Monday, December 24, 2012

MOURINHO juu ya KUTI KAVU REAL!!

KUTEMWA NAHODHA & KIPA NAMBARI WANI SPAIN, CASILLAS, KWAZUA ‘TIFU!’
 
WAMEMALIZA MWAKA wakiwa nafasi ya 3 kwenye La Liga, Pointi 16 nyuma ya Vinara Barcelona na Pointi 7 nyuma ya Timu ya Pili Atletico Madrid, Mabingwa wa Spain Real Madrid, chini ya Meneja makeke Jose Mourinho, wapo kwenye ‘tifu’ kubwa na limekolezwa na uamuzi wa kutomchezesha Kipa Nambari Wani wa Spain, Iker Casillas, ambae pia ndie Nahodha wao, juzi walipoaga Mwaka kwa kuchapwa 3-2 na Malaga na kukaribia kufuta ndoto zao za kutetea Ubingwa wao.
+++++++++++++++++++++++
MSIMAMO-Timu za Juu:
[Kila Timu imecheza Mechi 17]
1 Barcelona Pointi 49
2 Atletico Madrid 40
3 Real Madrid 33
4 Malaga 31
5 Real Betis 28
6 Levante 27
7 Real Sociedad 25
+++++++++++++++++++++++
IKER_CASILLASKwa sasa Soka la Spain liko Vakesheni hadi Januari 6 Mwakani na, kwa kila hali, inaonekana Real Madrid wameshaupoteza Ubingwa wao kwa Mahasimu wao Barcelona ambao wapo juu baada kutofungwa katika Mechi 17 za La Liga, na kilichobaki kwa Real ni kupindua kipigo cha 2-1 toka kwa Celta Vigo walichopewa kwenye Mechi ya Kwanza ya Copa del Rey wakirudiana Uwanja wao wa nyumbani Santiago Bernabeu.
Wakishindwa kufuzu kwenye Mechi hiyo na Celta Vigo, Real Madrid watabakiwa na kinyang’anyiro kimoja tu cha kuwania Taji Msimu huu na nacho ni kwenye UEFA CHAMPIONZ LIGI ambako kikwazo chao ni kuitoa Manchester United kwenye Raundi ya Mtoano ya Timu 16 hapo Februari 13 watakapocheza Santiago Bernabeu na kurudiana Machi 5 Uwanjani Old Trafford.
Hata hivyo, kwa sasa Jose Mourinho anakabiliwa na wakati mgumu kutokana na mwendo wao mbovu huku kukiwa na minong’ono kuwa ndani ya Klabu kuna mgawanyiko wa Wachezaji na yeye akihusishwa kuwa na bifu na baadhi yao lakini pia uamuzi wake wa kumpiga Benchi Kipa Nambari Wani wa Spain, Iker Casillas, kwenye Mechi na Malaga, Kipa ambae kwa Miaka 10 sasa amekuwa ndie yupo kila Mechi, kumezua mtafaruku mkubwa.
Kwenye Mechi hiyo na Malaga waliyofungwa 3-2, Mourinho alimpanga Kipa Nambari mbili Antonio Adan huku akitetea uamuzi huo kwa kudai Kipa Adan amekuwa kwenye Fomu nzuri kupita Casillas.
Mwenyewe Mourinho amepangua dhana zote kuwa hali si njema kwa kutamka: “Nikihisi mambo si shwari mie ni mkweli na siwezi kuendelea! Lakini Wachezaji bado wana ari, walicheza vizuri lakini tulikuwa hatuna bahati!”
Lakini Naibu Nahodha wa Real, Beki Sergio Ramos, amestushwa kwa kutemwa Casillas na alisema: “Si kawaida kumwona yuko Benchi lakini sisi hatuna la kusema, ni uamuzi wa Kocha!”
Hali hii ya sasa ni kitu kipya kabisa kwa Real Madrid ambao wanasifika kwa kutimua Makocha kwa sababu ndogo tu kupita ilivyo sasa lakini kitu kitakachomnusuru Jose Mourinho ni kuibwaga Celta Vigo kwenye Copa del Rey, kujiimarisha kwenye La Liga na kuitupa nje Manchester United kwenye UEFA CHAMPIONZ LIGI, kinyume cha hapo shoka litamkuta.

No comments:

Post a Comment