Wednesday, December 26, 2012

VINARA MAN UNITED 7 MBELE, MABINGWA CITY WACHAPWA!!

CHELSEA WASHINDA, WAINYEMELEA CITY!!
 
BPL_LOGOLEO MABINGWA WATETEZI wa Ligi Kuu England, Manchester City ambao wako nafasi ya pili, wamechapwa Bao 1-0 na Sunderland huko Stadium of Light, kwa Bao la Mchezaji wao wa zamani Adam Johnson, na kuwatupa Pointi 7 nyuma ya vinara Manchester United, ambao leo waliifunga Newcastle Bao 4-3 Uwanjani Old Trafford baada ya kuwa nyuma mara 3 na Bao la ushindi kufungwa Dakika ya 90 na Chicharito huku Chelsea wakiitungua Norwich City kwa Bao 1-0 na kujizatiti nafasi ya 3 wakiwa Pointi 4 nyuma ya City huku wakiwa na Mechi 1 mkononi.
+++++++++++++++++++++++
MATOKEO/RATIBA:
Jumatano 26 Desemba 2012
Everton 2 Wigan 1
Fulham 1 Southampton 1
Man United 4 Newcastle 3
Norwich 0 Chelsea 1
QPR 1 West Brom 2
Reading 0 Swansea 0
Sunderland 1 Man City 2
[SAA 2 na Nusu Usiku]
Aston Villa v Tottenham
[SAA 4 Dak 45 Usiku]
Stoke v Liverpool
+++++++++++++++++++++++
MAN UNITED 4 NEWCASTLE 3
Manchester United leo wameifunga Newcastle Bao 4-3 Uwanjani Old Trafford baada ya kutoka nyuma mara 3 na sasa wapo kileleni mwa Ligi Kuu England wakiwa Pointi 7 mbele.CHICHARITO_SHANGILIA
=================
MAGOLI:
Man United 4
-Evans Dakika ya 25
-Evra 58
-Van Persie 71
-Hernandez 90
Newcastle 3
-Perch Dakika ya 4
-Evans 28 [Kajifunga mwenyewe]
-Cisse 68
=================
Bao la ushindi kwa Manchester United lilifungwa na Javier Hernandez ‘Chicharito’ katika Dakika ya 90 baada ya pasi murua ya Michael Carrick.
Mechi hii iligubikwa na utata mkubwa kuhusu Bao la Pili la Newcastle ambalo awali lilikataliwa baada ya Refa Msaidizi kutoa ishara ya Kibendera kuwa Demba Ba alikuwa ameotea ingawa Bao hili lilikuwa la kujifunga mwenyewe Evans.
VIKOSI:
Man United: De Gea, Smalling, Ferdinand, Evans, Evra, Valencia, Carrick, Scholes, Giggs, van Persie, Hernandez
Akiba: Lindegaard, Vidic, Cleverley, Fletcher, Buttner, Wootton, Tunnicliffe.
Newcastle: Krul, Simpson, Williamson, Coloccini, Santon, Anita, Perch, Bigirimana, Cisse, Ba, Marveaux
Akiba: Elliot, Shola Ameobi, Obertan, Sammy Ameobi, Ferguson, Tavernier, Campbell.
Refa: Mike Dean
SUNDERLAND 1 MAN CITY 0
Winga wa zamani wa Mabingwa Manchester City, Adam Johnson, leo aliifungia Sunderland Bao moja, pekee na la ushindi, dhidi ya Timu yake ya zamani ilipozamishwa Bao 1-0 huko Stadium of Light na kuwatupa Mabingwa hao Pointi 7 nyuma ya vinara Man United wakiwa nafasi ya pili.
VIKOSI:
Sunderland: Mignolet, Gardner, Rose, Kilgallon, Cuellar, Larsson, Colback, Johnson, McClean, Sessegnon, Fletcher
Akiba: Bardsley, Campbell, Wickham, McFadden, Vaughan, Bramble, Westwood.
Manchester City: Hart, Kompany, Zabaleta, K Toure, Nastasic, Y Toure, Garcia, Silva, Milner, Aguero, Tevez
Akiba: Pantilimon, Lescott, Rekik, Barry, Razak, Sinclair, Dzeko.
Refa: Kevin Friend
EVERTON 2 WIGAN 1
Everton leo wameendeleza wimbi lao la kutofungwa katika Mechi 7 za Ligi baada ya Magoli ya Leon Osman na Phil Jagielka kuwapa ushindi wa 2-1 dhidi ya Wigan Uwanjani Goodison Park.
Bao la Wigan lilifungwa na Arouna Kone.
Bao la pili la Everton lilizalishwa na Nahodha wao Phil Neville ambae leo alikuwa akicheza Mechi yake ya 500 kwenye Ligi.
Ushindi wa leo umewapaisha Everton hadi nafasi ya 4 wakiwa Pointi 2 tu nyuma ya Chelsea ambao watacheza nao Uwanjani Goodison Park hapo Jumapili.
VIKOSI:
Everton: Howard, Neville, Jagielka, Distin, Baines, Osman, Hitzlsperger, Gibson, Pienaar, Jelavic, Anichebe
Akiba: Mucha, Heitinga, Oviedo, Naismith, Gueye, Barkley, Vellios.
Wigan: Al Habsi, Boyce, Caldwell, Figueroa, Stam, McCarthy, Jones, McArthur, Beausejour, Maloney, Kone
