Wakati Manchester United ikimtangaza
David Moyes kuwa mrithi wa Sir Alex Ferguson, hatma ya mchezaji Wayne
Rooney ndani ya Old Trafford imekuwa bado ya utata na kupelekea
mashabiki wa klabu hiyo kuwa katika hali ya wasiwasi.
Taarifa mbalimbali zimekuwa zikisema
mshambuliaji huyo amepeleka maombi ya kuondoka United kwa mara ya pili
ndani ya miaka 3, akisema anahitaji changamoto mpya sehemu nyingine,
huku vilabu vya Chelsea, PSG na Bayern Munich vikiwa tayari kutuma ofa
kwa ajili ya kumsaini Muingereza huyo.
Kutokana na sintofahamu hiyo kuhusu
hatma ya Wayne Rooney ambaye sasa amebadilisha biography yake kwenye
mtandao wa Twitter kutoka kuwa "mchezaji wa Manchester United mpaka kuwa
NikeUK athlete" - mashabiki wa klabu wamekuwa wakimtumia tweets za
vitisho na matusi kuhusu kutaka kuondoka Manchester United wakati huu
timu ikiwa kwenye huzuni kubwa kwa kustaafu kwa Fergie.
Kama vile haitoshi baaada ya Wayne
Rooney kukaa kimya bila kuwajibu chochote mashabiki ho kwenye Twitter
wakamfuata mkewe Coleen Rooney na kuanza kumuuliza kama ni kweli
wanataka kuondoka Manchester?
Mwanzoni Coleen alikaa kimya lakini
baadae akashindwa kuvumilia na kuwatumia tweet moja mashabiki na
kuwaambia kwamba "Mume wangu ana akaunti ya Twitter..... @WayneRooney
muulizeni yeye sio mimi".
No comments:
Post a Comment