Monday, June 3, 2013

JOSE MOURINHO RASMI STAMFORD BRIDGE!!

JOSE_MOURINHO-poaNI MENEJA WA 9 HIMAYA YA ABRAMOVICH!!
NI RASMI Jose Mourinho amerudi tena kama Meneja wa Chelsea kwa Mkataba wa Miaka minne.

Jose Mourinho, Miaka 50, anachukua nafasi ya Rafael Benitez ambae alikuwa Meneja wa muda tangu Novemba Mwaka jana na kumaliza Mkataba wake hivi Juzi tu.

Akiwa Chelsea kwa mara ya kwanza na kumalizia hapo Septemba 2007, Mourinho alifanikiwa kutwaa Ubingwa wa Ligi mara mbili mfululizo.

Akiongelea kuhusu ujio huu wa Mourinho, Mtendaji Mkuu wa Chelsea, Ron Gourlay, alitamka: “Alikuwa na bado ni Mtu anaependwa hapa Klabuni na kila Mtu ana hamu ya kufanya nae kazi tena.”

Mourinho alitua Stamford Bridge kwa mara ya kwanza kabla Msimu wa 2004 kuanza ikiwa ni muda mfupi tu baada ya kuiwezesha FC Porto kutwaa UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI.

Akiwa na Chelsea, Mourinho alitwaa FA CUP mbili, Kombe la Ligi mara mbili na Ubingwa mara mbili lakini alishindwa kuchukua UCL.

Mourinho atatambulishwa rasmi kama Meneja mpya wa Chelsea Jumatatu Juni 10.

Akiwa na Inter Milan, Mourinho alitwaa UCL kwa mara ya pili Mwaka 2010 lakini Mwaka huo huo akahamia Real Madrid kumbadili Manuel Pellegrini ambae sasa anasemekana kutaka kujiunga na Manchester City.

Katika Msimu wake wa kwanza wa La Liga, Real Madrid ilimaliza Nafasi ya Pili nyuma ya Barcelona lakini Msimu uliofuatia walinyakua Ubingwa.

Hata hivyo, Msimu huu, hakufanya vizuri na amekuwa na bifu na baadhi ya Wachezaji wake kina Iker Casillas, Sergio Ramos na Pepe na hatimae Barcelona kuipokonya Ubingwa.


MAMENEJA WA CHELSEA CHINI YA ROMAN ABRAMOVICH:

-Claudio Ranieri: Sep 2000 mpaka Mei 2004

-Jose Mourinho: Jun 2004 mpaka Sep 2007

-Avram Grant: Sep 2007 mpaka Mei 2008

-Luiz Felipe Scolari: Jul 2008 mpaka Feb 2009

-Guus Hiddink: Feb 2009 mpaka Mei 2009

-Carlo Ancelotti: Jun 2009 mpaka Mei 2011

-Andre Villas-Boas: Jun 2011 mpaka Machi 2012

-Roberto Di Matteo: Machi 2012 mpaka Nov 2012

-Rafael Benitez: Nov 2012 mpaka Mei 2013

-Jose Mourinho: Juni 2013 -


Mourinho anarudi Chelsea na kuwakuta tena baadhi ya Wachezaji aliokuwa nao mara ya kwanza kina Petr Cech, Ashley Cole, Frank Lampard, John Mikel Obi na John Terry pamoja na Michael Essien ambae alikuwa nae huko Real alikopelekwa kwa Mkopo na Chelsea.

Akizungumza kuhusu Mourinho, Mchezaji mkongwe wa Chelsea, Frank Lampard, alisema: “Ni Meneja Bora! Nimesema hili zaidi ya mara milioni, kiasi cha kuonekana kero kwa Watu, lakini nimebahatika kufanya nae kazi!”

No comments:

Post a Comment