Sunday, August 26, 2012

Milani wamtaka kwa mkopo, Real: KAKA ANAUZWA





Klabu ya AC Milan inajaribu kuishawishi Real Madrid iwape kiungo wao Kaka kwa mkopo kabla ya dirisha la usajili kufungwa ijumaa lakini mabingwa hao wa LaLiga wanatilia mkazo na kusema kaka siyo wa mkopo bali ni wa kuuzwa.

“Hali inaonyesha wazi kuwa Real wanataka kumuuza Kaka wakati sisi tunamtaka mkwa mkopo.” Gilliani aliiambia Sky Sport .

“Kama Real wakabadilisha mawazo nitafanya haraka kumchukua kwa mkopo”

Kocha wa Real Madrid,Jose Mourinho alimtema Kaka kwenye kikosi kilichocheza mechi ya alhamisi ya Super cup ikiwa ni mzunguko wa kwanza na Barcelona pale Nou Camp na mechi ya LaLiga na Getafeakisema kwamba mchezaji huyu aliyewahi kuwa mchezaji bora wa dunia kwa mwaka wa 2007 kuwa hayupo kwaenye mipango yake.

Mabingwa hao wa LaLiga wanakamilisha usajili wa kiungo Luca Modric akitokea Tottenham ambaye amefanya Kaka asiwe kwenye mipango ya Mreno huyo.
Kaka amekuwa akihusishwa na vyombo vya habari kuwa ataenda Paris St. German ya Ligue1 Ufaransa, klabu ambayoinanolewa na boss wake wa zamani pindi anakipiga katika klabu ya Milan Carlo Ancelotti.

No comments:

Post a Comment