Sunday, September 22, 2013

VITA YA FELLAINI DHID YA YAYA TOURE ITACHANGIA SANA MATOKEO YA MWISHO YA MANCHESTER DERBY LEO HII

Mbio za usajili wa kiungo wa kati katika klabu ya Manchester United zilileta vituko na maneneo mengi sana katika dirisha la 

Cesc Fabregas alikuwa chaguo la kwanza lakini kadri muda ulivyokuwa ukienda ndivyo ilivyoonekana wazi asingeweza kuondoka Barca. Kiungo wa Athletic Bilbao Ander Herrera alikuwa kiungo mwingine aliyetakiwa kama ilivyokuwa kwa Luka Modric. Na wakati Arsene Wenger akivunja kibubu na kulipa kiasi cha £42.5million kwa ajili ya Mezut Ozil katika siku ya mwisho ya usajili, David Moyes akarudi kwenye klabu yake ya zamani na kumsajili mchezaji wa Everton Marouane Fellaini kwa ada ya uhamisho wa £27.5m – usajili ambao umemfanya mchezaji wa zamani wa United Teddy Sheringham kusema kwamba klabu yake ya zamani imemsajili mtu asiye sahihi. 

Wakati ikiwa bado mapema sana, kiwango cha United katika mchezo wa Champions League dhidi ya Bayer Leverkusen, ambao  Fellaini alianza, unaonyesha kwamba Moyes alimpata mchezaji ambaye alikuwa anatakiwa na kuliliwa sana Old Trafford.

Mchezaji ambaye hatofautiani sana na kiungo wa Manchester City Yaya Toure. Na Moyes akiwa anajiandaa na derby yake ya kwanza leo hii, upande mwekundu wa jiji la Manchester unaweza ukawa umempata mtu sahihi waliyekuwa wakimhitaji kwenye kiungo ambaye anaongeza uimara wa safu ya kiungo kama ilivyo kwa Yaya Toure kwa City.

Ni kweli, Fellaini anaweza akawa hana kipaji cha Ozil au jicho la pasi nzuri kama Fabregas, lakini mbelgiji huyu ameongeza kitu kikubwa katika safu ya kiungo ya United, dhidi ya Bayer wachezaji kama Robin van Persie, Wayne Rooney, Antonio Valencia na Shinji Kagawa, walipata uhuru mkubwa wa kucheza wakiwa na ulinzi mzuri wa Fellaini na ndio maana waliweza kuleta madhara makubwa kwa wapinzani wao. 

Kitu kama hicho ndicho Toure anachokifanikisha kwa timu ya City - kuwafanya washambuliaji wacheze kwa uhuru chini ya ulinzi wake.
Kama ilivyoonekana katika ya Crystal Palace na Bayer Leverkusen - Moyes atakuwa akimtumia zaidi Fellaini katika kiungo cha kuziua pembeni ya Micheal Carrick. 
Kule City, Toure, amekuwa akitumika kwa namna mbili kama kiungo wa juu na muda mwingine akicheza chini zaidi, kwa sasa akiwa anashirikiana na kiungo aliyesajiliwa kwa £30million Fernandinho.

SIFA ZAO ZA KIMWILI


UREFUUZITO
Yaya Toure189cm90kg
Marouane Fellaini194cm95kg


Kiukweli kabisa katika dunia ya soka hivi sasa ni wachezaji wachache wanaweza kucheza anavyocheza kiungo wa Ivory Coast, akitumia zaidi nguvu, akili katika kuitawala safu yote ya kiungo. 
Moyes atakuwa akiomba na kutumaini Fellaini, kiungo mkabaji wa kwanza kusajiliwa na timu hiyo katika kipindi cha miaka sita, ataweza kucheza kama anavyocheza Toure katika safu ya kiungo ya United. 
Akiwa Fellaini atacheza kama alivyocheza usiku wa Jumanne, basi vita ya safu ya kiungo baina yake na Toure itachangia sana katika matokeo ya mwisho ya mchezo huo unaopigwa katika dimba la City of Manchester Stadium jumapili ya leo.
 
TAKWIMU ZA FELLAINI VS YAYA TOURE MSIMU ULIOPITA

AZAM FC VS YANGA: WACHEZAJI WAKIRI KUVURUNDA NA WAAHIDI USHINDI LEO DHIDI YA YANGA


Wachezaji wa Azam FC kwa pamoja wameahidi ushindi katika mchezo wa leo dhidi ya Yanga utakaochezwa kwenye uwanja wa taifa, Azam FC ikiwa nyumbani.

Ahadi hiyo ilitolewa na wachezaji mbele ya viongozi wao (Makocha Kaly Ongala na Ibrahim Shikanda, Mwenye kiti Said Muhammad, Katibu Mkuu Nassor Idrissa na Mratibu wa timu hiyo Patrick Kahemele) kwenye kikao cha pamoja kati ya wachezaji na viongozi kutathmini mwenendo wa timu hiyo baada ya mechi nne za mwanzo za ligi kuu.

Wachezaji wa Azam FC wakiongozwa na John Bocco, Jabir Aziz na Salum Abubakar, walisema matokeo ya sare nyingi walizopata katika mechi zilizopita hayatokani na matatizo ya huduma isipokuwa ni mitihani ya kawaida kwenye soka ambapo timu inaweza kucheza vizuri nab ado ikashindwa kupata matokeo. Wachezaji wameahidi kuongeza nguvu kwa kuanzia mechi ya leo ili kupata matokeo ya ushindi badala ya sare.

Wachezaji kwa pamoja walionesha masikitiko yao kwa matokeo yaliyopita na kuahidi kuongeza kujituma kwenye mazoezi na mechi ili kurudisha makali yaliyoifanya Azam FC kuwa timu ya kuogopwa.

Azam FC itashuka uwanjani leo kukwaana na Yanga SC ambapo katika mechi nne zilizopita Azam FC imeambulia kipigo toka kwa Yanga. Lakini timu zote mbili zinashuka uwanjani zikiwa na matokeo ya kufanana na idadi sawa ya pointi baada ya kucheza michezo minne kila moja, kusinda mmoja na kutoka sare michezo mitatu hivyo kuwa na pointi sita.

Azam FC leo itamkosa Agrey Morris Ambrose ambaye alipewa kadi nyekundu kwenye mechi iliyopita dhidi ya Ashanti United na nafasi yake itajazwa na David Mwantika.

SOURCE: AZAM FC WEBSITE