Friday, May 10, 2013

MZEE AKILIMALI AIBUKA - AMUOMBA MWAMUZI WA MECHI DHIDI YA SIMBA ACHEZESHE KWA HAKI - AHAIDI KIPIGO MSIMBAZI

 

 

 

Kuelekea mchezo dhidi ya Simba SC mei 18, Baraza wa wazee wa klabu ya Young Africans limeomba mwamuzi wa mchezo huo achezeshe kwa kufuata sheria 17 zote za mchezo na kwa kufanya hivyo mabingwa wapya wa Ligi Kuu ya Vodacom watoto wa Jangwani lazima wataibuka na ushindi katika mchezo huo.


Akiongea na wandishi wa habari kwa niaba ya baraza la wazee makao makuu ya klabu, katibu mkuu wa baraza la wazee Mzee Ibrahim Akilimali (Ibrahimovich) amesema wanaamini kikosi cha Yanga kitaibuka na ushindi katika mchezo huo ikiwa mwamuzi atachezesha kwa kufuata sheria zote 17 na kanuni za soka.


Akilimali amesema Yanga ni timu bora kwa sasa katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati kila mmoja anajua hilo, tuna wachezaji wazuri wenye kiwango cha hali ya juu ambao wamepikwa wakapikika wakaiva matunda ya mafunzo yao ndio yaliyotupatia ubingwa kabla ya ligi kumalizika.


Aidha aliongeza kuwa "Tunaahidi kwamba tutamfunga Simba SC siku ya mei 18 kutokana na umoja wetu, mshikamano na uongozi bora chini ya mwenyekiti Yusuf Manji na makamu wake Clement Sanga ambao mpaka sasa wameifnaya timu ya Yanga kuwa ya kuogopewa ukanda wote huuu".


Naye Mzee Hashim Mwika aliongeza kuwa waanahidi ushindi katika mchezo huo, idadi ya mabao haijalishi lakini kikubwa tunasema lazima tumfunge Simba mei 18 kikubwa tunaomba mwamuzi achezeshe kwa kufuata kanuni 17, na kama wakifanya hivyo basi Simba Sc wajiandae kupokea mvua ya mawe siku hiyo.


"Mwaka jana walitufunga kwa sababu hatukuwa pamoja, hatukua na maelewano lakini hivi sasa Yanga ni moja kuanzia viongozi, wachezaji, makocha na wanachama hivyo tunamini kwa kuwa pamoja na timu yetu bora lazima simba achezee kichapo "alisema mzee Mwika

KALI YA LEO: "KAMA UNAMPENDA KOCHA WAKO USIMSAJILI CAPTAIN WA ARSENAL"




 

1: Viera kwenda Juventus mwaka wa pili Capelo kaondoka

2: Thierry Henry kwenda Barca msimu wa pili Frank Rijkaard kaondoka

3: William Gallas kwenda Tottenham Spurs Redknapp kaondoka

4: Cesc Fabregas kwenda Barcelona Pep Guadiola msimu wa pili akaondoka

5: Van Persie kaenda Manchester United - Sir Alex Ferguson huyoooo Je, nani atamchukua Vermerleen?

ED WOODWARD MRITHI WA DAVID GILL NDANI YA MAN UNITED - ALIYE NYUMA YA MAFANIKIO YA KIBIASHARA YA MAN UNITED CHINI YA GLAZERS!

Ni mtaalam wa zamani wa mambo ya uwekezaji kwenye benki na mtu muhimu nyuma ya uongozi wa familia ya Glazer, ndio yupo nyuma ya mafanikio ya kibiashara ya Manchester United.


Wakati Ed Woodward, 40, anaweza asiwe na jina kubwa, ameweza kujenga sifa wakati wa miaka yake nane ndani ya Old Trafford. 
Na kipindi kijacho cha kiangazi Woodward atachukua nafasi ya ofisa mkuu wa Manchester United David Gill mbaye atastaafu.
Akiwa amehusika kwa kiasi kikubwa katika kuhakikisha familia ya Glazer inainunua klabu hiyo mwaka 2005, Woodward amekuwa mtu muhimu ndani ya klabu hiyo tangu wakati huo.

