Friday, December 28, 2012

GOODISON PARK KUMKARIBISHA BENITEZ KWA ‘CHUKI!’

>>JUMAPILI: EVERTON v CHELSEA!!!

>>MSIMU HUU, EVERTON HAWAJAFUNGWA NYUMBANI!!

>>CHELSEA WANAPIGWA GOODISON PARK KWA MISIMU MITATU SASA!

 BENITEZ-CHELSEARafael Benítez anajua fika kuwa Jumapili atapokelewa Uwanjani Goodison Park kwa ‘chuki’ kubwa toka kwa Mashabiki wa Everton wakati Timu yake Chelsea itakapotua hapo kucheza Mechi ya Ligi Kuu England ya ‘Funga Mwaka 2012’ kwa vile Mashabiki hao wanakumbuka kebehi ya Meneja huyo kwa kuibatiza Everton ni ‘Klabu Ndogo’ wakati akiwa Meneja wa Mahasimu wao wakubwa Liverpool.

Mwaka 2007 Benítez aliibatiza Everton ‘Klabu Ndogo’ na hilo liliwachukiza sana Mashabiki wa Everton wakati huo na hadi leo hawajaisahau kauli hiyo.
Alipokumbushwa na Mwanahabari, Benitez alitania: “Una kumbukumbu nzuri. Lakini sasa wanafanya vizuri bila kuwa na uwezo mkubwa kama Timu nyingine lakini ni wapinzani wagumu! Wako juu, wanastahili sifa!”
+++++++++++++++++++++++

MSIMAMO-Timu za Juu:
=Tofauti ya Magoli inatajwa kwa Timu zilizofungana Pointi

1 Man United Mechi 19 Pointi 46

2 Man City Mechi 19 Pointi 39

3 Chelsea Mechi 18 Pointi 35

4 Tottenham Mechi 19 Pointi 33 [Tofauti ya Magoli 9]

5 Everton Mechi 19 Pointi 33 [Tofauti ya Magoli 9]

6 WBA Mechi 19 Pointi 33 [Tofauti ya Magoli 5]

7 Arsenal Mechi 18 Pointi 30

8 Stoke Mechi 19 Pointi 28

9 Swansea Mechi 19 Pointi 25 [Tofauti ya Magoli 4]

10 Liverpool Mechi 18 Pointi 25 [Tofauti ya Magoli 2]
+++++++++++++++++++++++

Everton wapo Pointi mbili tu nyuma ya Timu ya 3 Chelsea na wameonyesha ushindani mkubwa Msimu huu wakiwa wamepoteza Mechi 2 tu za Ligi na ni moja ya Klabu mbili tu ambazo hazijafungwa nyumbani Msimu huu, nyingine ikiwa ni Stoke City.

Mbali ya changamoto ya Benitez kutua Goodison Park huku akiwa anachukiwa Chelsea, kwa Miaka ya hivi karibuni, wana Rekodi mbovu hapo na wamefungwa kwa Misimu mitatu Uwanjani humo.

Benitez, licha ya yeye kushinda Uwanjani Goodison Park mara 3 katika Mechi zake za mwisho hapo akiwa na Liverpool, amekiri: “Everton ni Timu nzuri na itakuwa Mechi ngumu kwetu. Ni Uwanjani mgumu Goodison Park!”
+++++++++++++++++++++++

RATIBA:
Jumamosi 29 Desemba 2012 

[SAA 9 Dak 45 Mchana]
Sunderland v Tottenham

[SAA 12 Jioni]
Aston Villa v Wigan
Fulham v Swansea
Man United v West Brom
Norwich v Man City
Reading v West Ham
Stoke v Southampton

[SAA 2 na Nusu Usiku]
Arsenal v Newcastle

Jumapili 30 Desemba 2012
[SAA 10 na Nusu Jioni]
Everton v Chelsea

[SAA 1 Usiku]
QPR v Liverpool

Jumanne 1 Januari 2013
SAA 9 Dak 45 Mchana]
West Brom v Fulham

[SAA 12 Jioni]
Man City v Stoke
Swansea v Aston Villa
Tottenham v Reading
West Ham v Norwich
Wigan v Man United

[SAA 2 na Nusu Usiku]
Southampton v Arsenal

Jumatano 2 Januari 2013
[SAA 4 Dak 45 Usiku]
Chelsea v QPR
Liverpool v Sunderland

[SAA 5 Usiku]
Newcastle v Everton

No comments:

Post a Comment