Monday, August 27, 2012

Barton kuihama QPR kwenda Marseille









Mtukutu Joey Barton alitumia akauntiyake ya twitter kumdhihaki kocha wa QPR Mark Hughes akimwambia kwamba anataka kuihama klabu hiyo na ke=wenda Olympique Marseille.

Barton 29 yupo katika kifungo cha mechi 12 baada ya kutolewa nje ya uwanja  kwa kufanya vurugu pale alipomkwatua Sergio Aguero na kwenda kupandishiana na Vicent Kompany.

Kiungo huyo ambaye ana’followers’ 1.68 millioni, alitoa hisia zake katika twiti 15 akisema, “ Moyowangu tayari upo katika uwanja wa Marseille.”

Barton ambaye alijiunga na QPR akitokea Newcastle na kocha aliyepita akimpa unahodha wa klabu hiyo.

“Sikuwahi hata siku moja kuongea maneno mabaya kwa mtu yoyote. Mimi ni mwanaume. Nataka kuondoka. Nmesema inatosha kwa hapa.” 

No comments:

Post a Comment