Saturday, September 21, 2013

DABI YA MANCHESTER: CITY v MAN UNITED, NI DABI YA 166!

UWANJA: Etihad SIKU: Jumapili Septemba 22 SAA 12 Jioni
 
DERBY_OF_MANCHESTER-2JUMAPILI, Jiji la Manchester litarindima kwa pande zake mbili, ile ya Kibuluu na ile Nyekundu, kukutana Uwanja wa Etihad kwa ajili ya Dabi ya 166 wakati Manchester City itakapowakaribisha Mahasimu wao Mabingwa Manchester United kwenye Mechi ya Ligi Kuu England huku Timu zote zikiwa na Mameneja wapya kwa Msimu huu.

Man City wanae Manuel Pellegrini na Man United wanae David Moyes.

Hali za Wachezaji

Manchester City wanaweza kuwachezesha Kiungo David Silva na Beki Micah Richards ambao wamepona maumivu yao lakini Beki Gael Clichy hatarajiwi kucheza kwa sababu hajapona vyema tatizo la Musuli za Pajani.

Manchester United wanaweza kumtumia Danny Welbeck ambae inasemekana amepata afueni tatizo la Goti lakini Phil Jones na Rafael bado hawajetengemaa maumivu yao.

++++++++++++++++++++++++++

REKODI:

MASHINDANO
MAN CITY-USHINDI
SARE
MAN UNITED-USHINDI
LIGI
40

49

59

FA CUP
3

0

6

LIGI CUP
3

1

2

NGAO YA
 JAMII
0

0

2

JUMLA

46


50


69



++++++++++++++++++++++++++

MATOKEO MECHI ZA MWISHONI:

27 Jan 2010 Manchester United 3 Manchester City 1 [Carling Cup]

17 Apr 2010 Manchester City 0 Manchester United 1 [BPL]

10 Nov 2010          Manchester City 0 Manchester United 0 [BPL]

12 Feb 2011 Manchester United 2 Manchester City 1 [BPL]

16 Apr 2011 Manchester City 1 Manchester United 0 [FA Cup]

07 Aug 2011           Manchester City 2 Manchester United 3 [NGAO YA JAMII]

23 Oct 2011 Manchester United 1 Manchester City 6 [BPL]

08 Jan 2012 Manchester City 2 Manchester United 3 [FA Cup]

30 Apr 2012 Manchester City 1 Manchester United 0 [BPL]

09 Dec 2012           Manchester City 2 Manchester United 3 [BPL]

08 Apr 2013 Manchester United 1 Manchester City 2 [BPL]

++++++++++++++++++++++++++

Tathmini

Timu zote hizi mbili, baada Mechi 4, zimefungana kwa Pointi zikiwa na Pointi 7 kila mmoja ikiwa ni Pointi 3 nyuma ya Vinara Liverpool.

Msimu huu, Man United walianza kwa kuifunga Swansea City Bao 4-1, Sare 0-0 na Chelsea, kufungwa 1-0 na Liverpool na kuichapa Crystal Palace Bao 2-0.

++++++++++++++++++++++++++

NINI WAMESEMA:

-PELLEGRINI: ‘Sijui nini kilitokea huko nyuma lakini kwa sasa najua tuna fikra zenye nguvu sawa na Man United au zaidi!’

-MOYES: ‘’Nina uzoefu wa Dabi nyingi-huko Glasgow na Merseyside. Ni muhimu sana kwa Mashabiki. Ni muhimu kwa Wachezaji lakini muhimu zaidi ni nini kitatokea mwishoni mwa Msimu na nani yuko kileleni!’

++++++++++++++++++++++++++

Man City walianza kwa kuifunga Newcastle 4-0, kufungwa 3-2 na Cardiff City, kuifunga Hull CityMAN_CITY_v_MAN_UNITED-TEAM_PITCH 2-0 na Sare ya 0-0 na Stoke City.

Nguzo muhimu kwa Man City ni Kiungo wao Yaya Toure ambae Msimu huu ameanza kwa kutawala vizuri katikati ikiwa pamoja na kufunga Bao pia likiwemo Bao kwenye Mechi ya Juzi ya UEFA CHAMPIONZ LIGI, UCL, ambayo walishinda Ugenini kwa kuichapa Viktoria Plzen Bao 3-0.

