Saturday, December 22, 2012

TAIFA STARS YAIPOPOA CHIPOLOPOLO 1-0!!

MABINGWA AFRIKA ZAMBIA HOI UWANJA wa TAIFA!!
NGASSA ni ‘KISIRANI’ BALAA!

MRISHO_NGASATimu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, leo imetoa burudani safi na zawadi safi ya Krismasi na Mwaka mpya kwa Watanzania kwa kuwalaza Mabingwa wa Afrika Zambia, maarufu kama Chipolopolo, kwa Bao 1-0 kwenye Mechi ya Kirafiki ya Kimataifa iliyochezwa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Bao la ushindi lilifungwa na Mrisho Ngassa katika Dakika ya 44 baada ya kupokea krosi safi kutoka kwa Mwinyi Kazimoto.

Kwa ujumla, Taifa Stars, wanaofundishwa na Kim Poulsen, walicheza vizuri sana na uwezo wa kuongeza Mabao mengine ulikuwepo.

Zambia, chini ya Kocha Bora Afrika Herve Renard, Kipindi cha Pili, waliongeza kasi na Mashambulizi lakini Stars walisimama imara na kusafisha hatari zote huku Kipa Juma Kaseja akiwa nguzo imara.

VIKOSI VILIVYOANZA:

TAIFA STARS: Juma Kaseja, Erasto Nyoni, Shomari Kapombe, Aggrey Morris, Kevin Yondan, Frank Domayo, Salum Abubakar, Mwinyi Kazimoto, Amri Kiemba, Mrisho Ngassa, Khamis Mcha

ZAMBIA: Danny Munyao, Chintu Kampamba, Hichani Himonde, Chisamba Lungu, James Chamanga, Moses Phiri, Christopher Katongo, Felix Katongo, Nathan Sinkala, Rodrick Kabwe, Isaac Chansa.

No comments:

Post a Comment