Sunday, August 26, 2012

Arsenal "Ngoma Ngumu" bila RVP

 
Stoke City na klabu ya Arsenal  wamebakia waiktafuta ushindi wao wa kwanza katika ligi kuu baada ya kutoka sare ya mabao bila ya kufungana. 
Matokea hayo yamezifanya klabu ya Stoke kushika nafasi ya 11 na ile ya Arsenal kushika nafasi ya 12 katika msimamo wa ligi kuu England baada ya timu zote kucheza mechi mbili.

Washika bunduki hao walipata nafasi nyingi sana lakini kutokuwepo kwa RVP ambaya amesajiliwa na klabu ya Manchester United, wakashindwakukwamisha mpira wavuni katika mechi yao ya piliambayo ya kwanza pia ilikuwa droo.
 "Pointi mbili katika mechi mbili za kwanza hazitoshi kabisa" Kiungo wa Arsenal, Mikel Arteta alikiambia kituo ca televisheni cha Sky Sports. "Tulihitaji pointi tatu lakini ilikuwa vigumu kwelikupata hizo pointi tatu." Aliongezea. "Tulikuwa na nafasi nzuri lakini hatukuzifanyia kazi kama ilivyotakiwa. Tulikuwa na nafasi nzuri ya kuchukua pointi tatu leo lakini tumepoteza mbili. Ni subira tu kabla ya Olivier Giroud na Lukas Podolski ambaoni wachezaji wapya kuzoea mfumo wa timu. Alimalizia Arteta.

Liverpool ambao wapo katika nafasiza chini kwenye msimamo wa ligi kuu England baada ya kichapo cha mabao 3-0 na West bromwich Albion wikiendi iliyopita, wanaikaribisha Manchester City  katika uwanja wa anifield baadae.
 

No comments:

Post a Comment