Thursday, December 27, 2012

ASILIMIA 82 YA MASHABIKI WA MADRID WANATAKA MOURINHO ATIMULIWE KAZI REAL MADRID !!

 
 Mashabiki wa Real Madrid wameamua. Wanataka Mourinho aondoke Bernabeu.

Kufuatia kupigwa benchi kwa Casillas katika mechi dhidi ya Malagamtandao wa gazeti maarufu nchini Hispania MARCA.com uliuliza "Je inabidi Real Madrid imtimue Mourinho?" na majibu ya takribani wasomaji 100,000 yalikuja yakisema ndio kwa asilimia  82.4%.

Kwa mujibu wa MARCA, mapenzi baina ya washabiki wa Los Blancos na Mourinho yamekwisha kabisa. Madrid wamekuwa na mfululizo wa matokeo mabaya katika kipindi cha hivi karibuni na kusababisha maneno mengi juu ya mustakabli wa kocha Jose Mourinho ndani ya klabu hiyo.

Real Madrid wapo nyuma kwa 16 dhidi ya viongozi wa La Liga Barcelona, na tayari Mourinho ameshasema kwamba ubingwa wa La liga msimu huu hawawezi kushinda tena, na inasemekana kwamba ikiwa atashindwa kuiongoza klabu hiyo kushinda ubingwa wa 10 wa mabingwa wa ulaya basi Mreno huyo atatemeshwa kibarua chake mwishoni mwa msimu.

No comments:

Post a Comment