Akiba: Pollitt, Di Santo, Gomez, McManaman, Boselli, Ramis, Golobart.
Refa: Lee Mason
QPR 1 WEST BROM 2
Ushindi kwa West Brom wa Bao 2-1 umewazamisha QPR hadi mkiani mwa Msimamo wa Ligi Kuu England.
Bao za WBA zilifungwa na Chris Brunt na la pili ni la kujifunga wenyewe QPR baada Kipa Robert Green kuutumbukiza mpira wavuni mwenyewe ingawa ilionekana wazi Kipa huyo alikuwa kabanwa na Marc Antoine-Fortune na halikustahili kuhesabiwa Goli halali.
Bao la QPR lilifungwa na Djibril Cisse.
VIKOSI:
QPR: Green, Da Silva, Ferdinand, Hill, Traore, Mbia, Faurlin, Mackie, Taarabt, Wright-Phillips, Cisse
Akiba: Julio Cesar, Diakite, Derry, Granero, Dyer, Hoilett, Ehmer.
West Brom: Foster, Jones, McAuley, Olsson, Popov, Mulumbu, Morrison, Fortune, Gera, Brunt, Lukaku
Akiba: Myhill, Ridgewell, Rosenberg, Long, Dorrans, Odemwingie, Tamas.
Refa: Chris Foy
NORWICH 0 CHELSEA 1
Bao tamu la Juan Mata limewafikisha Chelsea, ambao wako nafasi ya 3, kuwa Pointi 4 tu nyuma ya Manchester City ambao wako nafasi ya pili na kuwapa kipigo cha pili mfululizo Norwich.
Chelsea wamecheza Mechi moja pungufu.
VIKOSI:
Norwich: Bunn, Martin, Turner, Bassong, Garrido, Snodgrass, Tettey, Johnson, Pilkington, Hoolahan, Holt
Akiba: Rudd, Howson, Jackson, Morison, Elliott Bennett, Barnett, Ryan Bennett.
Chelsea: Cech, Azpilicueta, Ivanovic, Cahill, Cole, Mikel, Luiz, Moses, Oscar, Mata, Torres
Akiba: Turnbull, Lampard, Hazard, Ferreira, Marin, Piazon, Ake.
Refa: Jon Moss
READING 0 SWANSEA 0
Sare ya 0-0 na Swansea City Uwanjani Madejski leo imewanasua Reading toka mkiani kwenye Ligi Kuu England.
Licha ya sare hiyo, Swansea City pia wamekumbwa na wasiwasi baada ya Straika wao mkuu Michu, ambae ndie amefungana na Robin van Persie wa Man United kama Wafungaji Bora wa Ligi wote wakiwa na Goli 13 kila mmoja, kutolewa nje wakati wa Mechi akiwa anachechemea.
VIKOSI:
Reading: Federici, Gunter, Pearce, Mariappa, Harte, Kebe, Leigertwood, Karacan, McAnuff, Guthrie, Pogrebnyak
Akiba: Taylor, Le Fondre, Hunt, Morrison, Tabb, Robson-Kanu, Cummings.
Swansea: Vorm, Tiendalli, Chico, Williams, Davies, Dyer, Britton, Ki, Moore, Routledge, Michu
Akiba: Tremmel, Bartley, Graham, Monk, Shechter, de Guzman, Agustien.
Refa: Mike Jones
FULHAM 1 SOUTHAMPTON 1
Penati ya Dakika za mwishoni ya Rickie Lambert imewapa Southampton sare ya 1-1 walipocheza ugenini Uwanjani Craven Cottage walipocheza na Fulham ambao Bao lao lilifungwa na Dimitar Berbatov aliesheherekea Bao hilo kwa kuvua Jezi yake na kuonyesha Tisheti iliyoandikwa: ‘TULIZA BOLI, MUWE MNANIPASIA MIMI MPIRA!’
VIKOSI:
Fulham: Schwarzer, Riether, Hangeland, Senderos, Riise, Dejagah, Sidwell, Baird, Kacaniklic, Berbatov, Rodallega
Akiba: Stockdale, Kelly, Ruiz, Karagounis, Briggs, Hughes, Frei.
Southampton: Kelvin Davis, Clyne, Fonte, Yoshida, Shaw, Schneiderlin, Cork, Steven Davis, Puncheon, Ramirez, Lambert
Akiba: Boruc, Hooiveld, Rodriguez, Ward-Prowse, Do Prado, Richardson, Mayuka.
Refa: Phil Dowd
+++++++++++++++++++++++
MECHI ZIJAZO:
Jumamosi 29 Desemba 2012
[SAA 9 Dak 45 Mchana]
Sunderland v Tottenham
[SAA 12 Jioni]
Aston Villa v Wigan
Fulham v Swansea
Man United v West Brom
Norwich v Man City
Reading v West Ham
Stoke v Southampton
[SAA 2 na Nusu Usiku]
Arsenal v Newcastle
Jumapili 30 Desemba 2012
[SAA 10 na Nusu Jioni]
Everton v Chelsea
[SAA 1 Usiku]
QPR v Liverpool
Jumanne 1 Januari 2013
SAA 9 Dak 45 Mchana]
West Brom v Fulham
[SAA 12 Jioni]
Man City v Stoke
Swansea v Aston Villa
Tottenham v Reading
West Ham v Norwich
Wigan v Man United
[SAA 2 na Nusu Usiku]
Southampton v Arsenal
Jumatano 2 Januari 2013
[SAA 4 Dak 45 Usiku]
Chelsea v QPR
Liverpool v Sunderland
[SAA 5 Usiku]
Newcastle v Everton

No comments:

Post a Comment