Nao Man United wamaimarisha Kiungo chao walipomsaini Marouane Fellaini Septemba 2 na bila shaka ataongeza nguvu kazi kuwakabili kina Yaya na Fernandinho.

Lakini, bila shaka, Man United nguzo zao kubwa ni Washambuliaji wao, Robin van Persie na Wayne Rooney huku Rooney akiwa juu kwa hivi sasa baada kung’ara mno kwenye Mechi ya UCL Jumanne iliyopita Man United walipoicharaza Bayer Leverkusen Bao 4-2 na Rooney kufunga Bao 2.

Hizo zilikuwa Bao zake za 199 na 200 kwa Man United na kumfanya awe wa 4 katika Listi ya Wafungaji Bora Klabuni hapo.

++++++++++++++++++++++++++

DONDOO MUHIMU:

-Rooney amefunga Bao 10 katika Dabi za Manchester sawa na Wafungaji Bora wa Dabi hii katika Historia, Francis Lee na Joe Hayes, ambao wote wanatoka Man City, na Jumapili akifunga yeye atatwaa Nambari Wani.

++++++++++++++++++++++++++

Kwa Rooney Uwanja wa Etihad humpa mafanikio kwani amefunga Bao 4 katika Mechi 3 za mwisho alizocheza na Man City.

Uso kwa Uso

-Msimu uliopita kwenye Ligi, Man United walishinda Etihad Bao 3-2 na Man City kushinda 2-1 Old Trafford.

-Katika Mechi 10 za mwisho za Ligi walizocheza kati yao, Man United wameshinda 6 na Man City 3.

-Katika Mechi 16 za Ligi Kuu ambazo Man United wamekwenda kucheza Nyumbani kwa Man City wameshinda 9, Man City 5 na Sare 2.

VIKOSI VINATARAJIWA:

MAN CITY [Mfumo: 4-2-3-1]: 

-Hart

- Zabaleta, Kompany, Nastasic, Kolarov

-Toure, Fernandinho

-Navas, Aguero, Nasri

-Dzeko

MAN UNITED [Mfumo: 4-4-2]:

-De Gea

-Smalling, Ferdinand, Vidic, Evra

-Valencia, Carrick, Fellaini, Kagawa

-Rooney, Van Persie

Refa: Howard Webb

++++++++++++++++++++++++++

LIGI KUU ENGLAND

RATIBA:

[Saa za Bongo]

Jumamosi 21 Septemba

14:45 Norwich City v Aston Villa

17:00 Liverpool v Southampton

17:00 Newcastle United v Hull City

17:00 West Bromwich Albion v Sunderland

17:00 West Ham United v Everton

19:30 Chelsea v Fulham

Jumapili 22 Septemba

15:30 Arsenal v Stoke City

15:30 Crystal Palace v Swansea City

18:00 Cardiff City v Tottenham Hotspur

18:00 Manchester City v Manchester United

++++++++++++++++++++++++++

MSIMAMO:
NA

TIMU

P

PTS


1
Liverpool
4
10

2
Arsenal
4
9

3
Tottenham
4
9

4
Man. City
4
7

5
Man. United
4
7

6
Chelsea
4
7

7
Stoke City
4
7

8
Newcastle
4
7

9
Everton
4
6

10
West Ham
4
5

11
Southampton
4
5

12
Cardiff
4
5

13
Swansea
4
4

14
Fulham
4
4

15
Norwich
4
4

16
Hull City
4
4

17
Aston Villa
4
3

18
Crystal Palace
4
3

19
WBA
4
2

20
Sunderland
4
1

UEFA YASIMAMISHA MGAO KLABU 6

NYINGINE 25 ZACHUNGUZWA!!
 
UEFA imetangaza kusimamisha Malipo ya Mgao wao wa Fedha za Zawadi kwa Klabu 6 zinazoshiriki Mashindano ya UEFA ya Msimu huu wa 2013/14.

