Friday, May 31, 2013

GERMAN DFB POKAL: JUMAMOSI, BAYERN MUNICH v VfB STUTTGART

FAINALI: JUMAMOSI JUNI 1,  SAA 12 JIONI, OLYMPIASTADION, BERLIN

BAYERN YATAKA HISTORIA YA TREBO, BRAZIL YAWATIBUA!!

DANTE BAADA ya kutwaa Ubingwa wa Bundesliga na UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI, Bayern Munich wana nafasi ya kuweka historia hapo Jumamosi ya kuwa Klabu ya kwanza ya Kijerumani kutwaa ‘TREBO’ ikiwa wataifunga VfB Stuttgart kwenye Fainali ya German Cup, maarufu kama German DFB Pokal, lakini azma hiyo imeingia dosari baada ya Brazil kuzuia baadhi ya Wachezaji wao kuichezea Klabu yao.

Mzozo huu umemfanya Mwenyekiti wa Bayern Munich, Karl-Heinz Rummenigge, apandishe na kudai hilo halikubaliki baada ya Shirikisho la Soka la Brazil, CBF, kuwazuia Wachezaji wa Bayern Munich, Kiungo Gustavo na Sentahafu Dante, kutocheza Fainali hiyo na badala yake kutakiwa kuripoti Kambini Nchini Brazil Siku ya Alhamisi kuanza maandalizi ya Nchi hiyo kwa ajili ya Mashindano ya FIFA ya Kombe la Mabara yanayoanza kuchezwa Juni 15 Nchini Brazil.

Juni 2, Brazil watacheza Mechi ya Kirafiki na England Uwanja wa Maracana Jijini Rio De Janeiro.

Rummenigge amedai Wachezaji hao wa Brazil wametishwa kwamba hawatachukuliwa tena kuichezea Brazil wakichelewa kupiga ripoti Kambini.

Wakati Bayern wanadai huo ni ukatili, CBF, kupitia Mkurugenzi wao wa Ufundi, Carlos Alberto Parreira, amesema wao waliwapelekea DFB Barua yenye heshima ya kuelezea msimamo wao.

Hata hivyo Rummenigge amekiri wenye makosa ni wao wenyewe Germany, hasa Shirikisho la Soka, DFB, kwa kuipanga Fainali ya German DFB Pokal kuwa Juni 1, tarehe ambayo ipo kwenye Kalenda ya FIFA ya Mechi za Kimataifa.
 

No comments:

Post a Comment