Saturday, June 1, 2013

RADAMEL FALCAO: RASMI ASAINIWA NA MONACO!

RADAMEL_FALCAO2Monaco wamekamilisha Uahamisho wa Dau la Pauni Milioni 50 wa kumchukua Straika wa Atletico Madrid Radamel Falcao.
 
Falcao, Raia wa Colombia mwenye Miaka 27, amekuwa pia akihusishwa na kuhamia Chelsea na Manchester City.

FALCAO-WASIFU:
 

-KUZALIWA: 10 Februari 1986

-URAIA: Colombia

-KLABU: River Plate (2005-2009); Porto (2009-2011) & Atletico Madrid (2011-2013)

-ATLETICO MADRID: Mechi 46 Magoli 35

-JE WAJUA? Falcao ndie Mchezaji wa kwanza kwenye UEFA SUPER CUP kupiga

Hetitriki Mwezi Septemba Mwaka jana Atletico Madrid walipoinyuka Chelsea 4-1.



Falcao amesaini Mkataba wa Miaka mitano na Monaco na usajili huo umelipiwa na Mmiliki wa Klabu hiyo, Dmitry Rybolovlev, Bilionea kutoka Urusi.
 
Akitangaza usajili huo, Rybolovlev alisema: “Ni fahari kubwa kumsaini mmoja wa Wachezaji bora Duniani na tuna imani ataisaidia Monaco!”

Wakiwa chini ya Kocha Claudio Ranieri, Msimu huu uliokwisha juzi waliibuka Mabingwa wa Daraja la Pili huko France na Msimu ujao watacheza Daraja la juu Ligue 1 na hali hiyo imewafanya waimarishe Kikosi chao na tayari wameshawasajili Wachezaji wawili hatari toka FC Porto, Joao Moutinho, Miaka 26, na James Rodriguez, Miaka 21, na pia Beki Mkongwe kutoka Real Madrid, Ricardo Carvalho, ambae amehamishwa bure baada kumaliza Mkataba wake.

MANCHESTER UNITED INAVYOZIZIDI BARCELONA NA REAL MADRID KWENYE KUINGIZA FEDHA NYINGI KWENYE UDHAMINI WA JEZI

 


Real Madrid, klabu inayoongoza kuwa thamani kubwa zaidi duniani ($3.3 billion), imesaini dili la udhamini wa jezi na kampuni ya Emirates ambao utaiingizia klabu hiyo $39 million kwa mwaka kwa kipindi cha miaka 5.

 
Dili hilo na kampuni ya ndege ya Dubai limeshindwa kuipa Madrid fedha nyingi kama ilivyo kwa vilabu vingine vya juu barani ulaya.


Ndio, Los Blancos watapata asilimia 30 zaidi ya walichokuwa wakipewa na mdhamini wa sasa Bwin. Lakini kiasi hicho wanacholipwa na Emirates ni kidogo ukifananisha na wanacholipwa Manchester United(yenye thamani ya $3.2 billion) na Barcelona($2.6 billion) kwenye mikataba yao ya udhamini wa jezi. Mashetani wekundu wameingia mkataba na Chevrolet utakaowaingizia kiasi cha $80 million kwa mwaka kuanzia msimu wa 2014-15 - kwa miaka 5, wakati Barcelona wana mkataba wa miaka mitano Qatar Foundation wenye thamani ya $44 million kwa mwaka - dili linaloanza mwezi ujao.

 

 Real Madrid walitakiwa kupewa angalau dili lenye thamani ya kuzidi lile la Barcelona - ikitajwa kuwa klabu yenye mafanikio zaidi kwenye karne hii, imeshinda mataji mengi zaidi ya La Liga na Champions League, pia kwa sasa ina mchezaji mkubwa na maarufu zaidi kwenye ulimwengu wa mitandao ya kijamii Cristiano Ronaldo.