Kusimamishwa huko kumeamriwa na Bodi ya Klabu ya Udhibiti Fedha, UEFA Club Financial Control Body (CFCB) ili uchunguzi ufanyike.

CFCB inaongozwa na Mwenyekiti Jean-Luc Dehaene ambae alikuwa Waziri Mkuu wa zamani wa Belgium.

++++++++++++++++++++++++++++

KLABU 6 ZILIZOSIMAMISHIWA MGAO:

-FC Astra Ploieşti (Roumania)

-FC Metalurh Donetsk (Ukraine)

-HNK Hajduk Split (Croatia)

-HŠK Zrinjski (Bosnia)

-Skonto FC (Latvia)

-Trabzonspor AŞ (Turkey).

++++++++++++++++++++++++++++

UEFA_LOGO-2013Ikiwa ni hatua ya kuzingatia Sheria mpya za UEFA zinazotaka Klabu zijiendeshe kwa Mapato yao wenyewe, Financial Fair Play Regulations (FFP), Klabu zote zinazoshiriki Mashindano ya UEFA Msimu huu zilitakiwa zipeleke Taarifa za Madeni yao ambayo hayajalipwa ya Kipindi kinachomalizika Juni 30.

Kufuatia Taarifa hizo, CFCB imeamua kusimamisha Mgao kwa Klabu hizo 6 ambazo hazijalipa Madeni yao yakiwemo yale ya Klabu nyingine, Wafanyakazi na Kodi za Nchi.

Kusimamishwa huko kutadumu hadi Madeni yakatapolipwa ama utakapotoka uamuzi mwingine wa CFCB.
Mbali ya Klabu hizo 6, Klabu nyingine 25 zimetakiwa kupeleka Taarifa zaidi kuhusu hali zao Kifedha.

Kwa mujibu wa Taarifa za UEFA, tangu Sheria za FFP zianze kutumika Madeni ambayo hayajalipwa na Klabu yamepungua kutoka Euro Milioni 57 ya hapo Juni 2011 na kufikia Euro Milioni 9 hapo Juni 2013.

Pia UEFA imeripoti kuwa Hasara kwa Klabu imepungua kwa Euro Milioni 600 baada ya kuwa na ongezeko la Hasara kwa Miaka 6.

MOURINHO KWA MATA: ‘BADILIKA AU BENCHI!’, MOYES KWA ROONEY: ‘BAKI MCHEZAJI MKUBWA!’

MOYES_v_MOURINHONDIO kwanza UEFA CHAMPIONZ LIGI, UCL, imeanza kwa Klabu kubwa huko England na Ligi Kuu England ndio inaanza kupamba moto lakini Klabu kubwa huko England, Mabingwa Manchester United, na Chelsea, zimepata matokeo tofauti na kuzua mijadala huku Mameneja wao, David Moyes na Jose Mourinho, wakijitokeza na kutoa nadharia zao. 
PATA ZAIDI:

MOURINHO KWA MATA: ‘BADILIKA AU BENCHI!’

Bosi wa Chelsea Jose Mourinho amemwambia Mchezaji wakeJUAN_MATAJuan Mata ni lazima abadilike ikiwa anataka namba Chelsea.
Mata, ambae amekuwa Mchezaji Bora Chelsea kwa Misimu miwili iliyopita, amekuwa hapati namba tangu Jose Mourinho aanze kazi hapo Chelsea mwanzoni mwa Msimu.

Msimu huu amecheza Mechi 3 tu-alitolewa baada ya Dakika 65 na Aston Villa, kuchezeshwa Dakika 57 na Everton na kucheza Dakika 23 Chelsea walipofungwa 2-1 na FC Basel kwenye UCL hivi Juzi.

Mourinho ameweka bayana kuwa Nambari 10 wake ni Oscar na Mata inabidi abadili uchezaji wake ili apate namba.