Akiwa kama msaidizi wa Gill, muingereza huyo amekuwa na jukumu la kuhakikisha mbinu za biashara za United zinakuwa bora, baada ya kuondoka kwa Gill 30 June, ataingia katika majukumu ya kisoka zaidi, yakiwemo masuala ya usajili na uhamisho  pamoja majadiliano ya mishahara ya wachezaji.

 Woodward anasifika sana kwa kuweza kufanikisha kupatikana kwa dili za mikataba mingi ambayo ilisababisha ongezeko kubwa la faida ndani ya miezi mitatu iliyopita - United wakitangaza faida ya £91 millioni kutoka mwezi January. 
 Kuanzia 2014, dili lingine kama la Chevrolet litaiwezesha United kulipwa na kampuni hiyo ya magari ya Marekani kiasi cha £51m kwa mwaka kutokana na udhamini wa jezi pekee yake.

Jukumu la kuiongoza United linaweza kuonekana kama kitu ambacho hakikutegemewa kwa mhitimu huyo wa fizikia wa Bristol University, japokuwa Woodward alianza kazi hiyo ya masuala ya uongozi huko PricewaterhouseCoopers akiwa kama mhasibu na mshauri wa masuala ya kodi mwaka 1993.
Mwaka 1999 alihamia JP Morgan, ambapo alifanya kazi kama ofisa mkuu wa masuala ya uwezekezaji katika masuala ya biashara za kimataifa.
Na mahala hapo ndipo alipokutana na Malcom Glazer n kumshauri ainunue Manchester United, na mwaka 2005 aliitwa kuajiriwa na United chini ya Glazers.
Mwanzoni alipewa jukumu la upangaji wa masuala ya fedha, kabla hajapewa jukumu la kuendesha biashara na masuala yote ya media ya Manchester United mwaka 2007 na baadae mwaka jana akawa mkurugenzi.

Woodward alikuwa hana uzoefu wowote wa kufanya kazi kwenye taasisi ya kimichezo kabla hajaja United, lakini alianza kuhudhuria vikao vya wana hisa wa premier league kwa pamoja na Gill mwaka 2012 katika jaribio la kumuongezea uelewa kuhusu siasa za soka.


Jukumu lake jipya litamfanya afanye kazi kwa karibu na Sir Alex Ferguson na mrithi wake David Moyes katika kuifanya brand ya Manchester United inafanikiwa kibiashara na kisoka kama ilivyokuwa chini ya David Gill.

BAADA YA KUANDAMWA SANA MASHABIKI WA MAN U - MKE WA ROONEY ASEMA "MUULIZENI ROONEY MWENYEWE SIO MIMI"

  Wakati Manchester United ikimtangaza David Moyes kuwa mrithi wa Sir Alex Ferguson, hatma ya mchezaji Wayne Rooney ndani ya Old Trafford imekuwa bado ya utata na kupelekea mashabiki wa klabu hiyo kuwa katika hali ya wasiwasi.

Taarifa mbalimbali zimekuwa zikisema mshambuliaji huyo amepeleka maombi ya kuondoka United kwa mara ya pili ndani ya miaka 3, akisema anahitaji changamoto mpya sehemu nyingine, huku vilabu vya Chelsea, PSG na Bayern Munich vikiwa tayari kutuma ofa kwa ajili ya kumsaini Muingereza huyo.





 Kutokana na sintofahamu hiyo kuhusu hatma ya Wayne Rooney ambaye sasa amebadilisha biography yake kwenye mtandao wa Twitter kutoka kuwa "mchezaji wa Manchester United mpaka kuwa NikeUK athlete" - mashabiki wa klabu wamekuwa wakimtumia tweets za vitisho na matusi kuhusu kutaka kuondoka Manchester United wakati huu timu ikiwa kwenye huzuni kubwa kwa kustaafu kwa Fergie.

Kama vile haitoshi baaada ya Wayne Rooney kukaa kimya bila kuwajibu chochote mashabiki ho kwenye Twitter wakamfuata mkewe Coleen Rooney na kuanza kumuuliza kama ni kweli wanataka kuondoka Manchester?

  
Mwanzoni Coleen alikaa kimya lakini baadae akashindwa kuvumilia na kuwatumia tweet moja mashabiki na kuwaambia kwamba "Mume wangu ana akaunti ya Twitter..... @WayneRooney muulizeni yeye sio mimi".

