JUMAPILI,
Jiji la Manchester litarindima kwa pande zake mbili, ile ya Kibuluu na
ile Nyekundu, kukutana Uwanja wa Etihad kwa ajili ya Dabi ya 166 wakati
Manchester City itakapowakaribisha Mahasimu wao Mabingwa Manchester
United kwenye Mechi ya Ligi Kuu England huku Timu zote zikiwa na
Mameneja wapya kwa Msimu huu.
Man City wanae Manuel Pellegrini na Man United wanae David Moyes.
Hali za Wachezaji
Manchester City wanaweza kuwachezesha
Kiungo David Silva na Beki Micah Richards ambao wamepona maumivu yao
lakini Beki Gael Clichy hatarajiwi kucheza kwa sababu hajapona vyema
tatizo la Musuli za Pajani.
Manchester United wanaweza kumtumia
Danny Welbeck ambae inasemekana amepata afueni tatizo la Goti lakini
Phil Jones na Rafael bado hawajetengemaa maumivu yao.
++++++++++++++++++++++++++
REKODI:
MASHINDANO |
MAN CITY-USHINDI |
SARE |
MAN UNITED-USHINDI |
LIGI |
40 |
49 |
59 |
FA CUP |
3 |
0 |
6 |
LIGI CUP |
3 |
1 |
2 |
NGAO YA JAMII |
0 |
0 |
2 |
JUMLA |
46 |
50 |
69 |
++++++++++++++++++++++++++
MATOKEO MECHI ZA MWISHONI:
27 Jan 2010 Manchester United 3 Manchester City 1 [Carling Cup]
17 Apr 2010 Manchester City 0 Manchester United 1 [BPL]
10 Nov 2010 Manchester City 0 Manchester United 0 [BPL]
12 Feb 2011 Manchester United 2 Manchester City 1 [BPL]
16 Apr 2011 Manchester City 1 Manchester United 0 [FA Cup]
07 Aug 2011 Manchester City 2 Manchester United 3 [NGAO YA JAMII]
23 Oct 2011 Manchester United 1 Manchester City 6 [BPL]
08 Jan 2012 Manchester City 2 Manchester United 3 [FA Cup]
30 Apr 2012 Manchester City 1 Manchester United 0 [BPL]
09 Dec 2012 Manchester City 2 Manchester United 3 [BPL]
08 Apr 2013 Manchester United 1 Manchester City 2 [BPL]
++++++++++++++++++++++++++
Tathmini
Timu zote hizi mbili, baada Mechi 4,
zimefungana kwa Pointi zikiwa na Pointi 7 kila mmoja ikiwa ni Pointi 3
nyuma ya Vinara Liverpool.
Msimu huu, Man United walianza kwa
kuifunga Swansea City Bao 4-1, Sare 0-0 na Chelsea, kufungwa 1-0 na
Liverpool na kuichapa Crystal Palace Bao 2-0.
++++++++++++++++++++++++++
NINI WAMESEMA:
-PELLEGRINI: ‘Sijui nini kilitokea huko nyuma lakini kwa sasa najua tuna fikra zenye nguvu sawa na Man United au zaidi!’
-MOYES: ‘’Nina uzoefu wa
Dabi nyingi-huko Glasgow na Merseyside. Ni muhimu sana kwa Mashabiki. Ni
muhimu kwa Wachezaji lakini muhimu zaidi ni nini kitatokea mwishoni mwa
Msimu na nani yuko kileleni!’
++++++++++++++++++++++++++
Man City walianza kwa kuifunga Newcastle 4-0, kufungwa 3-2 na Cardiff City, kuifunga Hull City 2-0 na Sare ya 0-0 na Stoke City.
Nguzo muhimu kwa Man City ni Kiungo wao
Yaya Toure ambae Msimu huu ameanza kwa kutawala vizuri katikati ikiwa
pamoja na kufunga Bao pia likiwemo Bao kwenye Mechi ya Juzi ya UEFA
CHAMPIONZ LIGI, UCL, ambayo walishinda Ugenini kwa kuichapa Viktoria
Plzen Bao 3-0.
