Tuesday, December 25, 2012

BPL MECHI BOXING DEI: DONDOO MUHIMU MECHI ZA LEO

BPL_LOGOLEO huko England Mechi 9 za Ligi Kuu England zitachezwa na zifuatazo ni Taaarifa fupi kuhusu Hali za Wachezaji wa Kila Timu, Marefa wa Mechi za leo na Ratiba ya Mechi zijazo:

Jumatano Desemba 26
SAA 12 JIONI

EVERTON V WIGAN ATHLETIC
Kiungo wa Everton Darron Gibson anaweza kucheza Mechi hii licha ya kutolewa kwa Kadi Nyekundu kwenye Mechi na West Ham baada ya kukata Rufaa na sasa anasubiri isikilizwe hapo kesho lakini Everton watamkosa Marouane Fellaini anaetumikia Kifungo na hii ni Mechi ya pili kati ya 3 alizofungiwa.
Wigan watamkosa James McCarthy mwenye matatizo ya enka.
MECHI ILIYOPITA: West Ham 1 Everton 2, Wigan 0 Arsenal 1
Refa: Lee Mason
[Gemu: 11 Kadi za Njano: 36, Kadi Nyekundu: 0]
Wasaidizi: A Garratt & S Massey
Refa wa Akiba: M Oliver

MANCHESTER UNITED V NEWCASTLE UNITED
Kama kawaida, Bosi wa Manchester United Sir Alex Ferguson anatarajiwa kubadilisha Kikosi chake toka kile kilichotoka sare 1-1 na Swansea.
Javier Hernandez, Darren Fletcher na Danny Welbeck huenda wakaanza na Rafael huenda akapangwa baada ya kupona maumivu ya paja.
Newcastle United watamkosa Kiungo Chieck Tiote ambae amefungiwa Mechi moja baada ya kuzoa jumla ya Kadi za Njano 5.
Majeruhi watakaokosekana kwa Newcastle ni Hatem Ben Arfa, Steven Taylor, Yohan Cabaye na Ryan Taylor.
MECHI ILIYOPITA: Swansea 1 Man United 1, Newcastle 1 QPR 0
Refa: Mike Dean
[Gemu: 12, Kadi za Njano: 44, Kadi Nyekundu: 1]
Wasaidizi: J Collin & J Brooks
Refa wa Akiba: N Swarbrick

QUEENS PARK RANGERS V WEST BROMWICH ALBION
Kipa toka Brazil wa QPR, Julio Cesar, anaweza kupangwa baada ya kupona mgongo lakini Armand Traore, Nedum Onuoha, Park Ji-sung, Bobby Zamora na Andrew Johnson bado majeruhi.
Baada ya kutumikia Kifungo cha Mechi moja, Kiungo wa West Brom Youssouf Mulumbu ruksa kurejea Uwanjai lakini Claudio Yacob na Steven Reid bado majeruhi.
MECHI ILIYOPITA: West Brom 2 Norwich 1, Newcastle 1 QPR 0
Refa: Chris Foy
[Gemu: 12, Kadi za Njano: 20, Kadi Nyekundu: 0]
Wasaidizi: S Beck & H Lennard
Refa wa Akiba: A Davies

READING V SWANSEA CITY
Reading watawakosa Straika Jason Roberts, Sean Morrison na Alex McCarthy wote wakiwa majeruhi.
Swansea wanaweza kuwa nae Winga Pablo Hernandez aliezikosa Mechi 5 baada ya kuumia lakini Angel Rangel bado nje kwa maumivu.
MECHI ILIYOPITA: Swansea 1 Man United 1, Man City 1 Reading 0
Refa: Mike Jones
[Gemu: 11, Kadi za Njano: 41, Kadi Nyekundu: 1]
Wasaidizi: R Ganfield & M Wilkes
Refa wa Akiba: D Phillips

SUNDERLAND V MANCHESTER CITY
Winga wa Sunderland Adam Johnson yupo kwenye hatihati kucheza baada ya kuumia mguu Mechi iliyopita na pia upo wasiwasi kuhusu kucheza kwa Sebastian Larsson ambae ana maumivu ya goti.
Manchester City huenda wakawa nae Nahodha Vincent Kompany baada ya kupona nyonga na Mario Balotelli aliekuwa akiugua maradhi lakini upo wasiwasi kuhusu Aleksandar Kolarov na Gael Clichy, wenye maumivu, lakini Samir Nasri hatacheza kwa vile ni majeruhi.
MECHI ILIYOPITA: Southampton 0 Sunderland 1, Man City 1 Reading 0
Refa: Kevin Friend
[Gemu: 10, Kadi za Njano: 38, Kadi Nyekundu: 1]
Wasaidizi: A Halliday & G Beswick
Refa wa Akiba: K Wright

FULHAM V SOUTHAMPTON
Fulham hawana uhakika kuhusu kupona kwa Bryan Ruiz, Mahamadou Diarra na Mladen Petric.
Southampton watacheza bila ya Nahodha wao Adam Lallana ambae ni majeruhi.
MECHI ILIYOPITA: Southampton 0 Sunderland 1, Liverpool 3 Fulham 0
Refa: Phil Dowd
[Gemu: 12, Kadi za Njano: 34, Kadi Nyekundu: 2]
Wasaidizi: S Child & L Betts
Refa wa Akiba: D Coote