MOYES AFUNGUKA, NI WIKI HII TU ALIJUA SAFARI OLD TRAFFORD!

ASEMA OFA YA MAN UNITED HUWEZI KUIKATAA!!

MOYES_nFERGIE-NDEFU
DAVID MOYES amekiri hakuwa anajua kama Sir Alex Ferguson atastaafu Manchester United na yeye kuteuliwa kuwa Meneja huko lakini alipopewa ofa hakusita hata Sekunde moja.

Moyes amesema hatua hii ni kama ile alipotoka Preston North End Mwaka 2002 na kutua Everton.

Ametamka: “Nasikitika kuondoka Klabu safi kama Everton ambayo imekuwa sehemu ya maisha yangu lakini ukweli siwezi kuikataa ofa ya Man United!”

Ingawa Mkataba wake na Everton ulikuwa ukimalizika Juni 30, David Moyes alithibitisha hakuwa na mipango ya kuhama na alikuwa tayari yeye na Mwenyekiti wa Everton, Bill Kenwright, walikuwa wameshaandaa mipango ya Msimu ujao.

Moyes pia alimzungumzia Mtu atakaemrithi, Sir Alex Ferguson, na kutamka: “Hakuna Mtu aliefikiria ipo Siku Sir Alex Ferguson atastaafu. Tulidhani yeye ni Binadamu wa ajabu. Yeye ni mfano kwa kila Mtu. Heshima yangu kwake haielezeki. Tumetoka zama tofauti. Nimekua nikimwona yeye na Jock Stein ni Mashujaa, baadae nikashindana na Sir Alex. Sina neno lolote ala kumwelezea ambalo litamtendea haki Sir Alex Ferguson!’

Pia Moyes alizungumzia Mechi yake ya mwisho akiwa Meneja wa Everton Uwanja wa Nyumbani Goodison Park ambako Jumapili hii watacheza na Newcastle na kusema anatumaini Mashabiki watatoa heshima kama ile ya Siku ya kwanza yeye kutua hapo.

Mechi ya mwisho kabisa kwa David Moyes akiwa Meneja wa Everton ni hapo Mei 19 watakapocheza ugenini Stamford Bridge na Chelsea.

BPL: BARCLAYS PREMIER LEAGUE

RATIBA

Jumamosi Mei 11
[Saa 8 Dak 45 Mchana]
Aston Villa v Chelsea

Jumapili Mei 12
[Saa 9 na Nusu Mchana]
Stoke v Tottenham

[Saa 11 Jioni]
Everton v West Ham
Fulham v Liverpool
Norwich v West Brom
QPR v Newcastle
Sunderland v Southampton

[Saa 12 Jioni]
Man United v Swansea

Jumanne Mei 14
[Saa 3 Dak 45 Usiku]
Arsenal v Wigan

[Saa 4 Usiku]
Reading v Man City

Jumapili 19 Mei

MECHI ZA MWISHO ZA LIGI MSIMU HUU 

[Saa 12 Jioni]
Chelsea v Everton
Liverpool v QPR
Man City v Norwich
Newcastle v Arsenal
Southampton v Stoke
Swansea v Fulham
Tottenham v Sunderland
West Brom v Man United
West Ham v Reading
Wigan v Aston Villa


MSIMAMO:

FAHAMU: BINGWA TAYARI NI MANCHESTER UNITED!!

NA
TIMU
P
GD
PTS


1
Man Utd
36
42
85

2
Man City
36
31
75

3
Chelsea
36
34
69

4
Arsenal
36
31
67

5
Tottenham
36
18
66

6
Everton
36
14
60

7
Liverpool
36
25
55

8
West Brom
36
0
48

9
Swansea
36
0
46

10
West Ham
36
-8
43

11
Stoke
36
-10
41

12
Fulham
36
-11
40

13
Aston Villa
36
-21
40

14
Southampton
36
-11
39

15
Sunderland
36
-12
38

16
Norwich
36
-22
38

17
Newcastle
36
-23
38

18
Wigan
36
-23
35

19
Reading
36
-26
28

20
QPR
36
-28
25

*QPR & READING TAYARI ZIMESHUKA DARAJA!

