Saturday, December 29, 2012

WENGER AMKANA BA, NEYMAR BARCA BAADA 2014, ANCELOTTI na RONALDO!!

DEMBA_BARIPOTI zimebainisha kuwa Arsene Wenger ameua ile minong’ono kuwa wako njiani kumsajili Straika wa Newcastle, Demba Ba, huku Meneja wa Paris St Germain Carlo Ancelotti akisisitiza kuwa hamna nafasi ya wao kumchukua Cristiano Ronaldo na huko Brazil, Baba Mzazi wa Neymar, amedokeza kuwa Mwanawe atajiunga na Barcelona mara baada ya kumalizika Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2014 zitakazochezwa huko Brazil.

WENGER na BA
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amefuta ile dhana ya kuwa wana nia ya kumsajili Straika kutoka Senegal, Demba Ba, ambae hata Newcastle wenyewe wamenawa mikono kuwa huenda akauzwa.

Lakini Wenger amesema: “Nampenda Ba, lakini hatuwezi kumsaini!”
Demba Ba alijiunga na Newcastle akitokea West Ham Juni Mwaka 2011.

PSG na RONALDO
Kocha wa Paris St Germain Carlo Ancelotti amesisitiza Supastaa wa Real Madrid Cristiano Ronaldo hajiungi na na Timu yake.

Hivi karibuni kumekuwa na uvumi kuwa Ronaldo ataondoka Real na Klabu za Man United na PSG ndizo zinazotajwa kumchukua.

Ancelotti ametamka: “Hamna ukweli kuhusu Ronaldo kuja kwetu. Si tatizo la Pesa lakini je Klabu yake itakubali kuuzwa?”

Vile vile, Ancelotti aligusia kuwa pamoja na Lucas Moura kwenda PSG Mwezi Januari atakuwa na Wachezaji 30 Klabuni hapo.

NEYMAR na BARCA
Kwa mujibu wa Baba Mzazi wa Staa wa Brazil na Klabu ya Santos Neymar, Mchezaji huyo atajiunga na FC Barcelona mara baada ya Fainali za Kombe la Dunia zitakazochezwa Nchini Brazil Mwaka 2014.

Baba huyo amesema mipango hiyo ipo lakini bado haijakamilika na kufafanua: “Anataka kucheza Ulaya. Tumebadili kikomo cha Mkataba wake kutoka 2015 na kuwa 2014.

 Kwa sasa atabaki Brazil hadi Kombe la Dunia kwisha! Na kwa sasa ni bora kila Mtu akae kimya!”

No comments:

Post a Comment