Saturday, December 22, 2012

MKE WA SNEIJDER ASEMA "TUNAONDOKA MILAN MWEZI JANUARY"

Mke wa Wesley Sneijder amesema kwamba mumewe ataondoka Inter wakati dirisha la usajili la mwezi January.

"Tunakaribia kuondoka Milan," Yolanthe Cabau aliviambia vyombo vya habari vya Uholanzi. "Kila kitakuwa kimewekwa vizuri katika siku za mwanzo za mwezi January.

"Tutakapohamia? Tunaangalia mahala pazuri kwa ajili ya familia yetu. Kwa sasa hivi sijali sana kuhsu kazi yangu."

Sneijder amekuwa kwenye kutokuelewana na Inter katika siku za hivi karibuni baada ya kukataa ombi lao kwa mchezaji apunguze kiasi cha €2m kutoka kwenye mshahara wake.

Hajaichezea timu hiyo ya Serie A tangu alipocheza dhidi Chievo, kwanza kwa sababu ya majeruhi na baadae kwa sababu za kiufundi za boss Andrea Stramaccioni.

Sneijder aliruhusiwa kuanza mapumziko yake ya Christmas mapema wiki hii pamoja na kwamba Inter bado wana mechi mbili  za kucheza.

No comments:

Post a Comment