Tuesday, August 28, 2012

Ferguson awakataza wachezaji chini ya umri wa miaka 23 kuendesha magari ya kifahari!

Manager wa Manchester United Sir Alex Ferguson amewakataza wachezaji wenye umri wa klabu hiyo kuendesha magari ya kifahari kutoka kwa mdhamini wao mpya Chevrolet.

United hivi karibuni walisaini mkataba wa mamilioni ya paundi na kampuni hiyo kubwa ya kutengeneza magari kutoka Marekani, na watakuwa wadhamini wao rasmi wa jezi kuanzia msimu wa 2014-15.

Kama kuonyesha ishara ya urafiki mzuri mpya wa kibiashara baina yao na United, Chevrolet kwa haraka walitoa ofa kwa wachezaji wa kikosi cha kwanza cha United kuchagua magari ya kifahari wayatakayo na wangepewa bure na vijana wengi wakaagiza magari aina ya Iconic Corvettes.
Ingawa inasemekana Ferguson akaingilia kati na kuweka sheria kwamba vijana wa chini ya miaka 23  - haijalishi wana ukubwa na umuhimu gani kwenye timu - hawatoruhusiwa kutoa oda ya aina hiyo ya gari la kifahari.
 Kwa maana hiyo wachezaji kama Danny Welbeck, 21, Phili Jones 20, Chris Smalling 22, na Rafael 22, na wengine kibao hawatoruhusiwa kuendesha magari ya kifahari ya ofa kutoka Chevrolet aambayo yatakuwa hayajapata baraka kutoka kwa Mzee Fergie.

Uamuzi huu wa Ferguson unalenga kuhakikisha vijana wake wadogo hawavimbi vichwa na kujisahau isivyostahili. Pia hii sio mara ya kwanza kwa Fergie kufanya kitendo kama hiki, miaka miwili iliyopita alitoa katazo kwa vijana wa timu ya watoto kutovaa viatu vya bei mbaya hasa vya rangi.

No comments:

Post a Comment