Saturday, September 1, 2012

Fergie: Evra ajiandae kuwania namba

LONDON, England
ALEX Ferguson amemtaja beki Patrice Evra kama 'Askari wa Kweli' anayecheza kwa kujituma na mwenye moyo wa ushindi.

Ferguson amesema hayo wakati akimkaribisha beki mpya, Alexander Buttner ambaye ataziba pengo la Evra.

Evra, Mfaransa aliyecheza Man United mfululizo kwa miaka sita, atakabiliwa na wakati mgumu wa kuwania namba na Buttner aliyetua Old Traffor kwa ada ya uhamisho ya paundi 4 milioni.

Bosi wa United alisema: “Lazima tujipange kwa ajili ya baadaye. Evra ana miaka 31 na Alex amekuja pia kucheza nafasi ya Evra.

“Lakini hakuna aliyecheza mechi nyingi kuliko Evra katika kipindi cha miaka sita iliyopita. Amecheza akiwa majeruhi...ni mtu wa kujituma.

“Amepita kwenye mechi kwa miaka mitano. Sasa ni mechi 240 ameshacheza. Patrice amekuwa askari shujaa.

Evra amecheza mechi 291 katika kipindi cha miaka sita tangu alipojiunga kwa ada ya uhamisho paundi 5.5 milioni kutoka klabu ya Monaco.

Lakini sasa Fergie yuko tayari kufanya marekebisho kwenye kikosi chake kwa kumchezesha mlinzi Buttner raia wa Ufaransa.

Buttner (23) awasili kutoka Vitesse Arnhem na anaungana na Shinji Kagawa, Nick Powell, Angelo Henriquez na Robin van Persie kukamilisha usajili wa kipindi cha majira ya joto.

Ferguson aliongeza: “Tumekuwa tukimfuatilia Alex kwa muda sasa, anacheza kwa nguvu, anapanda kushambulia na kurudi haraka kulinda.

Huu Ndio baadhi ya usajili wa dakika za mwisho.

 Edinson Cavan amesaini mkataba mpya wa kuendelea kuichezea Napoli na kuzima uvumi wa kutaka kujiunga na Chelsea.

 Nigel De Jong ameondoka rasmi Manchester City na kujiunga na AC Milan kwa ada ya uhamisho ya £3.4million


 Gael Kakuta ameenda kwa mkopo Vitesse Arnhem kutokea Chelsea

 Yossi Benayoun amekamilisha uhamisho wa kujiunga na West Ham kwa mkopo wa mwaka mmoja.

 Liverpool wamepigwa bao na Tottenham baada ya Clint Dempsey kujiunga na Spurs dakika za mwisho kutoka Fulham kwa ada ya uhamisho wa £6million.

 Stephen Mbia yupo Loftus Road akikamilisha vipimo vya afya kwa ajili ya kujiunga na QPR.



 Matija Nastasic amekamilisha uhamisho wake kutoka Fiorentina na kujiunga na Mannchester City, na anakuwa mchezaji wa 3 kujiunga na mabingwa hao wa England kwenye siku ya mwisho ya usajili. Wakati huo huo Javi Garcia anafanya vipimo vya afya kwa ajili ya kukamilisha uhamsiho wake kutoka Benfica kwenda City.




Nicklas Bendtner amehama Arsenal na kwenda kujiunga na Juventus ya Italia


Scott Sinclair amekamilisha uhamisho wake kutoka Swansea na kuhamia kwa mabingwa wa England Man City

 Andy Carroll amejiunga na West Ham kwa mkopo wa mwaka mzima



 Rafael Van Der Vaart amejiunga na Schalke akitokea Tottenham Hotspur

 Mchezaji wa kimataifa wa Brazil Douglas Maicon amesajiliwa kutoka Inter Milan kwenda Manchester City

 Pablo Hernandez amejiunga na Swansea City akitokea Valencia ya Spain







 Javi Garcia akiingia kwenye hosptali ya Bridge water kwa ajili ya kufanya vipimo vya afya baada ya klaby yake ya Benfica kukubaliana ada ya uhamisho na City - £16MILLION


 Charlie Adam amejiunga na Stoke City City akitokea Liverpool kwa ada ya £4MILLION

 Hatimaye Dimitar Berbatov amehamia rasmi Fulham kutoka Manchester United kwa ada ya £5million
 Ryan Babel mchezaji wa zamani wa Liverpool, amerudi timu yake ya utotoni Ajax akitokea Hoffenheim

 Golikipa Hugo Lloris wa Lyon amekamilisha vipimo vya afya na Tottenham na muda mchache na amesaini mkataba wa miaka minne kujiunga klabu hiyo kwa ada ya uhamisho wa £13million.