  LISTI YA TIMU ZINAONGOZA KWA KUINGIZA FEDHA NYINGI KUPITIA UDHAMINI WA JEZI

 

LEO MOURINHO AMALIZA HIMAYA REAL BILA CASILLAS, RONALDO!

MOURINHO_KILIOLOPEZ MAJERUHI, KIPA NAMBARI 2 LEO KUCHEZA, RIZEVU KIPA WA B, CASILLAS NJE!!

NI MWENDELEZO WA BIFU: MOURINHO v CASILLAS!!
 
LEO Msimu wa La Liga unamalizika na pia leo ndio mwisho wa himaya ya Jose Mourinho ndani ya Real Madrid na amehakikisha anaondoka huku akizidi kumponda Kipa na Nahodha wa Mabingwa Spain, Iker Casillas, kwa kumtupa nje ya Kikosi chake na kumchagua Kipa Nambari 3 kucheza leo.

Inasemekana Casillas hata Benchi hatakaa na badala yake Kipa Nambar 4 ndio atakuwa Rizevu kwenye Mechi ya leo na Osasuna ambapo Antonio Adan, Miaka 26, akikaa Golini baada ya Kipa Nambari moja wa Real, Diego Lopez, kuumia.

Rizevu wa Kipa atanarajiwa kuwa Jesus Fernandez anaechezea Timu B.


LA LIGA-MECHI ZA MWISHO ZA MSIMU

RATIBA:
Real Madrid CF v Osasuna [SAA 12 JIONI]
FC Barcelona v Malaga CF [SAA 2 USIKU]

[ZOTE SAA 4 USIKU]
Celta de Vigo v RCD Espanyol
Deportivo La Coruna v Real Sociedad
Real Mallorca v Real Valladolid
Rayo Vallecano v Athletic de Bilbao
Sevilla FC v Valencia
Real Zaragoza v Atletico de Madrid
Levante v Real Betis
Granada CF v Getafe CF

Vile vile, Nyota wa Real, Cristiano Ronaldo, hatacheza Mechi ya leo ya kukamilisha Ratiba na Msimu kwa Real kwa vile watamaliza Nafasi ya Pili lolote litakalotokea kwenye Mechi za leo.

Bifu la Mourinho na Casillas ni la Siku nyingi kiasi ambacho hata Sentahafu wa Real, Pepe, anaetoka Nchi moja na Mourinho huko Ureno, aliwahi kubatuka kutaka Casillas aheshimiwa na jibu alilopata toka Mourinho ni kwanza yeye mwenyewe kupigwa Benchi.

Mourinho amedumu Miaka mitatu hapo Real na ingawa Mkataba wake unamalizika Mwakani hivi karibuni kulifikiwa makubaliano kwa Meneja huyo aondoke na inatarajiwa Msimu ujao atakuwa huko London na Timu ya Chelsea.


MSIMAMO:

TIMU

P
W
D
L
F
A
GD
PTS

FC Barcelona
37
31
4
2
111
39
72
97

Real Madrid CF
37
25
7
5
99
40
59
82

Atletico Madrid
37
22
7
8
62
30
32
73

Valencia
37
19
8
10
64
50
14
65

Real Sociedad
37
17
12
8
69
49
20
63

Malaga CF
37
16
9
12
52
46
6
57

Real Betis
37
16
7
14
56
55
1
55

Rayo Vallecano
37
16
4
17
48
64
-16
52

Sevilla FC
37
13
8
16
54
51
3
47

Getafe CF
37
13
8
16
43
55
-12
47

Levante
37
12
9
16
39
56
-17
45

RCD Espanyol
37
11
11
15
43
51
-8
44

Athletic Bilbao
37
12
8
17
42
63
-21
44

Real Valladolid
37
11
10
16
47
54
-7
43

Osasuna
37
10
9
18
31
46
-15
39

Granada CF
37
10
9
18
35
54
-19
39

Deportivo
37
8
11
18
47
69
-22
35

Celta de Vigo
37
9
7
21
36
52
-16
34

Real Zaragoza
37
9
7
21
36
59
-23
34

Real Mallorca
37
8
9
20
39
70
-31
33

Friday, May 31, 2013

GERMAN DFB POKAL: JUMAMOSI, BAYERN MUNICH v VfB STUTTGART

FAINALI: JUMAMOSI JUNI 1,  SAA 12 JIONI, OLYMPIASTADION, BERLIN

BAYERN YATAKA HISTORIA YA TREBO, BRAZIL YAWATIBUA!!

