Source http://www.youngafricans.co.tz/
Africans Sports Club imeanza mazoezi leo
asubuhi katika viwanja vya Fame Footballl vilivyopo pemebni kidogo mwa
hoteli ya Fame Residence Lara & Spa iliyopo kusini mwa mji wa
Antalya ambapo imeweka kambi ya mafunzo ya wiki mbili.
Kocha Brandts akisaidiwa na kocha
msaidizi Fred Felix Minziro na kocha wa makipa Razaki Siwa waliongoza
mazoezi hayo yaliyoanza majira ya saa 4 kamili asubuhi kwa saa za Afrika
Mashariki na awamu ya pili ilianza majira ya saa 10 kamili jioni kwa
saa za Afrika Mashariki.
Ratiba ya mazoezi ni mara mbili kwa siku
asubuhi na jioni, ambapo timu inapata huduma zote za kambi katika
Hoteli ya Fame Residence Lara & Spa kuanzia chakula, malazi, mazoezi
ya viungo (Gym) ufukwe kwa ajili ya mazoezi ya stamina na kujenga
mwili.
Mji wa Antalya ni maarufu katika medani
ya soka kwani kwa ripoti tuliyopewa timu zaidi ya 200 zimeshafika katika
mji huu kipindi cha majira ya baridi kuja kuweka kambi zikitokea katika
nchi tofauti duniani.
Wenyeji wa Young Africans Team Travel
wameandaa sherehe ya kuukaribisha mwaka mpya ambapo wachezaji na
viongozi pamoja wenyeji wa mji huu watasherehekea pamoja.
No comments:
Post a Comment