 Micheal Essien amethibitishwa kuwa ataungana tena na kocha Jose Mourinho, baada ya Chelsea kuthibitisha kwamba atajiunga na Real Madrid kwa mkopo wa mwaka mmoja.


Lassana Diara, mchezaji wa zamani wa Chelsea, Arsenal na Portsmouth, amejiunga na Anzhi Makhachkhala kutoka Real Madrid

Friday, August 31, 2012

Hawa ni wakina nani?


Cristiano Ronaldo anarudi Manchester. Kufanya nini?

Mshambuliaji wa kimataifa wa Ureno na Real Madrid Cristiano Ronaldo atarudi kwa mara nyingine kwenye jiji la Manchester baada ya kuondoka takribani miaka mitatu iliyopita.

Ronaldo ambaye alikaa kwenye jiji la Manchester kwa misimu mitano akiwa anaichezea klabu ya Manchester United kabla ya kuuzwa kwenda Real Madrid, atarudi kwenye jiji hilo kwa ajili ya kucheza mechi ya Champions league dhidi ya Mabingwa wa England Manchester City. Madrid wamepangwa kundi D, wakiwa  na City, Ajax, na Dortmund.

Haya ndio makundi yote ya Champions league msimu wa 2012-13




Group A

Team Pld W D L GF GA GD Pts
Portugal Porto 0 0 0 0 0 0 0 0
Ukraine Dynamo Kyiv 0 0 0 0 0 0 0 0
France Paris Saint-Germain 0 0 0 0 0 0 0 0
Croatia Dinamo Zagreb 0 0 0 0 0 0 0 0

Group B

Team Pld W D L GF GA GD Pts
England Arsenal 0 0 0 0 0 0 0 0
Germany Schalke 04 0 0 0 0 0 0 0 0
Greece Olympiacos 0 0 0 0 0 0 0 0
France Montpellier 0 0 0 0 0 0 0 0

Group C

Team Pld W D L GF GA GD Pts
Italy Milan 0 0 0 0 0 0 0 0
Russia Zenit St. Petersburg 0 0 0 0 0 0 0 0
Belgium Anderlecht 0 0 0 0 0 0 0 0
Spain Málaga 0 0 0 0 0 0 0 0

Group D

Team Pld W D L GF GA GD Pts
Spain Real Madrid 0 0 0 0 0 0 0 0
England Manchester City 0 0 0 0 0 0 0 0
Netherlands Ajax 0 0 0 0 0 0 0 0
Germany Borussia Dortmund 0 0 0 0 0 0 0 0

Group E

Team Pld W D L GF GA GD Pts
England Chelsea 0 0 0 0 0 0 0 0
Ukraine Shakhtar Donetsk 0 0 0 0 0 0 0 0
Italy Juventus 0 0 0 0 0 0 0 0
Denmark Nordsjælland 0 0 0 0 0 0 0 0

Group F

Team Pld W D L GF GA GD Pts
Germany Bayern Munich 0 0 0 0 0 0 0 0
Spain Valencia 0 0 0 0 0 0 0 0
France Lille 0 0 0 0 0 0 0 0
Belarus BATE Borisov 0 0 0 0 0 0 0 0

Group G

Team Pld W D L GF GA GD Pts
Spain Barcelona 0 0 0 0 0 0 0 0
Portugal Benfica 0 0 0 0 0 0 0 0
Russia Spartak Moscow 0 0 0 0 0 0 0 0
Scotland Celtic 0 0 0 0 0 0 0 0

Group H

Team Pld W D L GF GA GD Pts
England Manchester United 0 0 0 0 0 0 0 0
Portugal Braga 0 0 0 0 0 0 0 0
Turkey Galatasaray 0 0 0 0 0 0 0 0
Romania CFR Cluj 0 0 0 0 0 0 0 0