DANTE BAADA ya kutwaa Ubingwa wa Bundesliga na UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI, Bayern Munich wana nafasi ya kuweka historia hapo Jumamosi ya kuwa Klabu ya kwanza ya Kijerumani kutwaa ‘TREBO’ ikiwa wataifunga VfB Stuttgart kwenye Fainali ya German Cup, maarufu kama German DFB Pokal, lakini azma hiyo imeingia dosari baada ya Brazil kuzuia baadhi ya Wachezaji wao kuichezea Klabu yao.

Mzozo huu umemfanya Mwenyekiti wa Bayern Munich, Karl-Heinz Rummenigge, apandishe na kudai hilo halikubaliki baada ya Shirikisho la Soka la Brazil, CBF, kuwazuia Wachezaji wa Bayern Munich, Kiungo Gustavo na Sentahafu Dante, kutocheza Fainali hiyo na badala yake kutakiwa kuripoti Kambini Nchini Brazil Siku ya Alhamisi kuanza maandalizi ya Nchi hiyo kwa ajili ya Mashindano ya FIFA ya Kombe la Mabara yanayoanza kuchezwa Juni 15 Nchini Brazil.

Juni 2, Brazil watacheza Mechi ya Kirafiki na England Uwanja wa Maracana Jijini Rio De Janeiro.

Rummenigge amedai Wachezaji hao wa Brazil wametishwa kwamba hawatachukuliwa tena kuichezea Brazil wakichelewa kupiga ripoti Kambini.

Wakati Bayern wanadai huo ni ukatili, CBF, kupitia Mkurugenzi wao wa Ufundi, Carlos Alberto Parreira, amesema wao waliwapelekea DFB Barua yenye heshima ya kuelezea msimamo wao.

Hata hivyo Rummenigge amekiri wenye makosa ni wao wenyewe Germany, hasa Shirikisho la Soka, DFB, kwa kuipanga Fainali ya German DFB Pokal kuwa Juni 1, tarehe ambayo ipo kwenye Kalenda ya FIFA ya Mechi za Kimataifa.
 

ZIARA ZA KLABU KABLA MSIMU MPYA: KLABU ZA ENGLAND

BPL_LOGOKLABU kadhaa za BPL, Barclays Premier League, zimetoa Ratiba zao za awali za Ziara zao za kabla Msimu mpya wa 2013/14 kuanza na Klabu nyingi Vigogo, zikiwemo Mabingwa Manchester United, Man City, Chelsea, Arsenal na Liverpool, zitakuwa huko Bara la Asia na huo ni msisitizo wa umuhimu wa Soko la Bara hilo.
 
Msimu mpya wa BPL utaanuliwa rasmi hapo Agosti 11 kwa ile Mechi maalum ya kugombea NGAO YA JAMII kati ya Mabingwa Man United na Washindi wa FA CUP Wigan.
Baada ya Mechi hiyo, BPL itaanza rasmi Msimu wake Wiki moja inayofuatia.

