Monday, June 3, 2013

KOMBE LA DUNIA 2014: JAPAN KUWA NCHI YA KWANZA KWENDA BRAZIL?

JAPAN-WC2014KANDA ya Nchi za Asia itamaliza hatua yake ya mwisho ya Mechi za Mchujo kwa Mechi za Makundi yake mawili Mwezi huu Juni na kesho Jumanne Mei 4 Japan inaweza kuwa Nchi ya kwanza Duniani kufuzu kutinga Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2014 huko Nchini Brazil.
 
Bara la Asia litaingiza moja kwa moja Timu 4 kwenye Fainali za Kombe la Dunia, mbili toka kila Kundi la michuano yao, na Timu ya 5 itapatikana baada ya Timu zitazoshika Nafasi za 3 kwenye Makundi kucheza Mechi kati yao na Mshindi kwenda kucheza na Timu kutoka Kanda ya Nchi za Marekani ya Kusini itakayomaliza Nafasi ya 5.

Kesho Jumanne Juni 4, Japan, wanaoongoza Kundi B  wakiwa na Pointi 13, watakuwa Nyumbani kucheza na Australia na wanahistaji sare tu ili watinge Brazil na kuwa Nchi ya kwanza Duniani kufanya hivyo lakini pia hiyo kesho wanaweza kuingia Fainali hata wakifungwa ikiwa tu Iraq, wanaocheza Ugenini, watashindwa kuifunga Oman.

Japan wangeweza kufuzu kwenda Brazil kwenye Mechi za Raundi iliyopita lakini walifungwa 2-1 bila kutegemewa walipocheza Ugenini na Jordan lakini Mechi hii na Australia, itakayochezwa huko Saitama World Cup Stadium ni ngumu kwa vile Australia wana Wachezaji wazoefu na wao wanasaka ushindi ili nao waweze kufuzu.

Matumaini ya Japan yapo kwa Wachezaji wao kina Keisuke Honda, Yuto Nagatomo na Shinji Kagawa huku Australia ikitegemea Kikosi chao chenye Wachezaji wakongwe ambao nusu yao wako kwenye Umri unaozidi Miaka 30.

Katika Mechi yao ya kwanza kwenye Kundi lao Timu hizi zilitoka sare ya Bao 1-1.



RATIBA MECHI ZILIZOBAKI:

Jumanne Juni 4

[Saa ni za Bongo, Kwenye Mabano Matokeo Mechi za Kwanza]

13:30 Japan v Australia [1-1]
13:00 Oman v Iraq [1-1]
16:15 Qatar v Iran [0-0]
 17:30 Lebanon v South Korea [0-3]

Jumanne Juni 11
8:00 Australia v Jordan [1-2]
11:00 South Korea  v Uzbekistan [2-2]
14:30 Iraq v Japan [0-1]
16:30 Iran v Lebanon [0-1]

Jumanne Juni 18
11:00 Australia v Iraq [2-1]
15:00 South Korea v Iran [0-1]
15:00 Uzbekistan v Qatar [1-0]
19:00 Jordan v Oman [1-2]

MSIMAMO:

KUNDI A
NA
TIMU
P
W
D
L
F
A
GD
PTS
1
Uzbekistan
6
3
2
1
6
4
2
11
2
South Korea
5
3
1
1
11
5
6
10
3
Iran
5
2
1
2
2
2
0
7
4
Qatar
6
2
1
3
4
7
-3
7
5
Lebanon
6
1
1
4
2
7
-5
4

KUNDI B
NA
TIMU
P
W
D
L
F
A
GD
PTS
1
Japan
6
4
1
1
14
4
10
13
2
Jordan
6
2
1
3
6
12
-6
7
3
Australia
5
1
3
1
6
6
0
6
4
Oman
6
1
3
2
6
9
-3
6
5
Iraq
5
1
2
2
4
5
-1
5

No comments:

Post a Comment