Mourinho amesema: “Kuna vitu siwezi kuongea na nyinyi. Lakini alicheza na Everton tangu mwanzo na hebu chunguzeni uchezaki wake. Nataka kumjenga Oscar kama Namba 10 wangu. Nataka Wachezaji wengine wawili, kutoka Winga, wakubali hilo na kujifunza vitu ambavyo hawakuwa tayari kujifunza toka mwanzo.  ”

Mourinho alitamka: “Mata alicheza na Basel, si sawa na Ba na Mikel waliokuja kuokoa jahazi, alikuwepo Timu ikiongoza 1-0 na alikuwa na kazi maalum. Ajifunze. Kitu kimoja ni kumchezesha yeye pamoja na Ramires na Oscar, wao kuwabana Wapinzani na Mata kucheza Namba 10 nyuma ya Straika ili asaidie kutoa mchango wa Magoli kwa pasi safi, awajibike kwa sababu ana kipaji.”

Aliongeza: “Kingine ni kubadilika na kufuata uchezaji wetu sasa. Wakati huu, Oscar ndie Namba 10 wangu, na ukiniambia kuwa Oscar sie Mchezaji Bora Chelsea tangu Msimu uanze, nitakupinga!”
Mourinho amekuwa akimchezesha Eden Hazard Winga kushoto, Oscar nyuma ya Straika na kulia, kwenye Mechi na Basel, alianza Willian.

Na Mourinho amesisitiza Oscar na Mata wanaweza kucheza Timu moja lakini anataka Mata, anaetumia Mguu wa kushoto, acheze Winga ya Kulia na pia awajibike kukaba Timu inapopoteza Mpira.

MOYES KWA ROONEY: ‘BAKI MCHEZAJI MKUBWA!’

ROONEY_N_MOYESDavid Moyes amempa changamoto Straika wake Wayne Rooney ahakikishe kuwa yeye ni Mchezaji mkubwa wa Mechi kubwa huku Jumapili wakitarajiwa kusafiri kwenda Etihad kucheza na Mahasimu wao Manchester City kwenye Dabi ya Jiji la Manchester.

Rooney alisakamwa na sakata la kutaka kuhama kufuatia kauli ya Meneja Mstaafu Sir Alex Ferguson Mwezi Mei kuwa Mchezaji huyo anataka kuhama na kisha kuundamwa na kuumia lakini, hivi sasa, kwa Mechi mbili alizoanza Rooney ameonyesha yuko moto na ameshahau sakata hilo lililoleta utata.

Jumamosi iliyopita Rooney alianza Mechi na Crystal Palace na kufunga Bao na Jumanne alicheza Mechi ya UCL na Bayer Leverkusen na kufunga Bao 2.

Hivi Juzi, katika nia ya kusawazisha mambo, Sir Alex Ferguson aliibuka na kuzungumza kwa mara ya kwanza na kumsifia sana Rooney.

Sasa Moyes, ambae ndio anakumbana na Dabi yake ya kwanza kama Meneja wa Man United, amesema anaamini sasa ni wakati muafaka kwa Rooney kuonyesha cheche zake kama mmoja wa Wachezaji Bora Duniani.

Moyes ametamka: “Nadhani mtazamo wa Rooney ni kuwa yeye ni Mchezaji mkubwa wa Mechi kubwa. Anataka kuonyesha hilo kwa kila Mtu. Na Watu wanakuja Mpirani kuona Wachezaji kama yeye wakionyesha tofauti na kubadili Gemu na tunategemea atafanya hivyo. Kitu muhimu ni kuwa abakishe fomu yake. Akiendelea kucheza kama hivi, Magoli yatakuja tu!”

Rooney amefunga Bao 10 katika Dabi za Manchester sawa na Wafungaji Bora, Francis Lee na Joe Hayes, ambao wote wanatoka Man City, na Jumapili akifunga yeye atatwaa Nambari Wani.

Pia, Moyes alisema kwa Sir Alex Ferguson kuibuka na kumsifia Rooney ni jambo jema litakalosaidia sana.
Amesema: “Ukisifiwa na Mtu kama Sir Alex basi kubali. Lakini tukumbuke ni Wayne mwenyewe aliejifikisha hapa. Yeye ndie amefanya kazi ngumu.”

Aliongeza: “Ni Mwaka mkubwa kwake..Rekodi nyingi anaweza kuzipata. Ana Mwaka mkubwa kuelekea Kombe la Dunia.”