PATA ZAIDI:
MOURINHO KWA MATA: ‘BADILIKA AU BENCHI!’
Bosi wa Chelsea Jose Mourinho amemwambia Mchezaji wakeJuan Mata ni lazima abadilike ikiwa anataka namba Chelsea.
Mata, ambae amekuwa Mchezaji Bora
Chelsea kwa Misimu miwili iliyopita, amekuwa hapati namba tangu Jose
Mourinho aanze kazi hapo Chelsea mwanzoni mwa Msimu.
Msimu huu amecheza Mechi 3 tu-alitolewa
baada ya Dakika 65 na Aston Villa, kuchezeshwa Dakika 57 na Everton na
kucheza Dakika 23 Chelsea walipofungwa 2-1 na FC Basel kwenye UCL hivi
Juzi.
Mourinho ameweka bayana kuwa Nambari 10 wake ni Oscar na Mata inabidi abadili uchezaji wake ili apate namba.
Mourinho amesema: “Kuna vitu siwezi
kuongea na nyinyi. Lakini alicheza na Everton tangu mwanzo na hebu
chunguzeni uchezaki wake. Nataka kumjenga Oscar kama Namba 10 wangu.
Nataka Wachezaji wengine wawili, kutoka Winga, wakubali hilo na
kujifunza vitu ambavyo hawakuwa tayari kujifunza toka mwanzo. ”
Mourinho alitamka: “Mata alicheza na
Basel, si sawa na Ba na Mikel waliokuja kuokoa jahazi, alikuwepo Timu
ikiongoza 1-0 na alikuwa na kazi maalum. Ajifunze. Kitu kimoja ni
kumchezesha yeye pamoja na Ramires na Oscar, wao kuwabana Wapinzani na
Mata kucheza Namba 10 nyuma ya Straika ili asaidie kutoa mchango wa
Magoli kwa pasi safi, awajibike kwa sababu ana kipaji.”
Aliongeza: “Kingine ni kubadilika na
kufuata uchezaji wetu sasa. Wakati huu, Oscar ndie Namba 10 wangu, na
ukiniambia kuwa Oscar sie Mchezaji Bora Chelsea tangu Msimu uanze,
nitakupinga!”
Mourinho amekuwa akimchezesha Eden
Hazard Winga kushoto, Oscar nyuma ya Straika na kulia, kwenye Mechi na
Basel, alianza Willian.
Na Mourinho amesisitiza Oscar na Mata
wanaweza kucheza Timu moja lakini anataka Mata, anaetumia Mguu wa
kushoto, acheze Winga ya Kulia na pia awajibike kukaba Timu inapopoteza
Mpira.
MOYES KWA ROONEY: ‘BAKI MCHEZAJI MKUBWA!’
David
Moyes amempa changamoto Straika wake Wayne Rooney ahakikishe kuwa yeye
ni Mchezaji mkubwa wa Mechi kubwa huku Jumapili wakitarajiwa kusafiri
kwenda Etihad kucheza na Mahasimu wao Manchester City kwenye Dabi ya
Jiji la Manchester.
Rooney alisakamwa na sakata la kutaka
kuhama kufuatia kauli ya Meneja Mstaafu Sir Alex Ferguson Mwezi Mei kuwa
Mchezaji huyo anataka kuhama na kisha kuundamwa na kuumia lakini, hivi
sasa, kwa Mechi mbili alizoanza Rooney ameonyesha yuko moto na ameshahau
sakata hilo lililoleta utata.
Jumamosi iliyopita Rooney alianza Mechi
na Crystal Palace na kufunga Bao na Jumanne alicheza Mechi ya UCL na
Bayer Leverkusen na kufunga Bao 2.
Hivi Juzi, katika nia ya kusawazisha mambo, Sir Alex Ferguson aliibuka na kuzungumza kwa mara ya kwanza na kumsifia sana Rooney.
Sasa Moyes, ambae ndio anakumbana na
Dabi yake ya kwanza kama Meneja wa Man United, amesema anaamini sasa ni
wakati muafaka kwa Rooney kuonyesha cheche zake kama mmoja wa Wachezaji
Bora Duniani.
Moyes ametamka: “Nadhani mtazamo wa
Rooney ni kuwa yeye ni Mchezaji mkubwa wa Mechi kubwa. Anataka kuonyesha
hilo kwa kila Mtu. Na Watu wanakuja Mpirani kuona Wachezaji kama yeye
wakionyesha tofauti na kubadili Gemu na tunategemea atafanya hivyo. Kitu
muhimu ni kuwa abakishe fomu yake. Akiendelea kucheza kama hivi, Magoli
yatakuja tu!”
Rooney amefunga Bao 10 katika Dabi za
Manchester sawa na Wafungaji Bora, Francis Lee na Joe Hayes, ambao wote
wanatoka Man City, na Jumapili akifunga yeye atatwaa Nambari Wani.
Pia, Moyes alisema kwa Sir Alex Ferguson kuibuka na kumsifia Rooney ni jambo jema litakalosaidia sana.
Amesema: “Ukisifiwa na Mtu kama Sir Alex
basi kubali. Lakini tukumbuke ni Wayne mwenyewe aliejifikisha hapa.
Yeye ndie amefanya kazi ngumu.”
Aliongeza: “Ni Mwaka mkubwa kwake..Rekodi nyingi anaweza kuzipata. Ana Mwaka mkubwa kuelekea Kombe la Dunia.”
No comments:
Post a Comment