Monday, June 3, 2013

KOMBE LA DUNIA 2014: ARGENTINA YAITA WATATU TOKA NYUMBANI, TEVEZ BADO NJE!!

BRAZIL_2014_BESTTANGU KOCHA ALEJANDRO SABELLA ATEULIWE, TEVEZ HAJAIONA ARGENTINA!
 
FERNANDO GAGO, Kiungo wa zamani wa Valencia na AS Roma ambae sasa yuko Klabu ya kwaoARGENTINA_TEAM_JERSEYArgentina, Velez Sarsfield, ni mmoja wa Wachezaji watatu wa Nyumbani walioitwa kwenye Kikosi cha Argentina kwa ajili ya Mechi za Kanda ya Nchi za Marekani ya Kusini ya kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2014 zitakazochezwa huko Brazil lakini Straika wa Manchester City, Carlos Tevez, bado yupo nje baada ya kutoitwa kwa mara nyingine tena.

Pamoja na Gago, Wachezaji wengine wanaocheza ndani ya Argentina ni mwenzake wa Klabu ya Velez Sarsfield, Gino Peruzzi, na Kipa wa Boca Juniors, Agustin Orion.
Kuachwa kwa Carlos Tevez kwenye Timu ya Argentina ni kitu cha kawaida kwa Kocha wa Timu hiyo, Alejandro Sabella, ambaye hajamwita hata mara moja tangu Kocha huyo achukue madaraka Mwaka 2011.
Tevez ameichezea Argentina mara 62 na kufunga Goli 13.

Kwenye Mechi za Kanda ya Nchi za Marekani ya Kusini za kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2014, Argentina, ambao ndio Vinara, Ijumaa watacheza Nyumbani na Colombia na Siku 4 baadae watasafiri kuivaa Ecuador ambayo inashika Nafasi ya Pili.

KIKOSI KAMILI:

MAKIPA: Sergio Romero (Sampdoria), Mariano Andujar (Catania), Agustin Orion (Boca Juniors)

MABEKI: Pablo Zabaleta (Manchester City), Hugo Campagnaro (Napoli), Ezequiel Garay (Benfica), Federico Fernandez (Getafe), Fabricio Coloccini (Newcastle United), Jose Basanta (Monterrey), Marcos Rojo (Sporting Lisbon), Gino Peruzzi (Velez Sarsfield)

VIUNGO: Javier Mascherano (Barcelona), Fernando Gago (Velez Sarsfield), Ever Banega (Valencia), Walter Montillo (Santos), Jose Sosa (Metalist Kharkiv), Augusto Fernandez, (Celta Vigo), Lucas Biglia (Anderlecht), Pablo Guinazu (Libertad), Angel Di Maria (Real Madrid), Erik Lamela (AS Roma)

MAFOWADI: Lionel Messi (Barcelona), Gonzalo Higuain (Real Madrid), Ezequiel Lavezzi (Paris Saint-Germain), Rodrigo Palacio (Inter Milan), Sergio Aguero (Manchester City)

RATIBA

[Saa ni za Bongo, Kwenye Mabano Matokeo Mechi za Kwanza]

Ijumaa Juni 7
22:00 Bolivia v Venezuela [0-1]
00:05 Argentina v Colombia [2-1]

Jumamosi Juni 8
00:10 Paraguay v Chile [0-2]
02:10 Peru v Ecuador [0-2]

Jumanne Juni 11
22:30 Colombia v Peru [1-0]
23:00 Ecuador v Argentina [0-4]

Jumatano Juni 12
00:00   Venezuela v Uruguay [1-1]
00:30 Chile v Bolivia [2-0]

Jumapili Septemba 8
00:00 Colombia v Ecuador [0-1]
00:00 Chile v Venezuela [2-0]
00:00 Paraguay v Bolivia [1-3]
00:00 Peru v Uruguay [2-4]

MSIMAMO: 

NA
TIMU
P
W
D
L
F
A
GD
PTS
1

Argentina
11
7
3
1
24
8
16
24
2

Ecuador
10
6
2
2
16
10
6
20
3


Colombia
10
6
1
3
19
7
12
19
4

Chile
11
5
0
6
16
19
-3
15
5

Venezuela
11
4
3
4
9
12
-3
15
6

Uruguay
11
3
4
4
17
21
-4
13
7

Peru
10
3
2
5
11
15
-4
11
8

Bolivia
11
2
3
6
13
20
-7
9

9


Paraguay
11
2
2
7
8
21
-13
8

**FAHAMU: Timu 4 za Juu zitafuzu moja kwa moja kucheza Fainali za Kombe la Dunia 2014 huko Brazil na Timu ya 5 itakwenda kucheza Mechi ya Mchujo na Timu kutoka Kanda ya ASIA kupata Timu 1 ya kuingia Fainali.

No comments:

Post a Comment