WAKATI Wachezaji wa Manchester United, Rio Ferdinand na Michael Carrick, wakichekelea na uteuzi wa Meneja mpya David Moyes na kumkaribisha kwa furaha, Mwenyekiti wa Everton, Bill Kenwright, amesikitishwa na kuondoka kwake na kusema Man United wamebahatika sana kumpata.
Jumatano, Sir Alex Ferguson alitangaza
kustaafu kuwa Meneja na leo Man United imemtangaza Mrithi wake kuwa ni
David Moyes, Mtu ambae alipendekezwa na Sir Alex Ferguson mwenyewe.
David Moyes amepewa Mkataba wa Miaka 6 na Man United ambao utaanza rasmi Julai 1.
Moyes, ambae Mkataba wake na Everton
unamalizika Juni 30, ataisimamia Everton katika Mechi zake 2 zilizobakia
za BPL, Barclays Premier League, ambazo watacheza na West Ham na
kumaliza na Chelsea hapo Mei 19 Uwanjani Stamford Bridge.
Rio Ferdinand, ambae amecheza chini ya
Ferguson kwa Miaka 10 huko Old Trafford, amesema: "Ilikuwa ni muhimu kwa
Klabu kufanya uamuzi wa haraka kabla Watu hawajaanza kuleta uvumi.
Hatujawahi kuwa na tatizo nae na Watu wanaomjua wanasema ni Mtu mwema
aliefanya kazi nzuri huko Everton.”
Nae Michael Carrick amesema anachojua
yeye ni kuwa Moyes ni mkweli kwa Wachezaji wake na Mchapa kazi aliefanya
kazi njema Everton.
Mwenyekiti Everton- Bill Kenwright
Mwenyekiti wa Everton Bill Kenwright
amemsifia Meneja wake David Moyes ambae anaondoka na kuanza kazi ya
Umeneja huko Man United kuanzia Julai 1.
Kenwright, ambae ndie alimwingiza Moyes
Goodison Park kutoka Preston North End Mwezi Machi 2002, amesema
amehuzunishwa na kuondoka kwake.
Ametamka: “Huyu ni Meneja Bora na Man
United wana bahati sana kumpata! Everton yote itahuzunika kuagana nae,
ni Meneja Bora! Hatukuweza kumzuia Mkataba wake unakwisha na yeye kaamua
kwenda Man United! Huwezi kumzuia!”
Licha ya kutofanikiwa kuchukua Kombe
lolote akiwa na Everton kwa Miaka yake 11 aliyokuwa hapo kitu pekee na
kikubwa kilichompa umaarufu ni kuiongoza Klabu masikini, isiyokuwa na
Fedha kununua Wachezaji wakubwa, kubakia BPL na kuweza kushindana kiume
na Klabu kubwa na Tajiri.
-ALIANZA kucheza Soka na Celtic
na kumalizia Preston ambako alicheza na Chipukizi David Beckham
aliepelekwa hapo kwa mkopo na Man United kati ya Februari na Machi 1995
-BAADA ya kuifikisha Preston
kwenye Fainali ya Mechi za Mchujo wa Daraja la Kwanza, Moyes akahamia
Everton kama Meneja kumrithi Walter Smith hapo Machi 2002
-ALIMPA Wayne Rooney nafasi ya
kucheza Mechi ya kwanza kwenye Ligi Agosti 2002 na kumuuza Man United
Miaka miwili baadae kwa Pauni Milioni 20.
-ALIIFIKISHA Everton nafasi ya 4 kwenye Ligi Kuu Mwaka 2005 na kucheza UEFA CHAMPIONZ LIGI
-ALIIPELEKA Everton Fainali ya FA CUP Mwaka 2009 walipofungwa 2-1 na Chelsea baada ya kuitoa Man United kwenye Nusu Fainali
No comments:
Post a Comment