UEFA imetangaza kusimamisha Malipo ya
Mgao wao wa Fedha za Zawadi kwa Klabu 6 zinazoshiriki Mashindano ya UEFA
ya Msimu huu wa 2013/14.
Kusimamishwa huko kumeamriwa na Bodi ya Klabu ya Udhibiti Fedha, UEFA Club Financial Control Body (CFCB) ili uchunguzi ufanyike.
CFCB inaongozwa na Mwenyekiti Jean-Luc Dehaene ambae alikuwa Waziri Mkuu wa zamani wa Belgium.
++++++++++++++++++++++++++++
KLABU 6 ZILIZOSIMAMISHIWA MGAO:
-FC Astra Ploieşti (Roumania)
-FC Metalurh Donetsk (Ukraine)
-HNK Hajduk Split (Croatia)
-HŠK Zrinjski (Bosnia)
-Skonto FC (Latvia)
-Trabzonspor AŞ (Turkey).
++++++++++++++++++++++++++++
Ikiwa
ni hatua ya kuzingatia Sheria mpya za UEFA zinazotaka Klabu zijiendeshe
kwa Mapato yao wenyewe, Financial Fair Play Regulations (FFP), Klabu
zote zinazoshiriki Mashindano ya UEFA Msimu huu zilitakiwa zipeleke
Taarifa za Madeni yao ambayo hayajalipwa ya Kipindi kinachomalizika Juni
30.
Kufuatia Taarifa hizo, CFCB imeamua
kusimamisha Mgao kwa Klabu hizo 6 ambazo hazijalipa Madeni yao yakiwemo
yale ya Klabu nyingine, Wafanyakazi na Kodi za Nchi.
Kusimamishwa huko kutadumu hadi Madeni yakatapolipwa ama utakapotoka uamuzi mwingine wa CFCB.
Mbali ya Klabu hizo 6, Klabu nyingine 25 zimetakiwa kupeleka Taarifa zaidi kuhusu hali zao Kifedha.
Kwa mujibu wa Taarifa za UEFA, tangu
Sheria za FFP zianze kutumika Madeni ambayo hayajalipwa na Klabu
yamepungua kutoka Euro Milioni 57 ya hapo Juni 2011 na kufikia Euro
Milioni 9 hapo Juni 2013.
Pia UEFA imeripoti kuwa Hasara kwa Klabu imepungua kwa Euro Milioni 600 baada ya kuwa na ongezeko la Hasara kwa Miaka 6.
No comments:
Post a Comment