2012 - umeendelea kuwa
mwaka mzuri kwa Zlatan Ibrahimovic, baada ya kupata mafanikio ya
uwanjani na kiuchumi sasa jina lake limeongezwa katika kamusi ya
kisweden na taasisi inayoshughulikia lugha nchini Sweden - Neno
'Zlatanera' lenye maana ya Zlatan au 'kutawala' limeongezwa katika
kamusi rasmi ya Sweden.
Hii imekuja kama kumtunuku mchezaji huyo
ambaye amekuwa akiletea sifa nchi hiyo ndani na nje ya nchi hiyo kwa
miaka takribani 10 sasa.
Neno 'Zlatanera' limetokana na neno la
kifaransa 'zlataner' lenye maana ya kutawala, hivyo wasweden
wakalinyambua na kuongeza herufi 'a' katika 'zlataner'.
No comments:
Post a Comment