Sunday, August 26, 2012

Madrid yafungwa, Messi aiokoa Barca




Real Madrid kutokuanza msimu vizuri imeendelea baada ya mabingwa hao kupokea kipigo cha mabao 2 – 1 kutoka kwa Getafe kwenye LaLiga jumapili na kuwaweka pointi 5 nyuma ya mahasimu waoBarcelona.
Vijana haowa Mourinho ambao walitoka sare ya mabao 1- 1 wikiendi iliyopita na Valencia, walionekana kutulia na kucheza soka safi mpaka pale GonzaloHiguain alipopachika bao mnamodakika ya 27.

Dakika ya 8 baada ya mapumziko y kipindi cha kwanza, Juan Valera aliunganisha mpira wavuni baada ya kupigwa kwa “free kick” safi sana.

Ikatoka kuwa chachu mpka kuwa mbaya zaidi pale “supersub” Adrian Colunga alivyotoa pande kwa Abdelaziz Barrada na kuupeleka juumpira uliomshinda goli kipa Iker Casillas kutokana na mpira ule kumzidi umbali wa kwenda juu.

Lionel Messi aliiokoa timu yake ya Barcelona kwa kuifungia  magoli mawili mnamo kipindi cha pili baada ya kupigwa goli moja lililodumu dakika 45 za kwanza ambapo Osassuna waliongoza.
Barca wana pointi sita baada ya mechimbilina wakiushikilia uskaniwa ligi hiyo ikiwa ni tofauti ya magoli na Rayo Vallecano ambao pia wana pointi sita baada ya kuwafunga 2 – 1 Real Betis jana jumamosi.

No comments:

Post a Comment