Thursday, August 30, 2012

Jose Mourinho aendelea kuvunja rekodi duniani - awa kocha wa kwanza kuchukua makombe ya ligi na Supercup kwenye nchi nne za juu kisoka.

 Kocha Jose Mourinho ameendelea kuvunja rekodi mbalimbali katika ulimwengu wa soka, baada ya kuwa ndio kocha pekee aliyechukuwa ubingwa ligi kuu za nchi nne tofauti kubwa barani ulaya na vilabu vya Porto, Chelsea, Inter Milan na Real Madrid.

Usiku wa kumakia leo Jose Mourinho alikiongoza kikosi chake cha Real Madrid kuwafunga mahasimu wao wakubwa FC Barcelona bao 2-1 kwenye mchezo wa pili wa kogembea kombe la Supercup kwenye uwanja wa Santiago Bernebeu. Kwa matokeo hayo timu hizo zikafunga kwa jumla ya mabao 4-4, lakini kutoka na Madrid kuwa na idadi kubwa ya magoli ya ugenini wakatwaa ubingwa huo wa tatu tangu Mourinho afike Bernebeu.


Kwa maana hiyo baada ya kufanikiwa kutwaa uchampion huo wa Supercup, Mourinho anaweka historia nyingine kubwa duniani akiwa ndio kocha pekee kuwahi kutwaa makombe ya ligi na supercup - (ambalo hukutanisha bingwa wa ligi na bingwa wa kombe la FA ya nchi husika -au mshindi wa pili wa ligi) katika nchi nne tofauti zilizo juu kwenye viwango vya FIFA - England alichukua EPL na Community shield, Ureno walifanya hivyo hivyo, Italia pia na sasa Spain. 

No comments:

Post a Comment