Sunday, June 2, 2013

BAYERN YATWAA GERMAN DFB POKAL, YAWEKA REKODI!

BAYERN MUNICH 3 STUTTGART 2
BAYERN_MUNICH_LOGO


Mario Gomez alipiga Bao mbili na kuifanya Bayern Munich kuweka Historia ya kuwa Klabu ya kwanza ya Germany kutwaa ‘Trebo’ yaani, Ubingwa wa Nchi, Kombe la Nchi, hili DFB POKAL, na ule Ubingwa wa Ulaya, UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI kwenye Msimu mmoja, walipoifunga VfB Stuttgart 3-2 huko Berlin.

Hiyo ilikuwa Mechi ya mwisho kwa Kocha wa Bayern Jupp Heynckes ambae anastaafu na nafasi yake kuchukuliwa na aliekuwa Kocha wa FC Barcelona Pep Guardiola.

Mbali ya Bao 2 za Mario Gomez, Bao la kwanza la Bayern lilifungwa na Penati ya Thomas Mueller.


HISTORI:

-Bayern ni Timu ya kwanza ya Germany kutwaa Trebo ndani ya Msimu mmoja.

-Bayern inakuwa Klabu ya 7 Barani Ulaya kutwaa Trebo nyingine ni Celtic Mwaka 1967, Ajax 1972, PSV Eindhoven 1988, Manchester United 1999, Barcelona 2009 na Inter Milan hapo 2010.

**FAHAMU:
 Trebo ni kutwaa Ubingwa wa Ligi, Kombe kubwa la Nchi na Kombe la Ubingwa wa Ulaya ndani ya Msimu mmoja

 Bao za Stuttgart zilifungwa na Martin Harnick.

Huu ni ushindi wa 15 katika Mechi 16 walizocheza mwisho Bayern Munich na kipigo chao cha mwisho walikipata Oktoba Mwaka jana.

No comments:

Post a Comment