Thursday, December 27, 2012

FERGIE KULIKWAA RUNGU LA FA? MANCINI AKIRI MATATIZO!!

REDKNAPP AMLAUMU REFA KWA KURUDISHWA MKIANI!!
BENITEZ ASEMA 1-0 NI MUHIMU KAMA 8-0!!

FERGIE_KAZINIMENEJA wa Manchester United, Sir Alex Ferguson, anasubiri nini kitamkuta endapo Refa Mike Dean atamtaja kwenye Ripoti yake ya Mechi ya jana ambayo Man United waliifunga Newcastle Bao 4-3 baada ya kumkabili Refa huyo na Wasaidizi wake kabla Kipindi cha Pili kuanza akilalamikia Bao la pili la Newcastle.
Ferguson alikuwa amekasirishwa na Refa Mike Dean kufuta Ofsaidi iliyotolewa ishara na Msaidizi wake Jake Collin na kuamua ni Bao kwa vile Jonny Evans alijifunga mwenyewe.

Wakati Kipindi cha Pili kinataka kuanza, Ferguson alimvaa Refa Mike Dean na kumlalamikia kisha akamvaa Refa wa Akiba Neil Swarbrick na pia Refa Msaidizi Jake Collin.

Ikiwa tukio litatajwa kwenye Ripoti ya Mechi ya Refa Mike Dean basi huenda Sir Alex Ferguson akaadhibiwa FA lakini kwa vile Refa Dean hakumchukulia hatua yeyote Ferguson huenda akakwepa adhabu.

Akielezea tukio hilo Ferguson alisema: “Refa alimfanya Mshika Kibendera abadilishe uamuzi wake wa Ofsaidi. Alisema ni Goli la kujifunga mwenyewe lakini ukilirudia Goli lile, yule Mchezaji wa Newcastle alikuwa Ofsaidi na tena alimvuta mkono Evans! Sasa hilo kama si kuingilia uchezaji ni nini? Ni uamuzi mbovu!”

ROBERTO MANCINI AKIRI MATATIZO MANCHESTER CITY!!

Roberto Mancini amekiri kuwa ana matatizo makubwa mara baada ya jana kuchapwa 1-0 na Sunderland.
Mancini amesema: “Tatizo kubwa Mastraika hawafungi nafasi wanazopata!”
Sasa ni mara ya 3 mfululizo kwa Man City kufungwa Stadium of Light na Sunderland ambao jana Bao lao pekee lilifungwa na Winga wa zamani wa Man City, Adam Johnson.
Msimu huu, Man City wamefunga Bao 34 katika Mechi 19 za Ligi Kuu England ikiwa ni Magoli 14 nyuma ya vinara Man United.
Lakini, ingawa Man City sasa wako Pointi 7 nyuma ya Man United, Roberto Mancini amesema wao bado wana nafasi ya kutetea Taji lao.
Ametamka: “Man United wanafunga Bao nyingi kupita sisi lakini pia wanafungwa Bao nyingi kupita sisi! Msimu ni mrefu na ni juu yetu kubadilika!”

HARRY REDKNAPP CRITICISES REFEREE AFTER QPR'S LOSS TO WEST BROM
Bosi wa Queens Park Rangers Harry Redknapp amekasirishwa na maamuzi ya Refa Chris Foy ambayo amedai ni ‘Skandali!’ wakati jana walipofungwa 2-1 na West Brom na kuwatupa mkiani mwa Ligi Kuu England.
Refa Chris Foy alilikubali Goli la kujifunga mwenyewe Kipa Robert Green ambae alionekana akibanwa waziwazi na Mchezaji wa WBA, Marc-Antoine Fortune, na pia aliwayima Penati ya wazi mwishoni baada ya Beki Liam Ridgewell kuunawa mpira.
Redknapp amewaka: "Ile ni Faulo ya wazi kwa Kipa wetu na ile ni Penati ya wazi! Hii ni kashfa!”

BENITEZ ASEMA 1-0 NI MUHIMU KAMA 8-0!!
Bosi wa Chelsea Rafael Benitez anaamini ushindi wa Bao 1-0 dhidi ya Norwich hapo jana ni muhimu kama kile kipondo cha 8-0 walichowashushia Aston Villa Siku 3 zilizopita.
Ingawa Wadau wengi wa Klabu hiyo watahisi kimchezo ushindi wa 1-0 ni tofauti na ule wa 8-0, Benitez ametetea matokeo hayo kwa kusema: “Ni muhimu kuiona Timu ikicheza kwa bidii na kujilinda kisawasawa! Muhimu ni kuwa hatukufungwa Bao.”
Chelsea sasa wako nafasi ya 3 wakiwa Pointi 4 tu nyuma ya Man City na Mechi moja mkononi.
+++++++++++++++++++++++

MECHI ZIJAZO:
Jumamosi 29 Desemba 2012 

[SAA 9 Dak 45 Mchana]
Sunderland v Tottenham

[SAA 12 Jioni]
Aston Villa v Wigan
Fulham v Swansea
Man United v West Brom
Norwich v Man City
Reading v West Ham
Stoke v Southampton

[SAA 2 na Nusu Usiku]
Arsenal v Newcastle

Jumapili 30 Desemba 2012

[SAA 10 na Nusu Jioni] 
Everton v Chelsea

[SAA 1 Usiku]
QPR v Liverpool

Jumanne 1 Januari 2013 

SAA 9 Dak 45 Mchana]
West Brom v Fulham

[SAA 12 Jioni]
Man City v Stoke
Swansea v Aston Villa
Tottenham v Reading
West Ham v Norwich
Wigan v Man United

[SAA 2 na Nusu Usiku]
Southampton v Arsenal

Jumatano 2 Januari 2013 

[SAA 4 Dak 45 Usiku]
Chelsea v QPR
Liverpool v Sunderland

[SAA 5 Usiku]
Newcastle v Everton

No comments:

Post a Comment