Mshambuliaji
wa Real Madrid Cristiano Ronaldo amesisitiza kwamba hatoweza
kushangilia ikiwa atafunga katika hatua ya 16 ya UEFA Champions league
dhidi ya Manchester United.
Nahodha
huyo wa Ureno ambaye alicheza kwa mafanikio makubwa akiwa na United
katika kipindi cha miaka 6 kabla ya kuondoka na kujiunga Los Blancos
katika kipindi cha kiangazi mwaka 2009 kwa ada iliyovunja rekodi ya
dunia ya £80 million.
"Sitoshangilia goli nikiweza kufunga dhidi ya Man United," Ronaldo alikaririwa akisema siku ya alhamisi na mtandao wa AS.
Ronaldo,
27, hivi karibuni alielezea hisia zake juu ya kocha wa Manchester United
na kusema kocha huyo raia wa Scotland amecheza part kubwa katika
kumfanya mchezaji ambaye alivyo sasa.
"Ferguson ni mtu mzuri sana. Mwanadamu mwema. Amenifundisha vitu vingi," Ronaldo aliiambia The Sun.
"Kama nilivyosema huko nyuma, Fergie ni kama baba yangu kwenye soka. Nammisi sana yeye na mahusiano tuliyokuwa nayo."
No comments:
Post a Comment