Tuesday, January 1, 2013

MANCINI: “RVP ndie anafanya Man United iwe tofauti na City!”

RVP_in_RED2Bosi wa Manchester City Roberto Mancini anaamini Straika wa Manchester United Robin van Persie ndie anaeleta tofauti kati ya Timu hizo mbili ambazo zinafukuzana kwenye Ligi Kuu England huku Man United wakiwa kileleni Pointi 7 mbele ya Man City ambao ni Mabingwa watetezi.

Mancini amesema: "Tulimtaka Van Persie kwa sababu tulijua ni Mchezaji muhimu! Yuko tofauti kabisa na Mastraika wengine! Van Persie ni muhimu kwa United na huyu ndie alieleta tofauti kati ya United na sisi hivi sasa!”

Mancini alibainisha kuwa walikuwa karibu kidogo kumsaini Robin van Persie lakini hilo halikutokea.

Hivi karibuni Mancini amekuwa akilia na Mastraika wake Sergio Aguero, Carlos Tevez, Edin Dzeko na Mario Balotelli kwa ubutu wa kufunga.

Amesema: “Msimu uliopita tulifunga Bao nyingi kupita Timu nyingine kwenye Ligi na tungempata Van Persie tungecheza Mfumo wa kutumia Mastraika watatu.”

Kwa sasa, Robin van Persie ndie anaongoza kwa ufungaji Bao nyingi kwenye Ligi Kuu England.

No comments:

Post a Comment