Nao Man United wamaimarisha Kiungo chao
walipomsaini Marouane Fellaini Septemba 2 na bila shaka ataongeza nguvu
kazi kuwakabili kina Yaya na Fernandinho.
Lakini, bila shaka, Man United nguzo zao
kubwa ni Washambuliaji wao, Robin van Persie na Wayne Rooney huku
Rooney akiwa juu kwa hivi sasa baada kung’ara mno kwenye Mechi ya UCL
Jumanne iliyopita Man United walipoicharaza Bayer Leverkusen Bao 4-2 na
Rooney kufunga Bao 2.
Hizo zilikuwa Bao zake za 199 na 200 kwa Man United na kumfanya awe wa 4 katika Listi ya Wafungaji Bora Klabuni hapo.
++++++++++++++++++++++++++
DONDOO MUHIMU:
-Rooney amefunga Bao 10
katika Dabi za Manchester sawa na Wafungaji Bora wa Dabi hii katika
Historia, Francis Lee na Joe Hayes, ambao wote wanatoka Man City, na
Jumapili akifunga yeye atatwaa Nambari Wani.
++++++++++++++++++++++++++
Kwa Rooney Uwanja wa Etihad humpa mafanikio kwani amefunga Bao 4 katika Mechi 3 za mwisho alizocheza na Man City.
Uso kwa Uso
-Msimu uliopita kwenye Ligi, Man United walishinda Etihad Bao 3-2 na Man City kushinda 2-1 Old Trafford.
-Katika Mechi 10 za mwisho za Ligi walizocheza kati yao, Man United wameshinda 6 na Man City 3.
-Katika Mechi 16 za Ligi Kuu ambazo Man United wamekwenda kucheza Nyumbani kwa Man City wameshinda 9, Man City 5 na Sare 2.
VIKOSI VINATARAJIWA:
MAN CITY [Mfumo: 4-2-3-1]:
-Hart
- Zabaleta, Kompany, Nastasic, Kolarov
-Toure, Fernandinho
-Navas, Aguero, Nasri
-Dzeko
MAN UNITED [Mfumo: 4-4-2]:
-De Gea
-Smalling, Ferdinand, Vidic, Evra
-Valencia, Carrick, Fellaini, Kagawa
-Rooney, Van Persie
Refa: Howard Webb
++++++++++++++++++++++++++
LIGI KUU ENGLAND
RATIBA:
[Saa za Bongo]
Jumamosi 21 Septemba
14:45 Norwich City v Aston Villa
17:00 Liverpool v Southampton
17:00 Newcastle United v Hull City
17:00 West Bromwich Albion v Sunderland
17:00 West Ham United v Everton
19:30 Chelsea v Fulham
Jumapili 22 Septemba
15:30 Arsenal v Stoke City
15:30 Crystal Palace v Swansea City
18:00 Cardiff City v Tottenham Hotspur
18:00 Manchester City v Manchester United
++++++++++++++++++++++++++
MSIMAMO:
NA |
TIMU |
P |
PTS |
1 |
Liverpool |
4 |
10 |
2 |
Arsenal |
4 |
9 |
3 |
Tottenham |
4 |
9 |
4 |
Man. City |
4 |
7 |
5 |
Man. United |
4 |
7 |
6 |
Chelsea |
4 |
7 |
7 |
Stoke City |
4 |
7 |
8 |
Newcastle |
4 |
7 |
9 |
Everton |
4 |
6 |
10 |
West Ham |
4 |
5 |
11 |
Southampton |
4 |
5 |
12 |
Cardiff |
4 |
5 |
13 |
Swansea |
4 |
4 |
14 |
Fulham |
4 |
4 |
15 |
Norwich |
4 |
4 |
16 |
Hull City |
4 |
4 |
17 |
Aston Villa |
4 |
3 |
18 |
Crystal Palace |
4 |
3 |
19 |
WBA |
4 |
2 |
20 |
Sunderland |
4 |
1 |
No comments:
Post a Comment