Monday, December 24, 2012

Harry Redknapp: 'Wachezaji wengi QPR wanalipwa Fedha nyingi bure! '

AMTWANGA FAINI BOSINGWA £130,000!!
 
Bosi wa Queens Park Rangers Harry Redknapp ameponda msimamo wa Klabu hiyo wa kununua Wachezaji wanaolipwa Mishahara minono kuliko uwezo wao na kauli hiyo imekuja mara tu baada ya kupokea kipigo chake cha kwanza Klabuni hapo baada ya kutoka sare 3 na kushinda Mechi moja na kuwaacha wakamate nafasi ya 19.
+++++++++++++++++++++++
MSIMAMO-Timu za chini:
=Tofauti ya Magoli inatajwa kwa Timu zilizofungana Pointi
15 Sunderland Mechi 18 Pointi 19
16 Aston Villa Mechi 17 Pointi 18
17 Southampton 15 [Tofauti ya Magoli -10]
===============
18 Wigan Mechi 18 Pointi 15 [Tofauti ya Magoli -15]
19 QPR Mechi 18 Pointi 10
20 Reading Mechi 18 Pointi 9
+++++++++++++++++++++++
HARRY_REDKNAPP12Redknapp ametamka: “Wapo Wachezaji wengi Klabuni wanalipwa Fedha nyingi kupita uwezo wao na nini wanaipa Klabu!”
Aliongeza kuwa hataki kuwaona Wamiliki wa QPR waliwe Pesa zao bure na alishtuka alipompiga Faini Mchezaji mmoja na kugundua Mchezaji huyo analipwa Fedha za juu kuliko hata Wachezaji wa Tottenham ambako alikuwa akifanya kazi kable.
Kitu kilichomshangaza sana ni kuona Uwanja wa QPR unachukua Watu 18,000 tu wakati Newcastle wana Uwanja wa Watu 52,000 lakini huko hawafikii Mishahara ya Wachezaji wa QPR.
Harry Redknapp amechukua wadhifa wa Umeneja hapo QPR baada ya kufukuzwa Mark Hughes ambae alisajili Wachezaji wengi lakini Timu haikupata ushindi hata mmoja hadi Redknapp alipotua.
+++++++++++++++++++++++
WACHEZAJI WALIOSAJILIWA na Meneja Mark Hughes:
-Nedum Onuoha
-Djibril Cisse
-Bobby Zamora
-Federico Macheda (Mkopo)
-Taye Taiwo (Mkopo)
-Samba Diakite
-Ryan Nelsen
-Andy Johnson
-Robert Green
-Park Ji-Sung
-Junior Hoilett
-Jose Bosingwa
-Julio Cesar
-Esteban Granero
-Sam Magri
-Stephane Mbia
+++++++++++++++++++++++
Mchezaji aliepigwa Faini na Redknapp ni Jose Bosingwa ambae amepigwa Faini ya Mshahara wa Wiki mbili baada kukataa kukaa Benchi katika Mechi ambayo QPR walipata ushindi wao wa kwanza walipoifunga Fulham Bao 2-1.
Bosingwa, ambae alikuwa Chelsea Msimu uliopita, amecheza Mechi 12 za Ligi za QPR na sasa anaelekea kutemwa na Klabu hiyo.
Redknapp ameleza: “Hakutaka kukaa Benchi, alitaka acheze na akaenda nyumbani bila kuaga! Amepigwa Faini £130,000! Na ataona nini kipo Januari!”
Redknapp amedokeza kuwa Januari atatafuna kuimarisha Kikosi na pia kuuza Wachezaji.

No comments:

Post a Comment