PATA RATIBA ZA AWALI ZA ZIARA  KABLA MSIMU MPYA WA 2013/14 KUANZA:

[PRE-SEASON TOURS]

[Saa zikitajwa ni za Bongo]

**FAHAMU: Ratiba hii itakuwa ikirekebishwa kadri itakavyothibitishwa.

RATIBA YA AWALI

ARSENAL
Julai 14 Indonesia XI (Gelora Bung Karno Stadium, Jakarta) [1630]
Julai 17 Vietnam (My Dinh National Stadium, Vietnam) [1500]
Julai 22 Nagoya Grampus (Toyota Stadium, Japan) [1330]
Julai 26 Urawa Red Diamonds (Saitama Stadium, Japan) [1330] 
Agosti 3 Napoli (Emirates Cup)
Agosti 4 Galatasaray (Emirates Cup)

+++++++++++++++++++++++++++++

ASTON VILLA
Julai 10 SV Rodinghausen (Wiehenstadion, North Rhine-Westphalia) [2000]
Julai 12 SC Paderborn (Benteler Arena, Paderborn) [1900]
Julai 14 VFL Bochum (Rewirpowerstadion, Bochum) [1330]
Julai 20 Wycombe (Adams Park) [1700]
Julai 23 Luton (Kenilworth Road) [2145]
Julai 26 Crewe (Alexandra Stadium) [2130]
Julai 31 Walsall (Bescot Stadium) [2130]
Agosti 4 Shamrock Rovers (Tallaght Stadium) [1600]
Agosti 10 Malaga (Villa Park) [1700]
 
+++++++++++++++++++++++++++++

CARDIFF
Julai 24 Forest Green Rovers (New Lawn) [2145]
Julai 27 Cheltenham (Abbey Business Stadium) [1700]
Julai 30 Brentford (Griffin Park) [2145]

+++++++++++++++++++++++++++++

CHELSEA
Mei 24 Manchester City (Busch Stadium, St Louis) KIPIGO 3-4
Mei 25 Manchester City (Yankee Stadium, New York) KIPIGO 3-5
Julai 17 Singha All-Stars (Rajamangala Stadium, Bangkok - Singha 80th Anniversary Cup) [1600]
Julai 21 Malaysia XI (Kuala Lumpur - BNI Cup 2013) [1630]
Julai 25 BNI Indonesia All-Stars (Gelora Bung Karno National Stadium, Jakarta) [1600]
Agosti 2 Inter Milan (Lucas Oil Stadium, Indianapolis - Guinness International Champions Cup) [0300]
 
+++++++++++++++++++++++++++++

CRYSTAL PALACE
Julai 23 Gillingham (Priestfield Stadium) [2130]

+++++++++++++++++++++++++++++

EVERTON
Agosti 1 Juventus (AT&T Park, San Francisco - Guinness International Champions Cup) [0600]

+++++++++++++++++++++++++++++

FULHAM
-KUTANGAZWA BAADAE

+++++++++++++++++++++++++++++

HULL CITY
Julai 15 North Ferriby United (Grange Lane) [2130]
Julai 20 Sheffield Wednesday (Estadio Municipal de Albufeira) [2200]
Julai 27 Birmingham (St Andrew's) [1700]
Julai 29 Peterborough (London Road) [2145]

+++++++++++++++++++++++++++++

LIVERPOOL
Julai 20 Indonensia XI (Gelora Bung Karno National Stadium, Jakarta) [1630]
Julai 24 Melbourne Victory (Melbourne Cricket Ground, Melbourne) [1300]
Julai 28 Thailand (National Stadium, Bangkok) [1400]
Agosti 2 Olympiacos (Anfield - Steven Gerrard testimonial) [1600]
 
+++++++++++++++++++++++++++++

MANCHESTER CITY
Mei 24 Chelsea (Busch Stadium, St Louis) USHINDI 4-3
Mei 25 Chelsea (Yankee Stadium, New York) USHINDI 5-3
Julai 14  (South Africa) 
Julai 18  (South Africa) 
Julai 24 Tottenham/Sunderland/South China (Hong Kong - Barclays Asia Trophy) 
Julai 27 Tottenham/Sunderland/South China (Hong Kong - Barclays Asia Trophy) 
Julai 31 Bayern Munich/AC Milan/Sao Paulo (Allianz Arena, Munich - Audi Cup) 
Agosti 1 Bayern Munich/AC Milan/Sao Paulo (Allianz Arena, Munich - Audi Cup)
 
