Monday, December 31, 2012

MABINGWA MAN CITY WAHAHA KUSAINI WAPYA JANUARI, BA ALETA BALAA!!

>>CITY WAIKUBALI NYEKUNDU YA NASRI, KUIKOSA ARSENAL!
>>PARDEW ALIA NA WASHIRIKA WA DEMBA BA!!

MANCINI_n_MICAHMABINGWA wa England, Manchester City, wamedokeza kuwa upo uwezekano wa kusaini Wachezaji wapya Mwezi Januari na pia wamethibitisha kutokata Rufaa kuipinga Kadi Nyekundu ya Mchezaji wao Samir Nasri aliyopewa Juzi na huko Klabuni Newcastle, Meneja Alan Pardew, amelalamika kuhusu Washirika wa Straika wake Demba Ba ambae imetobolewa anasaka Klabu mpya Mwezi Januari.

MAN CITY
Meneja wa Manchester City Roberto Mancini amedokeza kuwa athari za kuwakosa Wachezaji wao, watakaokwenda kucheza AFCON 2013 na pia kuwa majeruhi, itawalazimisha kuingia Sokoni Mwezi Januari Dirisha la Uhamisho litakapofunguliwa ili kuimarisha Kikosi chao.

Mancini amethibitisha Mwezi Januari watawakosa Wachezaji watatu walioitwa kuichezea Ivory Coast kwenye AFCON 2013 ambao ni Yaya Toure, Kolo Toure na Abdul Razak, na pia inao majeruhi Micah Richards, JackRodwell, Aleksandar Kolarov na Maicon.

WAKATI HUO HUO, Man City imethibitisha haitakata Rufaa kupinga Kadi Nyekundu ya Mchezaji wao Samir Nasri aliyopewa Jumamosi huko Carrow Road wakati City ilipoifunga Norwich 4-3 kwa kumpiga kichwa Sebastien Bassong.

Mara baada ya uamuzi wa Man City, FA imetangaza kuwa Nasri atazikosa Mechi 3 ambazo ni za Ligi dhidi ya Stoke City Januari 1, FA CUP na Watford Januari 5 na ile ya Ligi ugenini na Arsenal hapo Januari 13.

PARDEW na BA
BOSI wa Newcastle Alan Pardew amewashambulia Washirika wa Demba Ba kwa kumshauri vibaya Straika huyo kutoka Senegal ambae juzi waliripotiwa kufanya mazungumzo na Chelsea kuhusu kuhama kwake lakini makubaliano hayakufikiwa.

Pardew amesema : “Kwa namna fulani, namsikitikia Demba kwani nadhani amezungukwa na Watu ambao si Wakilishi wake na wamekua wakisema hili na lile!”

Kwa Miezi kadhaa sasa, Newcastle imekuwa ikijitahidi kumpa Mkataba mpya Demba Ba ambao pia utaondoa Kipengele cha sasa kuwa anaweza kuuzwa wakati wowote ikiwa Malipo ya Pauni Milioni 7.5 yatatolewa.

No comments:

Post a Comment