha wetu mtu atatua hapa nchini Jumatatu. Kuhusu wachezaji wengi, Okwi (Emmanuel) na kipa wetu Abel Dhaira na Sunzu (Felix) watatua hapa nchini kesho (leo).
 
Kuhusu wale wachezaji waliokuwa kwenye timu ya taifa, Kapombe (Shomari), Ngassa (Mrisho) na wengineo watajiunga rasmi na timu Jumatatu.
 
Katika mchezo wa jana, Simba ilijaribu kufanya mabadiliko kadha ya kuwaingiza wachezaji wake, Boban, Edward Christopher, Nassor Chollo, Emily Isyaka, Salum Kinje, Jonas Mkude na Ramadhan Singano, lakini hakukuwa na mabadiliko yoyote na hivyo hadi mwisho wa mchezo, Simba ilikubali kipigo.
 
Simba: William Mwete, Haruna Shamte, Paul Ngalema, Hassan Hatibu, Komain Keita, Mussa Mudde, Haroun Athuman, Abdallah Seseme, Abdallah Juma, Ramadhan Chomo, Kiggy Makassy.
 
Tusker FC: Samwel Odhiambo, Luje Ochieng, Jeremiah Bright, Mana Odhiambo, Joseph Shikokoti, Khalid Aucho, Edwin Ombasa, Fredrick Onyango, Jesse Were, Robert Omonuk. Refa: Hashim Abdallah kutoka Dar es Salaam.
 
 SOURCE:http://handenikwetu.blogspot.com

LEO FUNGA MWAKA EVERTON v CHELSEA, QPR v LIVERPOOL!!

BPL_LOGO+++++++++++++++++++++++
RATIBA:
Jumapili 30 Desemba 2012 

[SAA 10 na Nusu Jioni]
Everton v Chelsea

[SAA 1 Usiku]
QPR v Liverpool
+++++++++++++++++++++++

LEO zipo Mechi mbili za Ligi Kuu England ambazo ndizo za mwisho kabisa kwa Mwaka 2012 na zifuatazo ni Dondoo kuhusu Mechi hizo:

EVERTON v CHELSEA
Uwanja: Goodison Park
Hali za Wachezaji:
Everton watacheza Mechi hii bila Marouane Fellaini ambae atakuwa akimalizia Kifungo chake cha Mechi 3 na pia itawakosa majeruhi Tony Hibbert na Kevin Mirallas.

Chelsea wataendelea kumkosa Nahodha wao John Terry ambae ni majeruhi lakini Kiungo Ramires atarudi dimbani baada kupona nyonga iliyomfanya akose Mechi ya Boxing Dei walipoifunga Norwich City.

Uso kwa Uso:
++Everton hawajafungwa na Chelsea Uwanjani Goodison Park katika Mechi 4 zilizopita kwa kushinda 3 na sare 1.

++Chelsea wameshinda Mechi moja tu kati ya 8 walizocheza mwishoni na Everton na hiyo ilikuwa ni ushindi wa Bao 3-1 Uwanjani Stamford Bridge Msimu uliopita.
+++++++++++++++++++++++

MSIMAMO:
=Tofauti ya Magoli inatajwa kwa Timu zilizofungana Pointi
1 Man United Mechi 20 Pointi 49
2 Man City Mechi 20 Pointi 42
3 Tottenham Mechi 20 Pointi 36
4 Chelsea Mechi 18 Pointi 35
5 Arsenal Mechi 19 Pointi 33 [Tofauti ya Magoli 18]
6 Everton Mechi 19 Pointi 33 [Tofauti ya Magoli 9]
7 WBA Mechi 20 Pointi 33 [Tofauti ya Magoli 3]
8 Stoke Mechi 20 Pointi 29
9 Swansea Mechi 20 Pointi 28
10 Liverpool Mechi 19 Pointi 25 [Tofauti ya Magoli 2]
11 Norwich Mechi 20 Pointi 25 [Tofauti ya Magoli -9]
12 West Ham Mechi 19 Pointi 23
13 Sunderland Mechi 20 Pointi 22
14 Fulham Mechi 20 Pointi 21
15 Newcastle Mechi 20 Pointi 20
16 Wigan Mechi 20 Pointi 18 [Tofauti ya Magoli -13]
17 Aston Villa Mechi 20 Pointi 18 [Tofauti ya Magoli -24]
18 Southampton Mechi 19 Pointi 17
19 Reading Mechi 20 Pointi 13
20 Mechi 20 Pointi 10
+++++++++++++++++++++++