+++++++++++++++++++++++++++++

MANCHESTER UNITED
Julai 13 Singha All Star XI (Rajamangala Stadium, Bangkok - Singha 80th Anniversary Cup) 
Julai 20 A-League All Stars (ANZ, Stadium, Sydney) 
Julai 23 Yokohama F-Marinos (Nissan Stadium, Yokohama) 
Julai 26 Cerezo Osaka (Osaka Nagai Stadium, Osaka) 
Julai 29 Kitchee (Hong Kong Stadium, Hong Kong)
 
+++++++++++++++++++++++++++++

NEWCASTLE
RATIBA KUTANGAZWA BAADAE

+++++++++++++++++++++++++++++

NORWICH
Julai 18 Dorados De Sinaloa (Raley Field, Sacramento) [0530]
Julai 21 San Jose Earthquakes (Buck Shaw Stadium, California) [0530]Julai 25 Portland Timbers (Jeld-Wen Field, Portland) [0600]
 
+++++++++++++++++++++++++++++

SOUTHAMPTON
RATIBA KUTANGAZWA BAADAE

+++++++++++++++++++++++++++++

STOKE
Julai 25 Houston Dynamo (BBVA Compas Stadium, Houston) [0400]
Julai 27 FC Dallas (FC Dallas Stadium, Dallas)
 
+++++++++++++++++++++++++++++

SUNDERLAND
Julai 24 Tottenham/Manchester City/South China (Hong Kong - Barclays Asia Trophy) 
Julai 27 Tottenham/Manchester City/South China (Hong Kong - Barclays Asia Trophy)
 
+++++++++++++++++++++++++++++

SWANSEA
RATIBA KUTANGAZWA BAADAE

+++++++++++++++++++++++++++++

TOTTENHAM
Mei 24 Jamaica (Thomas A. Robinson National Stadium, Bahamas) 1am - Sare 0-0
Julai 24 Manchester City/Sunderland/South China (Hong Kong - Barclays Asia Trophy) 
Julai 27 Manchester City/Sunderland/South China (Hong Kong - Barclays Asia Trophy)
 
+++++++++++++++++++++++++++++

WEST BROM
Julai 18 Hannover 96 (Stadionstrasse, Gleisdorf) [2200]

+++++++++++++++++++++++++++++

WEST HAM
Julai 7 Cork City (Turners Cross Stadium, Cork City) [2000]
Julai 10 Boreham Wood (Meadow Park) [2130]
Julai 13 Bournemouth (Goldsands Stadium) [1700]
Julai 16 Colchester (Weston Homes Community Stadium) [2145]
Julai 23 Hamburg (Flensburg) [2045]
 

LUIS SUAREZ: 'NI WAKATI MUAFAKA KUONDOKA!'

SUAREZ_n_IVANOVICSTRAIKA wa Liverpool Luis Suarez amesema sasa ni wakati muafaka kwa yeye kuondoka lakini hajafanya uamuzi wowote kuhusu nini afanye baadae.
 
Suarez, Miaka 26, ambae kwa sasa yupo kwenye Adhabu ya kufungiwa Mechi 10 kwa kumng’ata Beki wa Chelsea Branislav Ivanovic, amekiri ni vigumu kuikataa Real Madrid huku kukiwa na uvumi wa yeye kuunganishwa na kuhamia Klabu hiyo.

Amesema: “Ni wakati muafaka kubadilisha mazingira kwa sababu ya yale yaliyonitokea  huko England. ”

Suarez: 

-Goli 30 kwa Mechi 44 alizochezea Liverpool Msimu wa 2012/13 

-Tangu ajiunge Liverpool kutoka Ajax Januari 2011, amefunga Goli 51 katika Mechi 96. 

-Alifunga Bao 49 katika Mechi 48 alizochezea Ajax kabla kujiunga Liverpool 

-Amefunga Bao 31 kwa Mechi 62 alizochezea Uruguay 


Aliongeza: "Sijui wapi nitakwenda na sijui kama nitabaki!"