SHAFFIH DAUDA APEWA SIKU 7 AJIELEZE ALIPATAJE BARUA YA FIFA

KAGERA SUGAR, SHOOTING KUUMANA KAITABA VPL
 
 SIMBA, MGAMBO SHOOTING ZAINGIZA MIL 16

PATA TAARIFA KAMILI:

TFF_LOGO12Release No. 081

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Mei 10, 2013

KAGERA SUGAR, SHOOTING KUUMANA KAITABA VPL

Kagera Sugar inaikaribisha Ruvu Shooting ya Pwani katika mchezo pekee wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) utakaofanyika kesho (Mei 11 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Kaitba mjini Bukoba.

Ingawa timu zote mbili hazipambani kutafuta ubingwa ambao tayari umetwaliwa na Yanga wala kukwepa kushuka daraja, mechi hiyo bado ni muhimu kwao katika mazingira matatu tofauti.

Kagera Sugar inayonolewa na kocha mkongwe kuliko wote katika VPL, Abdallah Kibaden na ikiwa na pointi 40 yenyewe inasaka moja kati ya nafasi nne za juu ambazo zina zawadi kutoka mdhamini wa ligi, lakini pia timu zinazoshika nafasi hizo za juu zinapata tiketi ya kucheza michuano ya BancABC Super 8.

Kwa upande wa Ruvu Shooting ya Kocha Charles Boniface Mkwasa yenye pointi 31 inasaka moja ya nafasi sita za juu ambazo ni fursa ya kuingia kwenye Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPL Board) ambayo inatarajiwa kuundwa baada ya uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Septemba 28 mwaka huu.

Wagombea nafasi za uenyekiti na makamu wake ni lazima watoke katika timu zilizoshika nafasi sita la juu katika VPL msimu uliopita. Uchaguzi wa TPL Board utafanyika siku moja kabla ya ule wa TFF uliopangwa kufanyika Septemba 29 mwaka huu.

Raundi ya 25 ya ligi hiyo itakamilika keshokutwa (Mei 12 mwaka huu) kwa mechi kati ya wenyeji Azam na Mgambo Shooting ya Tanga. Mechi hiyo namba 169 itachezwa katika Uwanja wa Azam Complex ulioko Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

Azam yenye pointi 48 inahitaji moja zaidi ili kutetea nafasi yake ya umakamu bingwa iliyoutwaa msimu wa 2011/2013 na kupata tiketi ya kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.

Wakati Azam ikisaka pointi hiyo moja, Mgambo Shooting inayofundishwa na wachezaji wa zamani wa mabingwa wa Tanzania Bara mwaka 1988, Mohamed Kampira akisaidiwa na Joseph Lazaro ni moja ya timu ziko katika hatari ya kurudi Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu ujao.

Mgambo Shooting inahitaji pointi moja tu katika mechi mbili ilizobakiza kukwepa kurudi FDL, ikishindwa kupata pointi hiyo huku Polisi Morogoro na Toto Africans ya Mwanza zikishinda mechi zao za mwisho kwa uwiano mzuri wa mabao itakuwa imekwenda na maji.

Mechi ya Azam dhidi ya Mgambo Shooting itachezeshwa na refa Jacob Adongo kutoka Mara, na atasaidiwa na Abdallah Rashid wa Pwani na Charles Mbilinyi wa Mwanza. Mwamuzi wa mezani atakuwa Idd Lila wa Dar es Salaam wakati Kamishna ni Omari Walii wa Arusha.

SIMBA, MGAMBO SHOOTING ZAINGIZA MIL 16

Mechi namba 149 ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Simba na Mgambo Shooting iliyochezwa juzi (Mei 8 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa Simba kushinda bao 1-0 imeingiza sh. 16,651,000.

Watazamaji 3,006 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo ambayo viingilio vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 3,226,125 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 2,539,983.05.

Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 1,640,402.54, tiketi sh. 3,175,000, gharama za mechi sh. 984,241.53, Kamati ya Ligi sh. 984,241.53, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 492,120.76 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 382,760.60.

TFF YATAKA MAELEZO YA BARUA YA FIFA KWA DAUDA

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limemtaka Shaffih Dauda ambaye ni mmiliki wa tovuti ya www.shaffihdauda.com kutoa maelezo kuhusiana na barua ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) aliyoiweka kwenye mtandao wake huo.

