Monday, December 24, 2012

Fergie: RVP analeta matokeo kama Cantona!

>>ADAI: ‘KUTUA RVP OLD TRAFFORD NI ZAWADI YA MAPEMA YA X-MAS!’

ERIC_CANTONAKUTUA kwa Robin van Persie Manchester United kumeleta matokeo na mabadiliko kama yale yaliyoletwa na ujio wa ‘Mfalme’ Eric Cantona Klabuni hapo Mwaka 1992 wakati alipoiwezesha kutwaa Ubingwa wao wa kwanza baada ya Miaka 26 na kufananishwa kwa Magwiji hao wawili kumetolewa na Meneja wao Sir Alex Ferguson.
Tangu Robin van Persie atue Old Trafford Mwezi Agosti akitokea Arsenal ameshafunga Mabao 15 na Ferguson ametamka: “Nadhani Klabuni hapa tulipata zawadi yetu ya Krismasi mapema baada ya Robin van Persie kutua Old Trafford!”
Ferguson amesema yeye si muumini wa kuhusudu Mtu binafsi kwani anaamini katika Soka Timu bora hutokana na kucheza Kitimu na Man United si Timu ya kutegemea Mtu mmoja lakini amekubali kuna wakati Mtu mmoja huleta mabadiliko.
Amesema: “Kuna wakati una bahatika na Mtu mmoja husukuma mafanikio makubwa!”
Mwaka 1992, Eric Cantona alisainiwa kutoka Leeds United kwa Dau la Pauni Milioni 1.2 huku Timu ikiwa nafasi ya 8 lakini akitumia kipaji chake, ubishi na mvuto wake aliiwezesha Man United kutwaa Ubingwa Mwaka 1993 wakiwa Pointi 10 mbele na hilo lilikuwa ndio Taji la Kwanza la Sir Alex Ferguson katika Mataji 12 ya Ubingwa wa England ambayo ametwaa katika himaya yake.
Ferguson ametamka: “Tuliweza tulipomleta Cantona. Alikuwa Mchezaji safi kwa wakati muafaka kwa Klabu na alileta mabadiliko na mafanikio!”
Akishirikiana na Wayne Rooney katika mashambulizi, Robin van Persie ameiwezesha Man United ikae kileleni mwa Ligi Kuu England wakiwa Pointi 4 mbele ya Man City ambao Msimu uliopita walitwaa Ubingwa kwa tofauti ya Magoli tu baada ya kufungana Pointi na Man United.
+++++++++++++++++++++++
RATIBA=LIGI KUU ENGLAND:
Jumatano 26 Desemba 2012
[SAA 12 Jioni]
Arsenal v West Ham [IMEAHIRISHWA KUCHEZWA JANUARI]
Everton v Wigan
Fulham v Southampton
Man United v Newcastle
Norwich v Chelsea
QPR v West Brom
Reading v Swansea
Sunderland v Man City
[SAA 2 na Nusu Usiku]
Aston Villa v Tottenham
[SAA 4 Dak 45 Usiku]
Stoke v Liverpool
+++++++++++++++++++++++
MSIMAMO:
=Tofauti ya Magoli inatajwa kwa Timu zilizofungana Pointi
1 Man United Mechi 18 Pointi 43
2 Man City Mechi 18 Pointi 39
3 Chelsea Mechi 17 Pointi 32
4 Arsenal Mechi 18 Pointi 30 [Tofauti ya Magoli 14]
5 Everton Mechi 18 Pointi 30 [Tofauti ya Magoli 8]
6 Tottenham Mechi 18 Pointi 30 [Tofauti ya Magoli 5]
7 WBA Mechi 18 Pointi 30 [Tofauti ya Magoli 4]
8 Liverpool Mechi 18 Pointi 25 [Tofauti ya Magoli 4]
9 Stoke Mechi 18 Pointi 25 [Tofauti ya Magoli 2]
10 Norwich Mechi 18 Pointi 25 [Tofauti ya Magoli -7]
11 Swansea Mechi 18 Pointi 24
12 West Ham Mechi 18 Pointi 23
13 Fulham Mechi 18 Pointi 20 [Tofauti ya Magoli -5]
14 Newcastle Mechi 18 Pointi 20 [Tofauti ya Magoli -6]
15 Sunderland Mechi 18 Pointi 19
16 Aston Villa Mechi 18 Pointi 18
17 Southampton Mechi 17 Pointi 15 [Tofauti ya Magoli -10]
===============
18 Wigan Mechi 18 Pointi 15 [Tofauti ya Magoli -15]
19 QPR Mechi 18 Pointi 10
20 Reading Mechi 18 Pointi 9
+++++++++++++++++++++++
MECHI ZIJAZO:
Jumamosi 29 Desemba 2012
[SAA 9 Dak 45 Mchana]
Sunderland v Tottenham
[SAA 12 Jioni]
Aston Villa v Wigan
Fulham v Swansea
Man United v West Brom
Norwich v Man City
Reading v West Ham
Stoke v Southampton
[SAA 2 na Nusu Usiku]
Arsenal v Newcastle
Jumapili 30 Desemba 2012
[SAA 10 na Nusu Jioni]
Everton v Chelsea
[SAA 1 Usiku]
QPR v Liverpool
Jumanne 1 Januari 2013
SAA 9 Dak 45 Mchana]
West Brom v Fulham
[SAA 12 Jioni]
Man City v Stoke
Swansea v Aston Villa
Tottenham v Reading
West Ham v Norwich
Wigan v Man United
[SAA 2 na Nusu Usiku]
Southampton v Arsenal
Jumatano 2 Januari 2013
[SAA 4 Dak 45 Usiku]
Chelsea v QPR
Liverpool v Sunderland
[SAA 5 Usiku]
Newcastle v Everton

No comments:

Post a Comment