Monday, August 27, 2012

Madrid yamnasa Modric




Klabu ya Tottenham Hotspurs imetangaza rasmi kukubaliana na Real Madrid katika kumsajili kiungo wa timu hiyo Luka Modric na anasubiriwa kupimwa afya na klabu hiyo ya LaLiga.

Kutokana na maelezo ya mtandao wa Spurs, yalisema kuwa, “ Makubaliano yameafikiana na yamebakia makubaliano binafsi baina ya mchezajina klabu hiyo.”

Naye Raisi wa Real Madrid, Florentino Perez Rodriguez amefurahishwa na kitendo cha kufanikishwa kwa usajili wa mchezaji huyu.

“Mahusiano mazuri kati yetu na Spurs yamepelekea kukubaliana katika usajili wa Modric. Tunafuraha kumkaribisha Lika Modric na tutaendelea kufanya kazi na Tottenhammiaka ijayo.” Perez aliuambia mtandao wa Spurs.

“Modric amekuwa mchezaji muhimu kwetu na tulitamani abaki na sisi kwa muda zaid, lakini tunafuraha kwa luwa Real Madrid, klabu ambayo tunategemea kushirikiana nayo na kuwa nayo karibu sana katika soka”

Luka aliichezea Tottenham mechi 160, akifunga magoli 17, baada ya kujiunga nayo akitokea Dinamo Zagreb mwaka 2008.

No comments:

Post a Comment