NORWICH CITY V CHELSEA
Norwich watawakosa majeruhi Steven Whittaker, John Ruddy, Andrew Surman na Ryan Bennett.
Kiungo wa Chelsea John Mikel Obi anaweza kurudi dimbani baada ya kumaliza Kifungo cha Mechi 3 lakini Nahodha John Terry na Ryan Bertrand bado majeruhi.
MECHI ILIYOPITA: West Brom 2 Norwich 1, Chelsea 8 Aston Villa 0
Refa: Jon Moss
[Gemu: 9, Kadi za Njano: 25, Kadi Nyekundu: 1]
Wasaidizi: P Kirkup & D Bryan
Refa wa Akiba: A Madley
Jumatano Desemba 26

SAA 2 na NUSU USIKU

ASTON VILLA V TOTTENHAM HOTSPUR
Majeruhi wa Aston Villa ni Ron Vlaar, Gabriel Agbonlahor, Charles Nzogbia na Darren Bent.
Wasiwasi wa Tottenham ni juu ya Straika Clint Dempsey lakini Benoit Assou-Ekotto na Scott Parker huenda wakaanzishwa baada ya kuwa fiti kutokana na maumivu yao ya muda mrefu.
MECHI ILIYOPITA: Chelsea 8 Villa 0, Tottenham 0 Stoke 0
Refa: Mark Clattenburg
[Gemu: 9, Kadi za Njano: 34, Kadi Nyekundu: 4]
Wasaidizi: S Ledger & M McDonough
Refa wa Akiba: A Taylor

Jumatano Desemba 26
SAA 4 DAKIKA 45 USIKU

STOKE CITY V LIVERPOOL
Straika wa Stoke Michael Owen, ambae amekuwa nje tangu Oktoba, huenda akaikabili Klabu yake ya zamani Liverpool.
Mchezaji mwingine wa zamani wa Liverpool, Peter Crouch, huenda nae akapata namba baada ya kupigwa Benchi hivi karibuni.
Liverpool huenda wakamwanzisha Raheem Sterling ambae alianzia Benchi katika Mechi iliyopita na Fulham.
Majeruhi pekee wa Liverpool ni Joe Allen.
MECHI ILIYOPITA: Tottenham 1 Stoke 1, Liverpool 3 Fulham 0
Refa: Howard Webb
[Gemu: 13, Kadi za Njano: 48, Kadi Nyekundu: 2]
Wasaidizi: S Burt & D England
Refa wa Akiba: D Drysdale
+++++++++++++++++++++++

MSIMAMO:

=Tofauti ya Magoli inatajwa kwa Timu zilizofungana Pointi
1 Man United Mechi 18 Pointi 43
2 Man City Mechi 18 Pointi 39
3 Chelsea Mechi 17 Pointi 32
4 Arsenal Mechi 18 Pointi 30 [Tofauti ya Magoli 14]
5 Everton Mechi 18 Pointi 30 [Tofauti ya Magoli 8]
6 Tottenham Mechi 18 Pointi 30 [Tofauti ya Magoli 5]
7 WBA Mechi 18 Pointi 30 [Tofauti ya Magoli 4]
8 Liverpool Mechi 18 Pointi 25 [Tofauti ya Magoli 4]
9 Stoke Mechi 18 Pointi 25 [Tofauti ya Magoli 2]
10 Norwich Mechi 18 Pointi 25 [Tofauti ya Magoli -7]
11 Swansea Mechi 18 Pointi 24
12 West Ham Mechi 18 Pointi 23
13 Fulham Mechi 18 Pointi 20 [Tofauti ya Magoli -5]
14 Newcastle Mechi 18 Pointi 20 [Tofauti ya Magoli -6]
15 Sunderland Mechi 18 Pointi 19
16 Aston Villa Mechi 18 Pointi 18
17 Southampton Mechi 17 Pointi 15 [Tofauti ya Magoli -10]
===============
18 Wigan Mechi 18 Pointi 15 [Tofauti ya Magoli -15]
19 QPR Mechi 18 Pointi 10
20 Reading Mechi 18 Pointi 9
+++++++++++++++++++++++

MECHI ZIJAZO:  
Jumamosi 29 Desemba 2012
[SAA 9 Dak 45 Mchana]
Sunderland v Tottenham
[SAA 12 Jioni]
Aston Villa v Wigan
Fulham v Swansea
Man United v West Brom
Norwich v Man City
Reading v West Ham
Stoke v Southampton
[SAA 2 na Nusu Usiku]
Arsenal v Newcastle
Jumapili 30 Desemba 2012
[SAA 10 na Nusu Jioni]
Everton v Chelsea
[SAA 1 Usiku]
QPR v Liverpool
Jumanne 1 Januari 2013
SAA 9 Dak 45 Mchana]
West Brom v Fulham
[SAA 12 Jioni]
Man City v Stoke
Swansea v Aston Villa
Tottenham v Reading
West Ham v Norwich
Wigan v Man United
[SAA 2 na Nusu Usiku]
Southampton v Arsenal
Jumatano 2 Januari 2013
[SAA 4 Dak 45 Usiku]
Chelsea v QPR
Liverpool v Sunderland
[SAA 5 Usiku]
Newcastle v Everton

No comments:

Post a Comment