FIFA ambayo ilisimamisha mchakato wa uchaguzi wa TFF baada ya baadhi ya wagombea kuulalamikia, baadaye ilitoa maelekezo kuhusu mchakato huo kwa barua ambayo iliituma kwa Rais wa TFF, Leodegar Lenga.

Rais wa TFF katika mkutano wake na waandishi wa habari ambao Dauda alihudhuria alibainisha kuwa barua hiyo ya FIFA hawezi kupewa kila mtu, na kuruhusu waandishi kuisoma kwa Ofisa Habari wa TFF bila kuondoka nayo.

Wakati Rais Tenga anazungumza na waandishi wa habari (Mei 2 mwaka huu), nakala ya barua hiyo ya FIFA ilikuwa kwa viongozi wakuu wa TFF pekee, na viongozi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo. Hivyo TFF imemtaka Dauda kutoa maelezo ya mahali alipoipata barua hiyo ndani ya siku saba.

Boniface Wambura

Ofisa Habari

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

FA CUP-FAINALI: WIGAN v MAN CITY

JUMAMOSI MEI 11, SAA 1 NA ROBO USIKU UWANJANI WEMBLEY
 
WAMEPOKONYWA TAJI lao la Ubingwa wa England na Manchester United, wametupwa nje hatua ya Makundi ya UEFA CHAMPIONZ LIGI na sasa wamebakisha FA CUP tu kuokoa Msimu wao, na pengine kumnusuru Meneja wao Roberto Mancini, Manchester City Jumamosi watacheza Fainali na Wigan Athletic, Timu ambayo ipo hati hati kushushwa Daraja.

Hii ni Fainali ya 10 kwa Man City kwenye FA CUP na kwa Wigan ni Fainali ya kwanza tangu Timu yao ianzishwe Mwaka 1932.


WAPI WAMETOKA??

WIGAN:

-Raundi ya 3: Wigan 1 Bournemouth 1 MARUDIANO :Bournemouth 0 Wigan 1

-Raundi ya 4: Macclesfield Town  0 Wigan 1

-Raundi ya 5: Huddersfield Town 1 Wigan 4

-Raundi ya 6: Everton 0 Wigan 3

-NUSU FAINALI [Wembley]: Millwall 0 Wigan 2

MAN CITY:

-Raundi ya 3: Man City 3 Watford 0

-Raundi ya 4: Stoke City 0 Man City 1

-Raundi ya 5: Man City 4 Leeds United 0

-Raundi ya 6: Man City 5 Barnsley 0

-NUSU FAINALI [Wembley]: Man City2 Chelsea 2

FA_CUP-NEW_LOGO Kwa Man City, hii ni Mechi rahisi hasa kwa kukutana na Wigan Athletic ambayo kwenye Ligi, BPL,Barclays Premier League, ipo hatarini kushusuhwa Daraja.
Manchester City wanatinga Fainali ya FA CUP kwa mara ya 10 tangu kuundwa kwa Timu yao na wametwaa Kombe hili mara 5 katka Miaka ya 1904, 1934, 1956, 1969 na 2011.

Pia, Man United wameshatokea Washindi wa Pili mara 4 katika Kombe hli Miaka ya 1926, 1933, 1955 na 1981.

Man City wakiwa ndio wamechaguliwa kuwa ‘wenyeji’ kwenye Fainali hii, Wigan watalazikimika kuvaa Jezi zao za ugenini Nyeusi.

Hii itakuwa ni Fainali ya 132 ya FA CUP na ya pili kudhaminiwa na Budweiser, Kampuni ya Bia.

Mshindi wa Mechi hii hucheza EUROPA LIGI  kwa Msimu unaofuata lakini kwa vile Man City wameshafuzu UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI, kwa kutwaa nafasi ya Pili nyuma ya Mabingwa Manchester United kwenye BPL, Barclays Premier League, Wigan ndio watatwaa nafasi hii ya kucheza EUROPA LIGI.

MATOKEO KATI YAO MECHI ZAMWISHO: 

2012/2013
17 Apr Man City 1 Wigan 0
28 Nov Wigan 0 Man City 2

2011/2012
16 Jan Wigan 0 Man City 1
10 Sep Man City 3 Wigan 0

2010/2011
05 Mar Man City 1 Wigan 1
19 Sep Wigan 0 Man City 2

2009/2010
29 Mar Man City 3 Wigan 0
18 Okt Wigan 1 Man City 1.