QPR v LIVERPOOL
Uwanja: Loftus Road
Hali za Wachezaji:
Beki wa QPR Ryan Nelsen yupo kwenye hati hati ya kucheza Mechi hii baada ya kuugua na Wachezaji wengine ambao uchezaji wao upo kwenye wasiwasi kutokana na maumivu ni Kipa Julio Cesar, Beki Nedum Onuoha na Kiungo Park Ji-sung.

Fowadi wa Liverpool Luis Suarez anatarajiwa kucheza licha ya kuwa na maumivu ya enka huku Raheem Sterling na Joe Allen wakitarajiwa kuanza Mechi hii baada ya kuanzia Benchi katika Mechi mbili zilizopita.

Uso kwa Uso:
++Liverpool wameifunga QPR Mechi 3 kati ya 4 za Ligi walizocheza.
+++++++++++++++++++++++

RATIBA MECHI ZIJAZO:
 
Jumanne 1 Januari 2013 

SAA 9 Dak 45 Mchana] 
West Brom v Fulham

[SAA 12 Jioni]
Man City v Stoke
Swansea v Aston Villa
Tottenham v Reading
West Ham v Norwich
Wigan v Man United

[SAA 2 na Nusu Usiku]
Southampton v Arsenal

Jumatano 2 Januari 2013 

[SAA 4 Dak 45 Usiku]
Chelsea v QPR
Liverpool v Sunderland

[SAA 5 Usiku]
Newcastle v Everton

FA CUP RAUNDI ya 3: DIMBANI JANUARI 5!!

>>MECHI 4 TU KUKUTANISHA TIMU ZA LIGI KUU!!

FA_CUP-NEW_LOGO
MABINGWA WATETEZI wa FA CUP, Chelsea, wataanza utetezi wao wa FA CUP kwenye Raundi ya 3 kwa kucheza ugenini na Southampton hapo Januari 5 na hiyo ni Mechi moja kati ya 4 itakayozikutanisha Timu za Ligi Kuu England pekee.

Raundi ya 3 ya FA CUP ndiyo ambayo imejumuisha Timu toka Ligi Kuu England.
Mechi nyingine ambazo zitakutanisha Timu za Ligi Kuu England pekee ni zile za Manchester United kutua Upton Park kucheza na West Ham United, QPR kuikaribisha West Brom na Arsenal kusafiri kucheza na Swansea.

Timu nyingine vigogo wa Ligi Kuu, kama vile Mabingwa wa Ligi Manchester City, wao watacheza na Watford, Tottenham kucheza na Coventry.
Liverpool watakuwa ugenini kuivaa Mansfield.

RATIBA:
RAUNDI ya TATU: 

Jumamosi Januari 5
[SAA 9 Dak 45 Mchana]
Brighton v Newcastle

[SAA 12 Jioni]
Crystal Palace v Stoke
Tottenham v Coventry City
Wigan v Bournemouth
Fulham v Blackpool
Aston Villa v Ipswich
Charlton v Huddersfield
Barrow au Macclesfield v Cardiff
Barnsley v Burnley
Manchester City v Watford
Leicester v Burton
Millwall v Preston
Derby v Tranmere
Crawley v Reading
Aldershot v Rotherham
Middlesbrough v Hastings
Oxford v Sheffield United
Southampton v Chelsea
QPR v West Brom
Peterborough v Norwich
Bolton v Sunderland
Nottingham Forest v Oldham
Hull v Alfreton or Leyton Orient
Blackburn v Bristol City
Leeds v Birmingham
Southend v Brentford
Luton v Wolves
Sheffield Wednesday v MK Dons

[SAA 2 na Dak 15 Usiku]
West Ham v Manchester United

Jumapili Januari 6
Swansea v Arsenal [SAA 10 na Nusu Jioni]
Mansfield v Liverpool [SAA 1 Usiku]

Jumatatu Januari 7
Cheltenham v Everton [SAA 4 Dak 45 Usiku]