Sunday, December 30, 2012

LEO FUNGA MWAKA EVERTON v CHELSEA, QPR v LIVERPOOL!!

BPL_LOGO+++++++++++++++++++++++
RATIBA:
Jumapili 30 Desemba 2012 

[SAA 10 na Nusu Jioni]
Everton v Chelsea

[SAA 1 Usiku]
QPR v Liverpool
+++++++++++++++++++++++

LEO zipo Mechi mbili za Ligi Kuu England ambazo ndizo za mwisho kabisa kwa Mwaka 2012 na zifuatazo ni Dondoo kuhusu Mechi hizo:

EVERTON v CHELSEA
Uwanja: Goodison Park
Hali za Wachezaji:
Everton watacheza Mechi hii bila Marouane Fellaini ambae atakuwa akimalizia Kifungo chake cha Mechi 3 na pia itawakosa majeruhi Tony Hibbert na Kevin Mirallas.

Chelsea wataendelea kumkosa Nahodha wao John Terry ambae ni majeruhi lakini Kiungo Ramires atarudi dimbani baada kupona nyonga iliyomfanya akose Mechi ya Boxing Dei walipoifunga Norwich City.

Uso kwa Uso:
++Everton hawajafungwa na Chelsea Uwanjani Goodison Park katika Mechi 4 zilizopita kwa kushinda 3 na sare 1.

++Chelsea wameshinda Mechi moja tu kati ya 8 walizocheza mwishoni na Everton na hiyo ilikuwa ni ushindi wa Bao 3-1 Uwanjani Stamford Bridge Msimu uliopita.
+++++++++++++++++++++++

MSIMAMO:
=Tofauti ya Magoli inatajwa kwa Timu zilizofungana Pointi
1 Man United Mechi 20 Pointi 49
2 Man City Mechi 20 Pointi 42
3 Tottenham Mechi 20 Pointi 36
4 Chelsea Mechi 18 Pointi 35
5 Arsenal Mechi 19 Pointi 33 [Tofauti ya Magoli 18]
6 Everton Mechi 19 Pointi 33 [Tofauti ya Magoli 9]
7 WBA Mechi 20 Pointi 33 [Tofauti ya Magoli 3]
8 Stoke Mechi 20 Pointi 29
9 Swansea Mechi 20 Pointi 28
10 Liverpool Mechi 19 Pointi 25 [Tofauti ya Magoli 2]
11 Norwich Mechi 20 Pointi 25 [Tofauti ya Magoli -9]
12 West Ham Mechi 19 Pointi 23
13 Sunderland Mechi 20 Pointi 22
14 Fulham Mechi 20 Pointi 21
15 Newcastle Mechi 20 Pointi 20
16 Wigan Mechi 20 Pointi 18 [Tofauti ya Magoli -13]
17 Aston Villa Mechi 20 Pointi 18 [Tofauti ya Magoli -24]
18 Southampton Mechi 19 Pointi 17
19 Reading Mechi 20 Pointi 13
20 Mechi 20 Pointi 10
+++++++++++++++++++++++

QPR v LIVERPOOL
Uwanja: Loftus Road
Hali za Wachezaji:
Beki wa QPR Ryan Nelsen yupo kwenye hati hati ya kucheza Mechi hii baada ya kuugua na Wachezaji wengine ambao uchezaji wao upo kwenye wasiwasi kutokana na maumivu ni Kipa Julio Cesar, Beki Nedum Onuoha na Kiungo Park Ji-sung.

Fowadi wa Liverpool Luis Suarez anatarajiwa kucheza licha ya kuwa na maumivu ya enka huku Raheem Sterling na Joe Allen wakitarajiwa kuanza Mechi hii baada ya kuanzia Benchi katika Mechi mbili zilizopita.

Uso kwa Uso:
++Liverpool wameifunga QPR Mechi 3 kati ya 4 za Ligi walizocheza.
+++++++++++++++++++++++

RATIBA MECHI ZIJAZO:
 
Jumanne 1 Januari 2013 

SAA 9 Dak 45 Mchana] 
West Brom v Fulham

[SAA 12 Jioni]
Man City v Stoke
Swansea v Aston Villa
Tottenham v Reading
West Ham v Norwich
Wigan v Man United

[SAA 2 na Nusu Usiku]
Southampton v Arsenal

Jumatano 2 Januari 2013 

[SAA 4 Dak 45 Usiku]
Chelsea v QPR
Liverpool v Sunderland

[SAA 5 Usiku]
Newcastle v Everton

No comments:

Post a Comment