Tuesday, December 25, 2012

BOXING DEI: VINARA MAN UNITED OLD TRAFFORD, CITY, CHELSEA UGENINI!

BPL_LOGOMASHABIKI KUVAA KIVAZI CHA SANTA CLAUS!!
KWA MIAKA 3 SASA, TIMU INYOONGOZA XMASI NDIO BINGWA!!
Baada ya Sala na Shamrashamra za Krismasi, Ligi Kuu England Jumatano Desemba 26, Boxing Dei, itarindima kwenye Viwanja 9 na vinara Manchester United watakuwa kwao Old Trafford kuikaribisha Newcastle huku Timu zinazoifukuza, Mabingwa watetezi Man City wakiwa ugenini kucheza na Sunderland na Chelsea wapo huko Carrow Road kuivaa Norwich City.
+++++++++++++++++++++++
RATIBA:
Jumatano 26 Desemba 2012
[SAA 12 Jioni]
Arsenal v West Ham [IMEAHIRISHWA KUCHEZWA JANUARI]
Everton v Wigan
Fulham v Southampton
Man United v Newcastle
Norwich v Chelsea
QPR v West Brom
Reading v Swansea
Sunderland v Man City
[SAA 2 na Nusu Usiku]
Aston Villa v Tottenham
[SAA 4 Dak 45 Usiku]
Stoke v Liverpool
+++++++++++++++++++++++
Mechi moja, Arsenal v West Ham, iliyokuwa ichezwe Uwanjani Emirates imeahirishwa kutokana na mgomo wa Wafanyakazi wa Treni za Chini kwa Chini za Jiji la London, London Underground, hii ikiwa ni Mwaka wa Pili mfululizo Mechi ya Siku ya Boxing Dei kutochezeka Uwanjani Emirates kwa sababu hizo hizo.
Mbali ya mitanange ya Timu za kileleni, huko Mkiani Reading watawakaribisha Timu ngumu Swansea City ambao Juzi Jumapili waliibana Man United na kutoka nao 0-0 na QPR wako nyumbani kucheza na WBA.
Pengine Dondoo muhimu katika Kipindi hiki ni kuwa katika Misimu mitatu iliyopita Timu ambayo imekuwa ikiongoza Ligi wakati wa Krismasi iliendelea na kutwaa Ubingwa.
Mara ya mwisho kwa Timu kukaa kileleni wakati wa Krismasi na kuukosa Ubingwa ni Liverpool chini ya Rafael Benitez hapo Mwaka 2009 ambapo Man United ndio walimaliza Msimu wakiwa Mabingwa.
TATHMINI ZA MECHI, HALI ZA WACHEZAJI TUTARUSHA KESHO Jumatano Desemba 26.
+++++++++++++++++++++++
MSIMAMO:
=Tofauti ya Magoli inatajwa kwa Timu zilizofungana Pointi
1 Man United Mechi 18 Pointi 43
2 Man City Mechi 18 Pointi 39
3 Chelsea Mechi 17 Pointi 32
4 Arsenal Mechi 18 Pointi 30 [Tofauti ya Magoli 14]
5 Everton Mechi 18 Pointi 30 [Tofauti ya Magoli 8]
6 Tottenham Mechi 18 Pointi 30 [Tofauti ya Magoli 5]
7 WBA Mechi 18 Pointi 30 [Tofauti ya Magoli 4]
8 Liverpool Mechi 18 Pointi 25 [Tofauti ya Magoli 4]
9 Stoke Mechi 18 Pointi 25 [Tofauti ya Magoli 2]
10 Norwich Mechi 18 Pointi 25 [Tofauti ya Magoli -7]
11 Swansea Mechi 18 Pointi 24
12 West Ham Mechi 18 Pointi 23
13 Fulham Mechi 18 Pointi 20 [Tofauti ya Magoli -5]
14 Newcastle Mechi 18 Pointi 20 [Tofauti ya Magoli -6]
15 Sunderland Mechi 18 Pointi 19
16 Aston Villa Mechi 18 Pointi 18
17 Southampton Mechi 17 Pointi 15 [Tofauti ya Magoli -10]
===============
18 Wigan Mechi 18 Pointi 15 [Tofauti ya Magoli -15]
19 QPR Mechi 18 Pointi 10
20 Reading Mechi 18 Pointi 9
+++++++++++++++++++++++
MECHI ZIJAZO:
Jumamosi 29 Desemba 2012
[SAA 9 Dak 45 Mchana]
Sunderland v Tottenham
[SAA 12 Jioni]
Aston Villa v Wigan
Fulham v Swansea
Man United v West Brom
Norwich v Man City
Reading v West Ham
Stoke v Southampton
[SAA 2 na Nusu Usiku]
Arsenal v Newcastle
Jumapili 30 Desemba 2012
[SAA 10 na Nusu Jioni]
Everton v Chelsea
[SAA 1 Usiku]
QPR v Liverpool
Jumanne 1 Januari 2013
SAA 9 Dak 45 Mchana]
West Brom v Fulham
[SAA 12 Jioni]
Man City v Stoke
Swansea v Aston Villa
Tottenham v Reading
West Ham v Norwich
Wigan v Man United
[SAA 2 na Nusu Usiku]
Southampton v Arsenal
Jumatano 2 Januari 2013
[SAA 4 Dak 45 Usiku]
Chelsea v QPR
Liverpool v Sunderland
[SAA 5 Usiku]
Newcastle v Everton

No comments:

Post a Comment