Sunday, June 2, 2013

CAF KOMBE LA SHIRIKISHO: TP MAZEMBE YAFUNGWA LAKINI YASONGA!

MBWANA_SAMATTA_IN_TPTIMU 8 ZAINGIA HATUA YA MAKUNDI!
 
JANA Mechi za Marudiano za Raundi ya Mtoano ya Timu 16 za Mashindano ya CAF ya Kombe la Shirikisho zilikamilika na TP Mazembe ya Congo DR, ambayo ina Wachezaji muhimu wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu, ilifungwa Bao 2-1 huko Maputo, Msumbiji na Liga Muculmana lakini ilisonga mbele kwa Jumla ya Mabao 5-2 kwa vile ilishinda katika Mechi ya Kwanza huko Lubumbashi Bao 4-0.

TP Mazembe na Washindi wengine 7 wa Raundi hii wataingizwa kwenye Droo kupanga Makundi mawili ya Timu 4 kila moja.

Timu nyingine 7 zilizosonga ni Entente Setif (Algeria), Stade Malien (Mali), Enugu Rangers (Nigeria), Etoile Sahel (Tunisia), St George (Ethopia), 3 FUS Rabat (Morocco) na 1 CA Bizertin (Tunisia).

Mashindano mengine makubwa ya CAF kwa Klabu ni CHAMPIONZ LIGI na hayo yataanza hatua za Makundi hapo Julai 20 kwa kuwepo Timu 4 kila Kundi na kucheza Ligi ya Nyumbani na Ugenini na Timu 2 za juu toka kila Kundi kuingia Nusu Fainali.

RAUNDI YA MCHUJO YA TIMU 16-MARUDIANO

MATOKEO:

[Kwenye Mabano Jumla ya Magoli kwa Mechi mbili]

Jumamosi Juni 1

2 US Bitam (Gabon) 2 Entente Setif (Algeria) 0 [2-2, Penati 3-5]

Jumapili Juni 2

Liga Muculmana (Mozambique) 2 TP Mazembe (DRC) 1 [2-5]

Lydia Academic (Burundi) 0 Stade Malien (Mali) 1 [0-6]

CS Sfaxien (Tunisia) 0 Enugu Rangers (Nigeria) 0 [0-1]

Etoile Sahel (Tunisia) 2 JSM Bejaia (Algeria) 1 [4-3]

ENPPI (Egypt) 3 St George (Ethopia) 1 [3-3, St George yasonga Goli Ugenini]

FAR Rabat (Morocco) 3 FUS Rabat (Morocco) 3 [3-4]

Ismaily (Egypt) 1 CA Bizertin (Tunisia) 0 [1-3]

No comments:

Post a Comment