Suarez, ambae pia alifungiwa Mechi 8 kwa kumkashifu Kibaguzi Beki wa Manchester United Patrice Evra Mwaka 2011, aliongeza: “Ni wajibu kuishukuru Klabu, na Mashabiki wa Liverpool. Lakini kwa jinsi ninavyotendewa na waliobaki huko England imefanya Wiki hizi zilizopita kuwa ngumu. Liverpool ni Klabu ya ajabu lakini wanajua jinsi ninavyotendewa na Vyombo vya Habari!”

Suarez alijiunga na Liverpool kutoka Ajax Mwaka 2011 kwa Dau la Pauni Milioni 22.7 na Msimu uliopita alifunga Bao 30 lakini alizikosa Mechi mbili za mwisho za Ligi alipoanza kutumikia Kifungo chake cha Mechi 10 kwa kumuuma Ivanovic.

MAN UNITED: NANI KUIMARISHA KIUNGO?

FABREGAS, ALCANTARA AU STROOTMAN??
 CESC_FABREGAS
KEVIN_STROOTMAN
INAAMINIKA, kitu cha kwanza kabisa kwa Meneja mpya wa Manchester United, David Moyes, ni kuimarisha Idara ya Kiungo ya Timu hiyo ambayo Miaka nenda rudi ndio dhaifu kupita nyingine na udhaifu huo unazidi baada ya kustaafu kwa Paul Scholes, kufifia kwa Anderson, kutotabirika kwa Tom Cleverley na umri kuyoyoma kwa Michael Carrick lakini ‘wakombozi’ wanatajwa kuwa ni Cesc Fabregas na Thiago Alcantara wa Barcelona na Kevin Strootman wa PSV.

NANI WANAFAA NA NANI WATAPATIKANA?
Habari za ndani ya Barcelona zinasema kuwa wao wako tayari kumuuza Cesc Fabregas ikiwa Klabu itafikia Dau la Pauni Milioni 25 kiwango ambacho Man United wako tayari kulipa lakini inaelekea Dau hilo linaweza kupanda baada ya Man City kutia mkono na wao kuonyesha nia ya kumnunua Kiungo huyo mwenye akili ya mpira ambae alikuwa Nahodha wa Arsenal.
Thiago_Alcantara
Hata hivyo, Klabu hizo za Jijini Manchester zinaweza tu kumnasa Fabregas, mwenye Miaka 26, ikiwa tu Arsenal itatamka kuwa haitaki kumnunua kwa vile Mkataba wake wa kumuuza kwa Barcelona una kipengele kuwa hawezi kuuzwa Klabu nyingine hadi Arsenal ithibitishe haitaki kumnunua.

Zipo dalili Arsenal haitaki kumrudisha Fabregas na kilichobaki ni Klabu ipi ya Manchester itamnasa ingawa dalili zinaonyesha David Moyes ana nia kubwa ya kumfanya Fabregas kuwa Mchezaji wake wa kwanza kumsaini ili aungane na mwenzake aliekuwa nae Arsenal kwa muda mrefu, Robin van Persie.

Wengine wanaotazamwa na Man United kuimarisha Kiungo ni Mchezaji Chipukizi wa Barcelona, Thiago Alcantara na Nahodha wa PSV Kevin Strootman.

Wakati Alcantara ni ‘kinda’, Strootman ni Mchezaji mrefu na mzoefu anaemudu pozisheni zote za Kiungo, iwe Kiungo Mkabaji au Kiungo Mshambuliaji, kitu kinachomfanya awe na uhakika wa kupata namba endapo atatua Old Trafford.

Kiungo gani atatua Old Trafford ndio sakata linalosubiriwa kwa hamu kabla Msimu mpya kuanza hapo Agosti 11 kwa pambano la Fungua Pazia Msimu Mpya la kugombea Ngao ya Jamii kati ya Mabingwa Man United na Mabingwa wa FA CUP Wigan.