Thursday, May 9, 2013

Robin Van Persie • Manchester United - Best Goals •Skills • Emotions 2013.

RIO FERDINAND, CARRICK WAMKARIBISHA DAVID MOYES MAN UNITED. . .

MWENYEKITI EVERTON KENWRIGHT AHUZUNIKA: “NI MENEJA BORA! MAN UNITED WANA BAHATI!

DAVID_MOYES WAKATI Wachezaji wa Manchester United, Rio Ferdinand na Michael Carrick, wakichekelea na uteuzi wa Meneja mpya David Moyes na kumkaribisha kwa furaha, Mwenyekiti wa Everton, Bill Kenwright, amesikitishwa na kuondoka kwake na kusema Man United wamebahatika sana kumpata.
Jumatano, Sir Alex Ferguson alitangaza kustaafu kuwa Meneja na leo Man United imemtangaza Mrithi wake kuwa ni David Moyes, Mtu ambae alipendekezwa na Sir Alex Ferguson mwenyewe.MOYES_n_FERGIE-POA
David Moyes amepewa Mkataba wa Miaka 6 na Man United ambao utaanza rasmi Julai 1.
Moyes, ambae Mkataba wake na Everton unamalizika Juni 30, ataisimamia Everton katika Mechi zake 2 zilizobakia za BPL, Barclays Premier League, ambazo watacheza na West Ham na kumaliza na Chelsea hapo Mei 19 Uwanjani Stamford Bridge.
Rio Ferdinand, ambae amecheza chini ya Ferguson kwa Miaka 10 huko Old Trafford, amesema: "Ilikuwa ni muhimu kwa Klabu kufanya uamuzi wa haraka kabla Watu hawajaanza kuleta uvumi. Hatujawahi kuwa na tatizo nae na Watu wanaomjua wanasema ni Mtu mwema aliefanya kazi nzuri huko Everton.”
Nae Michael Carrick amesema anachojua yeye ni kuwa Moyes ni mkweli kwa Wachezaji wake na Mchapa kazi aliefanya kazi njema Everton.

Mwenyekiti Everton- Bill Kenwright
Mwenyekiti wa Everton Bill Kenwright amemsifia Meneja wake David Moyes ambae anaondoka na kuanza kazi ya Umeneja huko Man United kuanzia Julai 1.
Kenwright, ambae ndie alimwingiza Moyes Goodison Park kutoka Preston North End Mwezi Machi 2002, amesema amehuzunishwa na kuondoka kwake.
Ametamka: “Huyu ni Meneja Bora na Man United wana bahati sana kumpata! Everton yote itahuzunika kuagana nae, ni Meneja Bora! Hatukuweza kumzuia Mkataba wake unakwisha na yeye kaamua kwenda Man United! Huwezi kumzuia!”
Licha ya kutofanikiwa kuchukua Kombe lolote akiwa na Everton kwa Miaka yake 11 aliyokuwa hapo kitu pekee na kikubwa kilichompa umaarufu ni kuiongoza Klabu masikini, isiyokuwa na Fedha kununua Wachezaji wakubwa, kubakia BPL na kuweza kushindana kiume na Klabu kubwa na Tajiri.


-ALIANZA kucheza Soka na  Celtic na kumalizia Preston ambako alicheza na Chipukizi David Beckham aliepelekwa hapo kwa mkopo na Man United kati ya Februari na Machi 1995
-BAADA ya kuifikisha Preston kwenye Fainali ya Mechi za Mchujo wa Daraja la Kwanza, Moyes akahamia Everton kama Meneja kumrithi Walter Smith hapo Machi 2002
-ALIMPA Wayne Rooney nafasi ya kucheza Mechi ya kwanza kwenye Ligi Agosti 2002 na kumuuza Man United Miaka miwili baadae kwa Pauni Milioni 20.
-ALIIFIKISHA Everton nafasi ya 4 kwenye Ligi Kuu Mwaka 2005 na kucheza UEFA CHAMPIONZ LIGI
-ALIIPELEKA Everton Fainali ya FA CUP Mwaka 2009 walipofungwa 2-1 na Chelsea baada ya kuitoa Man United kwenye Nusu Fainali