Monday, August 27, 2012

Eto’o akataa kurudi Cameroon








Samuel Eto’o amekataa nafasi ya kurudi kukipiga katika timu yake ya taifa ya Cameroon na kusema kwamba timu hiyobado ina utawala mbovu.

Mshambuliaji huyo mwenye miaka 31 aliitwa wiki iliyopita kwa ajili ya michuano ya African Cup of Nation round ya kwanza katiya Cameroon na Cape Verde Septemba 8, miezi nane baada ya kusimamishwa baada ya kuwaongoza wachezaji wenzake kufuatiwa na mgomo kwa sababu ya kutolipwa posho zao.

“Napenda kuwaambia kuwa nimeamua kutokuja kushiriki michuano hiyona timu yangu ya taifa.” Eto’o aliandika kwenye barua aliyoituma kwa shirikisho la mpira la Cameroon akiichapisha kwenye mtandao wake (www.samweletoo-officiel.com).

“Mazingira ya timu ya taifa bado yametawaliwa na utawala mbovu ambao haufai kwa mahitaji ya viwango vya hali ya juu kwenye michezo.” Aliongezea hivyo mshambuliajihuyo aliyewahi kuwa mchezaji bora wa Afrika mara nne na akiichezea timu yake ya taifa zaidi ya mara 100.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa klabu ya Inter Milan na Barcelona, kwa sasa anakipiga katika klabu tajiri kwenye ligi kuu ya Urusi  ya Anzi Makhachkala.

Mechi kati ya Cameroon na Cape Verde itaamua nafasi ya kushiriki fainali za AFCON 2013 huko kwa Madiba, Afrika kusini.

No comments:

Post a Comment