Saturday, June 1, 2013

RADAMEL FALCAO: RASMI ASAINIWA NA MONACO!

RADAMEL_FALCAO2Monaco wamekamilisha Uahamisho wa Dau la Pauni Milioni 50 wa kumchukua Straika wa Atletico Madrid Radamel Falcao.
 
Falcao, Raia wa Colombia mwenye Miaka 27, amekuwa pia akihusishwa na kuhamia Chelsea na Manchester City.

FALCAO-WASIFU:
 

-KUZALIWA: 10 Februari 1986

-URAIA: Colombia

-KLABU: River Plate (2005-2009); Porto (2009-2011) & Atletico Madrid (2011-2013)

-ATLETICO MADRID: Mechi 46 Magoli 35

-JE WAJUA? Falcao ndie Mchezaji wa kwanza kwenye UEFA SUPER CUP kupiga

Hetitriki Mwezi Septemba Mwaka jana Atletico Madrid walipoinyuka Chelsea 4-1.



Falcao amesaini Mkataba wa Miaka mitano na Monaco na usajili huo umelipiwa na Mmiliki wa Klabu hiyo, Dmitry Rybolovlev, Bilionea kutoka Urusi.
 
Akitangaza usajili huo, Rybolovlev alisema: “Ni fahari kubwa kumsaini mmoja wa Wachezaji bora Duniani na tuna imani ataisaidia Monaco!”

Wakiwa chini ya Kocha Claudio Ranieri, Msimu huu uliokwisha juzi waliibuka Mabingwa wa Daraja la Pili huko France na Msimu ujao watacheza Daraja la juu Ligue 1 na hali hiyo imewafanya waimarishe Kikosi chao na tayari wameshawasajili Wachezaji wawili hatari toka FC Porto, Joao Moutinho, Miaka 26, na James Rodriguez, Miaka 21, na pia Beki Mkongwe kutoka Real Madrid, Ricardo Carvalho, ambae amehamishwa bure baada kumaliza Mkataba wake.

No comments:

Post a Comment